Mambo ya msingi kufanya kabla ya kufika miaka 28

mm nadhani ni mipango ya mungu.. mbona yule mzee aliyekua ana miliki KFC alifanikiwa akiwa na miaka 65..
 
Ngoja niwape mchanganuo wa umri na kile unachotakiwa ANGALAU UWE NACHO KIBONGOBONGO.

20 - 25 =Iwe kama ni kielimu hujafikia malengo yako,sitisha mara moja tafuta kazi/biashara ya kufanya,pigana kufa na kupona ili kama vipi urudi shule kwa pesa yako.

25 - 30 = Hakikisha uwe na angalau na SHUGHULI RASMI kama umeajiliwa au umejiajili.

30 - 35 = Uwe na angalau kama sio nyumba basi kiwanja,tena ujitahidi uwe umeoa/umeolewa kama sio kuishi nae,tena si mbaya ukawa umeshatengeneza familia,kwa maana ya kuwa na watoto kama mungu kakuwezesha.

35 - 40 = