Mambo ya Ngoswe tumuachie Ngoswe,,!

Mambo ya Ngoswe tumuachie Ngoswe,,!

red fox

Senior Member
Joined
Jan 5, 2017
Posts
127
Reaction score
342
*MITOMINGI*; nadhani sasa mgeni amekwisha kumaliza kula hebu nenda kaondoe vyombo

*MAMA_MAZOEA*; Basi fanya haraka (Mazoea anatoka, anaenda kwa Ngoswe alipo).

*MAZOEA*; Hodi! Hodi!

*NGOSWE*; Karibu

*MAZOEA*; (Akiingia). Ahsante. Nimekuja kuchukua vyombo.

*NGOSWE*; Vyombo! Kaa basi mbona unasimama kama vile hakuna viti.

*MAZOEA*; Nimeambiwa nifanye haraka.

*NGOSWE*; Mmm! Haya ngoja ninawe basi (Ngoswe ananawa kwa taratibu jicho likiwa usoni mwa Mazoea ambaye anatazama kando). Hivo mzima wee?

*MAZOEA*; Bee?

*NGOSWE*; Salama?

*MAZOEA*; Salama tu.

*NGOSWE*; Sasa ndio umekataa kukaa?

*MAZOEA*; (Ajidai hakusikia) Si umekwisha maliza?

*NGOSWE*; Bado kidogo.

*MAZOEA*; Basi nitakuja chukua baadaye. (Ataka kutoka)

*NGOSWE*; Basi nenda navyo. (Mazoea anarudi kuinama kuvichukua. (Ngoswe kwa sauti ndogo). Hivyo waitwa nani?

*MAZOEA*; Mie?

*NGOSWE*; Ndio wewe hapo kisura.

*MAZOEA*; (anatabasamu huku akiondoka). Mazoea!i

Story ni tamu sema nini jamaa ndo walishasemaga kuwa, ya Ngoswe tumuachie Ngoswe! ! !

 
Leta full package mkuu.

Unakumbuka Ngoswe alidabwa na mama Mazoea kule mtoni akipiga kiss la nguvu kwa mazoea
 
Na kimvua hiki chenye ubarid mujaraabu ndani ya jiji la bashite, nami kijogoo nipo ugenini, lazima nitengeneze mazingira kwa mazoea
 
Kati ya kitabu(ngoswe penzi kitovu cha uzembe) na usemi wa ya ngoswe tumuachie ngoswe) kipi kilitangulia???
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom