Mambo yanayo takiwa wakati wa kumpekua mruhumiwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mambo yanayo takiwa wakati wa kumpekua mruhumiwa

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by LOOOK, May 18, 2011.

 1. LOOOK

  LOOOK JF-Expert Member

  #1
  May 18, 2011
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 3,392
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  MAMABO YANAYO TAKIWA WAKATI WA KUMPEKUA MRUHUMIWA
  KUNA mambo kadhaa ambayo ndugu msomaji unatakiwa uyajue, pale ambapo mtuhumiwa wa kosa la jinai anatakiwa afanyiwe wakati wa kumpekua na kumkamata mtuhumiwa.


  Kwanza, kumkamata mtuhumiwa kunaweza kuwa kwa kutumia hati ya kumkamata au inaweza kufanyika bila kutumia hati ya kumkamata. Kwa mujibu wa kifungu cha 13 cha sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai.


  Iwapo mtuhumiwa atakuwa ameshafunguliwa mashtaka, basi mahakama kwa kutumia hakimu wake itamuita kwa kutumia hati ya kumkamata mtuhumiwa huyo.


  Kama mtuhumiwa huyo atakuwa hajafunguliwa mashitaka kabla hajakamatwa, basi samansi itatumika na wakati mwingine mtuhumiwa anaweza kukamatwa bila hata kutumia hati ya kumkamata.


  Kumkamata mtuhumiwa bila kutumia hati ya kukamata kunaweza kufanywa na mtu yeyote yule, si lazima awe afisa wa polisi kama ambavyo kifungu cha 16 na 14 cha sheria hii kinavyotamka bayana.


  Miongoni mwa watu ambao pia wanaweza kumkamata mtuhumiwa wa kosa la jinai ni pamoja na hakimu wa mahakama yoyote iliyowekwa kisheria, walinzi wa amani, yaani wajumbe wa nyumba kumi na ofisa watendaji wa kata na baadhi ya viongozi wa serikali za mitaa.


  Hata hivyo, watu hawa watamkamata mtuhumiwa ikiwa tu kama mtu huyo atakuwa anafanya kosa la jinai lililoainishwa chini ya kifungu cha 18 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai.
  Kimsingi, ni jukumu la ofisa wa polisi au mtu yeyote anayemkamata mtuhumiwa, kumtaarifu mtuhumiwa huyo sababau ya kumkamata na si kumkamata kiholela kama ambavyo wakati mwingine inafanyika.


  Hali hii wakati mwingine inasababisha watuhumiwa kukataa kukamatwa na hivyo kuleta mtafaruku baina yao na mtu/watu wanaoenda kutimiza wajibu wao wa kisheria kuwakamata watuhumiwa hao.


  Hiki ni kigezo muhimu cha kisheria kwa watu wanaoenda kuwakamata watuhumiwa wao kukitimiza kabla ya kuwakamata.
  Kwa upande wa watu wasio askari polisi wanaokwenda kuwakamata watuhumiwa, inawalizimu kuwakabidhi watuhumiwa hao katika mamlaka zinazohusika bila kuchelewa.


  Kwa mamlaka husika tuna maanisha ampeleke mtuhumiwa kituo cha polisi au mahakama iliyo karibu naye. Hii ni muhumu kwa sabababu watu binafsi hawana nyenzo au mahala panakokidhi viwango vya kuwaweka watuhumiwa na zaidi ya yote kuna uwezekano mkubwa kwa wao kutozingatia kanuni na  vigezo muhimu vya kisheria katika kuwahifadhi watuhumiwa wao.
  Mfano mzuri tunaupata katika kesi ya Jamhuri dhidi ya Dastur, A. L. R. 421, ambapo mtuhumiwa aligoma kukamatwa kwa kutoambiwa sababu ya kukamatwa. Zaidi ya hapo, mtuhumiwa alitoa kisu na kumchoma nacho askari mmojawapo kati ya watatu waliokwenda kumkamata.
  Mahakama baada ya kuridhika na maelezo yake, ilisema kwamba mtuhumiwa alikuwa na haki ya kuelezwa sababu ya kukamatwa.


