trachomatis
JF-Expert Member
- Jun 7, 2011
- 3,758
- 746
pamoja mkuu!mwanaume huwezi ruhusu ujinga kama huo!yaani hii iko very close to murder case!dk 2 tu unatoa mtu roho!
Mimi ninapokea na ninamwambia bi harus kisha namuuliza kama ataenda kumshukuru jamaa ama vp. Hlf nione atakavyojib.
nitapokea ila kwa shingo upande aisee... dah!! na mchumba wangu hatastahili fahamu hili.
Usifanye mchezo na ugonjwa wa moyo,Kumjua tu jamaa aliyekuwa anagonga hiyo kitu before ni noma.Kila ukikutana naye pressure inapanda.HAKIYA NANI MOTO UNGEWAKA NA KIKAO KINGEVUNJIKA!!!!!
huyo x hana akili.
Baba yangu kabla hajafa aliniambia kuna vitu viwili tuu ambavyo sitakiwi kususa chini ya hili jua navyo ni pesa na chakula,nitaipokea tena na shukrani tele nitampa,hakuna kaburi la mjinga bwana!!!Wewe unatarajia kuoa hivi karibuni!upo ktk kikao chako cha harusi,mmepanga bajeti ni 12m!Bwana harusi umeanza ahadi yako kwamba utatoa 3.5m!wanakamati wawili watatu nao wakatoa ahadi zao!Sasa unajua tena haya mambo ya marafiki kuleta watu pengine wasio rafiki zako ktk kikao wachangie kumbe mmoja wa marafiki zako kamleta X-boyfriend wa mchumba wako mtarajiwa.
Ikafika zamu ya x wa mtarajiwa wako huku nawe ukiwa unajua jamaa alikuwa anakula mzigo wako,jamaa kwa mbwembwe akauliza so far ahadi ya bw harusi na wanakamati wengine ni sh ngapi?ikaonekana jumla ni 5m!jamaa papo hapo akaahidi kutoa pesa yote iliyobakia yaani 7m yaani mara 2 ya pesa uliyoahidi wewe bwana harusi!kama hataki vile jamaa akatoa cheque book ya kampuni yake ambayo mchumba wako alikuwa akifanya kazi enzi ya mahusiano yake na jamaa hapo awali!Jamaa akaanguka saini akakukabidhi cheque ya 7m!
JE UTAIPOKEA?UTAMWAMBIA MCHUMBA WAKO KUWA X WAKE KATOA KIASI HICHO CHA PESA?AU UTAMTOA NDUKI JAMAA?
Atakaye enda naye fungate ndio aliyeoa,sasa kama fungate ataenda na jamaa jibu nitapata hapo!!!mkuu King Kong!utamwambia mtarajiwa wako kwamba jamaa katoa hiyo kiasi?mara 2 yako?nani kaoa sasa wewe au jamaa?
Hii inawahusu wanaoowa kwa michango, ukikubali kuoa kwa mchango, ukubali kuchangia na mkeo.
Mimi sikubaliani na michango ya harusi wala mazishi, sijawahi kutoa, sitotoa, na sitochangisha. Iwe ya harusi au ya maziko. Ni upunguani tu.
Pokea manake yaliyopita si ndwele! Kuacha kupokea ni kuonyesha kuwa hujiamini, pokea na uende ukamwambie mchumba ako bila woga! Ukisita utamfanya jamaa arudiane na mkeo mtarajiwa..
SWALI LA NYONGEZA KWA AKINA DADA MLIOOLEWA!ma-x wenu waliwapa mchango wa harusi?mlipeleka hiyo hela ktk kamati?mlisema imetoka kwa nani?mliwaambia waume zenu kwamba x wako kakuchangia enhe?kama hamkusema kwanini hamkusema?
Kwani kumwambia ni vibaya? Kwamba unaona kama mkeo mtarajiwa ataona jamaa ana hela zaidi yako then amrudie ama? Usipomwambia manake ni kwamba hujiamini...
mie napokea tu, namshukuru na kukiwa na umuhimu wa kumuambia wife kuwa ex wake ametoa mchango huo haina shida namuambia...... issue ni TRUST between you two
sweetlady?umeolewa?jibu swali la nyongeza nililouliza!au niliweke kwa upande wako ili upate hisia zake!x wa mmeo mtarajiwa kajitolea kumnunulia suti ya harusi mmeo mtarajiwa na honeymoney atawapeleka kwa gharama zake!UTAKUBALI UACHIWE KUMBUKUMBU YA AINA HIYO FOR THE REST OF YOUR LIFE?fikiri kabla ya kujibu
Nitapokea vizuri. Aliyepita kapita.