Mambo yote ni Maakuli - Hunogesha Mapenzi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mambo yote ni Maakuli - Hunogesha Mapenzi

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Lizzy, Jun 30, 2011.

 1. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #1
  Jun 30, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Chakula ni sehemu muhimu sana maishani...kwanza tunakula ili kushiba baadhi hawajali mapishi ilimradi tumbo lijae na wengine kila siku wanaongeza ubunifu kunogesha vyakula vyao mpaka wote wanaoonja wanafurahi.

  Hii ishu ya "usawa" unaopelekea kina mama kufanya kazi sawa na kina baba..."uvivu" unaopelekea mama kubweteka wakati ‘dada‘ anaunguza jikoni..."umjini" unaopelekea wasichana wasijifunze kupika kwakweli vinachangia kuvunja mahusiano au hata kuyakoroga na kupunguza hamasa ya kula majumbani wa baadhi ya watu.

  Unakuta mama akirudi kachoka dada ameshachemsha (korofisha kwa kiasi ajuacho yeye) "matabolo" huko kama mjomba wangu anavyoita chakula kibaya...au hata kama ana muda anaona uvivu kusimama/kaa jikoni akapikia familia yake...then wale wenzangu ambao hawakujifunza utotoni/ujanani hivyo hata akisema ajitahidi unakuta hajui nini kinachotangulia kati ya nyanya na hoho basi utamu wa chakula familia inaishia kupata siku wakiwa out...kwa ndugu na jamaa au siku mzee akijiopolea nyumba ndogo huko.

  Wengine hata chakula kipendwacho zaidi na familia yake anajua ‘dada‘ na sio yeye.Fanya familia/ndugu/marafiki/mpenzi wako wakumiss kwa vitu tofauti tofauti ukiwa haupo au umezidiwa na kazi.Wape vitu zaidi vya kusema "natamani mama/dada/mke/mpenzi wangu ndo angekua amepika" au "natamani chapati za mama".

  Nikiandika yote yanayocheza kichwani kuhusiana na hili jambo thread itakua ndefu watu fidenge waanze kulalamika so let me cut to the chase.Nataka kuwachalenge wadada /wamama wote hapa jamvini.Nna uhakika weekend wote mnapata vijisaa kidogo vya kupumzika...so. chukua lisaa limoja na nusu hivi au mawili uwaandalie ndugu/marafiki/familia/mpenzi wako chakula.

  Kwa wale mnaingiaga jikoni kuangalia kilichopo kwenye sufuria tu usiogope jiko bwana...haliumi!!Kama wahitaji recipe ya kitu fulani unaweza kuuliza hapa hapa nadhani wajuzi wapo!
  Kama ukifanya hivi feedback isikosekane...washangaze watu na mlo wa ukweli mpaka uulizwe "ULIKUA WAPI SIKU ZOTE...?"(Kwa hisani ya babu Asipirini)

  Picha kwa ushawishi zaidi.....

  Leo nimekula huo wali kuku wa kienyeji mtamu balaa!!

  52913_171837546166922_100000220329471_633770_4058434_o-1.jpg 133726_184860704864606_100000220329471_745248_184902_o-1.jpg IMG386.jpg IMG729-1.jpg IMG790-1.jpg IMG1014-1.jpg IMG1093-1.jpg 56785_181165328567477_100000220329471_718162_4710432_o-1.jpg
   
 2. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #2
  Jul 1, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Sasa huku kupeana njaa!!!! Nimeshasonga ugali wangu.. nakula kwa picha.
   
 3. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #3
  Jul 1, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Ohh pole!!Shushia na maji!
   
 4. Mwendabure

  Mwendabure JF-Expert Member

  #4
  Jul 1, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,054
  Likes Received: 296
  Trophy Points: 180
  Duh! Misotojo ya haja. Ila tumbo halina kioo, hata ule vizuri havionekani. Shibe sawa na aliyekula Kabichi la kuchemsha na Mashelisheli! Tumbo linatunza siri si haba.
   
 5. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #5
  Jul 1, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  lizzy
  unaweza pika mkate wa kumimina?
   
 6. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #6
  Jul 1, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Sijawahi kutengeneza maana haujawahi kunivutia!!!We unapenda?!
   
 7. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #7
  Jul 1, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  napenda vibaya mno kwa chai asubuhi

  yaani nipate chai ya rangi yenye mchaichai na mkate wa kumimina na katresi....duh..

  hebu jifunze tafadhali....

  katresi unajua?
  mchaichai unaujua?????
   
 8. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #8
  Jul 1, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Hahaha mchaichai ntaachaje kuujua?!Bado tangawizi na iliki sasa...dah mpaka mtu unatamani chai isiishe!!Ila katles najua!!Basi ntajaribu weekend hii nione kama ntaupenda!!
   
 9. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #9
  Jul 1, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  jaribu na huo mkate wa kumimina unaweza weka iliki pia
   
 10. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #10
  Jul 1, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Owkey...will give it a try!!
   
 11. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #11
  Jul 1, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,291
  Likes Received: 19,446
  Trophy Points: 280
  we mpare?
   
 12. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #12
  Jul 1, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Jee mkate wa chila, vikhosa (vilosa), kuku wa mahishi, mkate wa bwana, na msanif?!

  Mkate Wa ufuta, ajemi, mahamuri jee?

  Wali wa asumini, biriani na bokoboko imekaaje ?
   
 13. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #13
  Jul 1, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,496
  Likes Received: 81,820
  Trophy Points: 280
  Lizzy mie ukishawekwa mchaichai basi sitaki kingine chochote kile halafu kuwe na vitumbua vya moto na chuzi zito la kuku..weee! unaweza kujitafuna vidole :)
   
 14. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #14
  Jul 1, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Dah mbona wataka kunitoa mate mwenzio BAK???!Dah inabidi nitafute namna ya kufanikisha vyote hivyo kwa pamoja!!
   
 15. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #15
  Jul 1, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280

  ha haaaa gaijin
  nahisi wewe una damu ya kihindi hivi
  au ndugu wahindi
  kwa haya mapishi....
  hiyo mikate mingine nimeisikia tu
  sijawahi onja...
   
 16. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #16
  Jul 1, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  bubu utafanya hii thread watu wachukie misosi yao ya nyumbani
  mtu atoke kula ugali na kisamvu hala aingie hapa atoke udenda akasirike lol

  umewahi kula vitumbua na maharage ya nazi?????????
  acha kabisa
   
 17. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #17
  Jul 1, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  gaijin na lizzy
  chai ya maziwa yenye vanilla je????????
   
 18. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #18
  Jul 1, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Eeeee nimesahau kutaja na bajia na kachori pamoja na chatne ya mtindi na chicha!!!

  Kama hujala bado, fanya mpango haraka sana

  Usisahau ndizi za mkono wa tembo za sukari na nazi pamoja na tambi za kukaanga
   
 19. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #19
  Jul 1, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Mmh mi chai ya maziwa situmii ila napenda kuipika inavyopendezaga rangi naharufu!!!Weeee vitumbua na maharage pmoja vinashuka???!
   
 20. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #20
  Jul 1, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Ndizi zinatiwa sukari???!Nachukia tambi za kukaanga...
   
Loading...