Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania (TMA) yatahadharisha ujio wa ukame, njaa

Habari wanajamii hakika kila MTU anaweza kukubaliana nami kuwa hali ya nchi yetu sio nzuri has a kwa kutawala ukame sehemu kubwa na hali ngumu ya maisha inayotukabili. Najiuliza maswali machache kuwa tumekosea wapi?. Ndio nikapata jibu langu kuwa je ni vile tulimkataa Musa 2015 aliyetuahidi kutupeleka nchi ya ahadi? Tukang'ang'ania nyama za utumwani..?? Au safari tumeanza ya miaka 40 ya mateso ili tufikie nchi ya ahadi.?? Naomba kuwasilisha wadau???

Sent from my TECNO-L5 using JamiiForums mobile app
 
Hapa Morogoro Ng'ombe Wamekonda Sana Kwa Uhaba Wa Marisho Na Kiu Ya Maji Baadhi Ya Mifugo Inajifia Yenyewe Pia Ng'ombe Hawauzwi Bei Juu Tena Maana Wamekonda Sana.

Kwenye tafsiri ya kiroho ina maana gani?
Je ni ile peku peku ya Nabii mwenye mbawa?
Je ni lile bao la mkono?
Je ni dhikaha ya kutaka kuombewa?
Ukiandika sana unaweza kujikuta shimo la tewa hapa ndani au kule nje!
mkuu,kuna watu zikiletwa habari kama hizi wanaamini ni uchochezi wa wapinzani ili kumkomoa jamaaa
 
Hapa Morogoro Ng'ombe Wamekonda Sana Kwa Uhaba Wa Marisho Na Kiu Ya Maji Baadhi Ya Mifugo Inajifia Yenyewe Pia Ng'ombe Hawauzwi Bei Juu Tena Maana Wamekonda Sana.
huyo mkuu wa mkoa kama ameshindwa kazi aseme au tumtumbue,maana haiwezekani wana inchi walioumbwa kwa mfano wa mungu wanyama wao wafe alafu yeye uko kwa ofsi tuu
 
"....Akizungumza na wanahabari leo, Dk. Agness Kijazi, Mkurugenzi Mkuu wa TMA amesema, kutokana na kukosekana kwa mvua kati ya Desemba na Oktoba mwaka huu katika maeneo mengi ya nchi, migogoro baina ya wakulima na wafugaji pia itaongezeka...."

Naamini usahihi ilitakiwa kuwa ".....kati ya Oktoba na Desemba..." badala ya Desemba na Oktoba.
 
huyu atimuliwe kama yule wa ZIKA

taarifa yake haijapitishwa na wizara
 
Ajiangalia vyema au muda si mrefu anatumbuliwa maana yule Mfalme wa Nchi ni habari nyingine hapendi ukweli, ila anahubiri msema kweli ni mpenzi wa Mungu mniombee!! Kijazi kaa mguu sawa!
 
Mkurugenzi huyu wa mamlaka ya hali ya hewa katulia kabisaaa,hatutabirii tena mvua itanyesha wapi na lini.

Ni mmoja wa akina mama ambao kwa kweli taifa linajivunia kuwa nao.

Sasa sijui anahofia nini kutangaza hali ya mvua,hata kama vipimo vinasema itanyesha mwezi wa nane aseme tu

Au naye kashikwa hofu baada ya wakurugenzi wenzie Mafuru na dk. Mwele kufurumushwa?
 
Huku site niliko hali ni mbaya kupita maelezo,mvua hakuna na bahati mbaya miti ya mkaa nayo imeisha sijui wenyeji wataishije mwaka huu
 
Mkurugenzi huyu wa mamlaka ya hali ya hewa katulia kabisaaa,hatutabirii tena mvua itanyesha wapi na lini.

Ni mmoja wa akina mama ambao kwa kweli taifa linajivunia kuwa nao.

Sasa sijui anahofia nini kutangaza hali ya mvua,hata kama vipimo vinasema itanyesha mwezi wa nane aseme tu

Au naye kashikwa hofu baada ya wakurugenzi wenzie Mafuru na dk. Mwele kufurumushwa?
Kwa nini mnapenda kusikia mambo mabaya mabaya kuhusu nchi yenu.?

Toa Suluhu jinsi ya kukabiliana na balaa la njaa kwa kuwashauri wakulima pamoja na kulima mahindi walime na baadhi ya mazao yanayohimili ukame.

Au shauri serikali iongeze nguvu kuwasaidia wakulima wanaotaka kulima kilimo cha kisasa sio cha kutegemea msimu.

Unalamisha atangaze hali mbaya, kwa hiyo akitangaza ndio hali itabadilika.? Rais amesema yeye ndio anajua wapi kuna njaa wapi hakuna njaa.

Hamuwezi kuingia Ikulu kwa siasa za chuki namna hii huku mkijifanya mnauchungu na wananchi kumbe mnatafuta umaarufu wa kisiasa.
 
Mkurugenzi huyu wa mamlaka ya hali ya hewa katulia kabisaaa,hatutabirii tena mvua itanyesha wapi na lini.

Ni mmoja wa akina mama ambao kwa kweli taifa linajivunia kuwa nao.

Sasa sijui anahofia nini kutangaza hali ya mvua,hata kama vipimo vinasema itanyesha mwezi wa nane aseme tu

Au naye kashikwa hofu baada ya wakurugenzi wenzie Mafuru na dk. Mwele kufurumushwa?
mvua ina nyesha MOSHI, SHINYANGA.MBEYA,njOMBE,mtwara,lindi ,kigoma.n.k
 
Back
Top Bottom