Mambo ya X

Mc Tilly Chizenga

JF-Expert Member
Feb 7, 2012
4,641
3,674
Wewe unatarajia kuoa hivi karibuni!upo ktk kikao chako cha harusi,mmepanga bajeti ni 12m!Bwana harusi umeanza ahadi yako kwamba utatoa 3.5m!wanakamati wawili watatu nao wakatoa ahadi zao!Sasa unajua tena haya mambo ya marafiki kuleta watu pengine wasio rafiki zako ktk kikao wachangie kumbe mmoja wa marafiki zako kamleta X-boyfriend wa mchumba wako mtarajiwa.

Ikafika zamu ya x wa mtarajiwa wako huku nawe ukiwa unajua jamaa alikuwa anakula mzigo wako,jamaa kwa mbwembwe akauliza so far ahadi ya bw harusi na wanakamati wengine ni sh ngapi?ikaonekana jumla ni 5m!jamaa papo hapo akaahidi kutoa pesa yote iliyobakia yaani 7m yaani mara 2 ya pesa uliyoahidi wewe bwana harusi!kama hataki vile jamaa akatoa cheque book ya kampuni yake ambayo mchumba wako alikuwa akifanya kazi enzi ya mahusiano yake na jamaa hapo awali!Jamaa akaanguka saini akakukabidhi cheque ya 7m!

JE UTAIPOKEA?UTAMWAMBIA MCHUMBA WAKO KUWA X WAKE KATOA KIASI HICHO CHA PESA?AU UTAMTOA NDUKI JAMAA?
 
SWALI LA NYONGEZA KWA AKINA DADA MLIOOLEWA!ma-x wenu waliwapa mchango wa harusi?mlipeleka hiyo hela ktk kamati?mlisema imetoka kwa nani?mliwaambia waume zenu kwamba x wako kakuchangia enhe?kama hamkusema kwanini hamkusema?
 
Pokea manake yaliyopita si ndwele! Kuacha kupokea ni kuonyesha kuwa hujiamini, pokea na uende ukamwambie mchumba ako bila woga! Ukisita utamfanya jamaa arudiane na mkeo mtarajiwa..
 
SWALI LA NYONGEZA KWA AKINA DADA MLIOOLEWA!ma-x wenu waliwapa mchango wa harusi?mlipeleka hiyo hela ktk kamati?mlisema imetoka kwa nani?mliwaambia waume zenu kwamba x wako kakuchangia enhe?kama hamkusema kwanini hamkusema?
Mie alinipa mchango ila niliutumia kwa mambo yangu mengine, sikumwambia husb manake haimuhusu kwanza hawakuwahi kufahamiana! Yeye pia alipooa nilimpa mchango wangu na aliupokea!
 
mkuu King Kong!utamwambia mtarajiwa wako kwamba jamaa katoa hiyo kiasi?mara 2 yako?nani kaoa sasa wewe au jamaa?
Kwani kumwambia ni vibaya? Kwamba unaona kama mkeo mtarajiwa ataona jamaa ana hela zaidi yako then amrudie ama? Usipomwambia manake ni kwamba hujiamini...
 
Ndani ya ndoa kuna siri nzito sana usione unapata wafadhili ukanenua meno ukaona umepata watu wema ukiona kilicho nyuma ya pazia unaweza usifunge hiyo ndoa unakuta mbaba anajitoa kweli kweli kumbe anapumzika kwa b harusi mtarajiwa na kwa kina mama hivyo hivyo anagaramia kila kitu kumbe kijana anamtafuna mama huu ufisadi cjui utaisha lini.
 
Pokea
manake yaliyopita si ndwele! Kuacha kupokea ni kuonyesha kuwa
hujiamini, pokea na uende ukamwambie mchumba ako bila woga! Ukisita
utamfanya jamaa arudiane na mkeo mtarajiwa..
Mavi ya kale hayanuki bwana,pokea with a broad smile.
 
mkuu umeonaee?tena na hivi vikao vinavyofanyika bar ambako kuna wale jamaa wa nyama choma,naweza kwenda chukua ile sime ya kukatia nyama nikirudi nimraruerarue!dharau hiyo!
Dharau kukupa mchango??? Kama ni hivyo usipokee michango yote ufanikishe harusi peke ako....
 
Kwani kumwambia ni vibaya? Kwamba unaona kama mkeo mtarajiwa ataona jamaa ana hela zaidi yako then amrudie ama? Usipomwambia manake ni kwamba hujiamini...

sweetlady?umeolewa?jibu swali la nyongeza nililouliza!au niliweke kwa upande wako ili upate hisia zake!x wa mmeo mtarajiwa kajitolea kumnunulia suti ya harusi mmeo mtarajiwa na honeymoney atawapeleka kwa gharama zake!UTAKUBALI UACHIWE KUMBUKUMBU YA AINA HIYO FOR THE REST OF YOUR LIFE?fikiri kabla ya kujibu
 
mie napokea tu, namshukuru na kukiwa na umuhimu wa kumuambia wife kuwa ex wake ametoa mchango huo haina shida namuambia...... issue ni TRUST between you two
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom