Nanaado1010
New Member
- May 14, 2021
- 1
- 5
Nampongeza Mheshimiwa Raisi Mama Samia kwa uteuzi wa ndugu Ishmael Andulile kuwa mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TADB. Pamoja na pongezi hizo ninakuomba mheshimiwa Raisi utupie jicho nafasi ya Mkurugenzi Mtendaji kwani Ndugu Japhet Justine sio mtu sahihi kwa sababu zifuatazo:-
1. MATUMIZI MABAYA YA MADARAKA
1. MATUMIZI MABAYA YA MADARAKA
- Hivi karibuni alinunua gari binafsi kwa mkopo wa Benki ambao kwa mujibu wa kanuni na taratibu za mikopo kwa wafanyakazi, mkopo wake ungetakiwa kuidhinishwa na mamlaka yake ya uteuzi lakini hilo halikufanyika na mbaya zaidi alitumia nafasi yake kulipiwa kodi ya gari husika na Benki ya zaidi ya milioni ishirini fedha ambazo angepaswa kulipa mwenyewe. Ninakuomba utumie vyombo vyako kufuatilia hili.
- Amehamia kwenye nyumba ambayo Benki inamlipia zaidi ya Tsh.6,000,000.00 kwa mwezi ambapo stahiki yake ya posho ya nyumba ni 15% ya mshahara wake wa mwezi na nina uhakika haiwezi kufika kiasi hicho. Nyumba aliyokuwa anakaa awali ilikuwa inalipiwa Tsh.2,3000,000.00 na haikuwa na tatizo lolote. Ikumbukwe kwamba mwaka 2020 alikuwa na kesi TAKUKURU kinondoni kwa kufanya ukarabati bila kufuata taratibu za mananuzi kwenye nyumba hiyo aliyohama cha ajabu kesi ile ilifutwa kwa amri kutoka juu na wale maofisa kuchukuliwa hatua kwa sababu aliwasingizia kwamba walikuwa wanamwomba rushwa. Ninaomba ufuatilie ukweli wa hili jambo na wale maofisa wapate haki yao.
- Kukiuka taratibu za manunuzi. Imekuwa ni jambo la kawaida. Tender yeyote amabayo mzabuni amepatika na hana maslahi nae lazima ifutwe. Hi imepelekea kitengo cha manunuzi kushidwa kutekeleza wajibu wake inavyopaswa. Wakati anajiunga na Benki miaka mitatu iliyopita kitengo hicho kilikuwa na wafanyakazi wanne leo kinamfanyakazi mmoja tuu. Wengine wote wameondoka kwa sababu za kutakiwa kufanya kazi kwa matakwa yake binafsi.
2. KUSHIDWA KUSIMAMIA SWALA LA RASILIMALI WATU KWA MUJIBU WA SHERIA NA TARATIBU - Upendeleo wa wazi katika kupandisha wafanyakazi madaraja na mishahara. Hakuna vigezo vinavyoeleweka katika hili.Hata asiyefikisha miaka mitatu anapandishwa ilimradi tuu ni mtu wake.Hili ni tatizo kubwa sana na linaadhiri sana mahusiano ya wafanyakazi kwani ni chanzo cha makundi. Hivi karibun tuu amefanya hivyo.
- Kufukuza kazi wafanyakazi bila sababu za msingi na bila kufuata taratibu.Kesi za kutosha zipo Utumishi. Hili ni tatizo tangu ajiunge na Benki Benki imeshapoteza wafanyakazi zaidi ya 30 idadi hii ni kubwa mno kwa Benki yenye wafantakazi wasiozidi 70.
- Matusi, Vitisho, Kejeli na dharau kwa wafanyakazi. Haya anayaonyesha waziwazi hata kwenye vikao na kujinasibu kwamba yeye ndo menyeakili kuliko watu wote ndiyo maana Hayati John Pombe Magufuli alimteua kuongoza Benki hiyo na anaheshimu uwezo wake.Hili limepelekea kila uchao wafanyakazi kuacha kazi. Kwa mfano tangu mwaka huu uanze wameshaacha wafanyakazi 05.
- Swala la uhamisho wa wafanyakazi kwenda ofisi za kanda kutokea Dar limekuwa likitumiwa kama adhabu jambo ambalo sio sahihi hata kidogo. Yeyote anayetofautiana nae kimtazamo anahamishwa Katavi/Mbeya kama adhabu.
- Amekuwa akiajiri wafanyakazi bila kufuata taratibu za ajira kwa watumishi wa umma.Hili limepelekea kuwa na watumishi wasio na sifa stahiki hasa kwenye ngazi za juu. Amekuwa akifanikisha hili kwa kushirikiana na baadhi ya viongozi wa BOT. Wanatoa vetting safi hata kama mtu hana sifa kwa mujibu wa miongozo.
- Anatumia kigezo cha poor perfomance kuwafukuza watu kazi lakini ukiangalia kwa undani hamna ukweli wowote kwani vigezo vya perfomance mpaka sasa ni kitendawili. UNAGUNDUA tuu kwamba kama mtu hampelekei majungu na umbea anakuwa poor performer.
3. UPENDELEO KATIKA KUTOA MIKOPO - Zaidi ya 60% ya mikopo ya Benki imetolewa kanda ya ziwa na mingi haina tija.Hili lilifanyika kwa sababu ambazo sitaki kuzielezea hapa. Kwa sasa inatafutwa miradi kwa udi na uvumba kuelekea kanda ya kaskazini hasa wiliya moja ambapo anatoka moja ya mawaziri wa serikali ya awamu ya sita. HILI sio sawa kwa sababu linaleta ubaguzi kwa wananchi kwa kigezo cha kanda wanazotoka na lengo la kuanzishwa kwa Benki ni kwa kuwahudumia wananchi wote.
- Kunabadhi ya mawaziri na wenza wao ambao wamekopeshwa au wanakaribia kukopeshwa na Benki. Ninaomba ulitizame hili kwani wanatumia nafasi zao na ukaribu walionao na Bwana Japhet Justine kulifanikisha hili.Mikopo hiyo itakuja kugeuka kilio kwa Benki.
- Zimefanyika juhudi za makusudi kuhakikisha kwamba kurugenzi ya mikopo haiwi na mkurugenzi kwa zaidi ya mwaka mmoja ili Bwana Japhet Justine aweze kuendelea kudetect zoezi la utoaji mikopo. Jukumu kuu la Benki hii ni kutoa mikopo iweje kurugenzi husika kutokuwa na mtu kwa zaidi ya mwaka?. Hili halifanyiki kwa bahati mbaya ni mkakati wake wa makusudi mheshimiwa raisi.
- Mikopo ya wafanyakazi wa Benki kwa mujibu wa taratibu za mikopo inatolewa kwa wale tuu anaowaona wako upande wake wengine wote wananyimwa mikopo kwa kigezo cha kwamba ni poor perfomers ukiuliza nikigezo kipi unatumia kumwita mtu poor perfomer kesho Katavi.