  Kitu kingine cha msingi ambacho ndugu msomaji unatakiwa kujua ni kwamba mtu anayetakiwa kumkamata mtuhumiwa ni kwamba anatakiwa kutotumia nguvu za ziada wakati wa kumkamata.
  Hii inamaana kwamba vitu kama pingu, kumshika mtu kibindo na kadhalika, vinatakiwa kutumika ikiwa tu mtuhumiwa mwenyewe atakuwa anakataa kukamatwa kihalali. Hii ndiyo maana ya nguvu za ziada kama zilivyoelezewa chini ya kifungu cha 12 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai.
  Kwa mujibu wa maamuzi ya mahakama katika kesi ya M’bui dhidi ya Dyer,(1967) E.A 315, ikiwa kama ofisa wa polisi (au mtu yeyote anayemkamata mtuhumiwa) atatumia nguvu za ziada kumkamata mtuhumiwa, basi mtuhumiwa huyo anaweza kumfungulia madai ya kutumia nguvu za ziada kumkamata.


  Hata hivyo, suala la kuamua kama nguvu za ziada zimetumika au la, litaamulia kutokana na mazingira ya kesi yenyewe.


  Sheria hii pia imetoa mamlaka kwa polisi kuvunja nyumba ili kumkamata mtuhumiwa aliyejifungia ndani, kama ambavyo kifungu cha 19 na 20 cha sheria hii kinavyoelekeza.
  Hii ni kwa sababu inawezekana kwa mtuhumiwa wa kosa la jinai akajifungia ndani ya nyumba au jengo ili akimbie mkono wa sheria. Hivyo kwa kutambua hilo ndipo chini ya kifungu cha 20 cha sheria kikatoa msimamo huu.


  Pamoja na hayo yote, sheria hii imekataza kitendo cha kuwakamata watoto au mke/mume wa mtuhumiwa kwa madhumuni ya kumshurutisha mtuhumiwa ajisalimishe katika mkono wa sheria.
  Kitendo hiki ni kinyume cha sheria kama ilivyoamriwa katika kesi ya Lulu Titu dhidi ya Jamhuri (1968), H.C.D 30, ambapo mke wa mtuhumiwa alikamatwa na polisi kwa nia ya kumshurutisha mtuhumiwa ‘ajisalimishe’ polisi.
  Katika maamuzi yake, mahakama ilisema kwamba kitendo hiki ni kinyume cha sheria na kanuni za msingi za haki na kwamba mke wa mtuhumiwa anaweza kuwafungulia polisi shauri la madai kwa kudai fidia.
  Kwa upande wa kumpekua mtuhumiwa au nyumba yake, kitendo hiki pia kinaweza kufanywa kwa kutumia hati ya kupekua au bila hata kutumia hati ya kupekua.
  Ndugu msomaji unatakiwa kujua kwamba kuna mazingira ambayo yanaweza kumlazimisha askari polisi kukupekua bila kuwa na hati ya kukupekua na hii mara nyingi ni pale ambapo suala lililokuwepo ni dharura.


  Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai pia imeiingiza dhana hii katika vifungu vyake. Hata hivyo, mtu mwenye jinsia ya kile ni lazima apekuliwe na mwanamke mwenzake na hivyo hivyo kwa mwanamume ambae naye ni lazima apekuliwe na askari mwenye jinsia ya kiume.
  Hii ni katika kulinda heshima na utu wa mtuhumiwa anayepekuliwa, kwa mujibu wa kifungu cha 26 cha sheria hii. Kitu cha msingi kuhusu kupekuliwa ni kwamba, kwa mujibu wa sheria, mtu anatakiwa kupekuliwa kati ya mchana mpaka jioni, yaani kipidi ambacho jua linachomoza na pale jua linapokuchwa tu na si vinginevyo.


  Kwa maneno mengine ni kwamba mtuhumiwa haruhusiwi kupekuliwa wakati wa usiku, isipokuwa kama mahakama imeruhusu hivyo chini ya kifungu cha 40 cha sheria hii.
   
 2. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #2
  Sep 12, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  mkuu tunashukru kwa kutuelimisha hasa ukizingatia nchi yetu wengi sheria hatuzijui ila nilikuwa naomba kuuliza kama mtu ameamua kuchoma vyeti vyako ya shule sheria inasemaje nawewe unaenda kwa polisi au kwa mwenyekiti atakusaidije kwa haraka ilikuokoa hali kama hiyo?
   
Loading...