IKUNGURU IJIRU CHUKU
JF-Expert Member
- Feb 27, 2021
- 484
- 548
Viongozi wengi sana wanaamini katika KUKALIPIA, KUKUSOA na kuwafanya watu wengine waonekane HAWAWEZI. Lakini viongozi wazuri ni wale ambao wanatoa mrejesho ambao unaweza kumjenga mtu na kumfanya afanye vizuri zaidi.
Kumbuka hata wewe wakati unaanza haukuwa hivyo na haukuwa kiongozi bora namna hiyo bali kuna watu WALIKUVUMILIA, wakakupa nafasi mara nyingi, wakakuelekeza, na wakakwambia mambo ya MSINGI ya kufanya, Kwa hiyo na wewe inatakiwa utoe fursa kwa watu wengine pia ili waweze kukua na kuwa bora zaidi.
Zingatia mambo ya msingi mojawapo ikiwa ni:
~ Toa mrejesho kwa wakati (timely feedback). Kuna wengine wanatoa feedback wakati wanakufukuza, ndiyo wanaanza kusema nilikuwa nakuvumilia tu kwa sababu niliona ukikosea na leo ndio mwisho wa mimi na wewe kufanya kazi pamoja.
Taasisi ya Ken branched (Ken branched institute) ilifanya utafiti wa kuhusu vitu gani ambavyo vinawajenga watu zaidi au kuwafanya wawapende viongozi wao. Wakawachukua watu 1400 wakawafanyia utafiti na wakagundua kitu kimojawapo ni kutoa MREJESHO UNAOJENGA.
Unapotoa mrejesho hutakiwi kutoa mrejesho hasi tu. Watu wakisikia mrejesho wanadhani ni mrejesho hasi tu mfano kwenye biashara unaweza kukuta mrejesho unaoambiwa ni bidhaa yako leo hujaitengeneza vizuri.
Lakini kuna mrejesho chanya pia ambapo unaweza kusifia yale mazuri yaliyofanyika na mrejesho huo unaongeza motivation ya kufanya mambo mazuri zaidi.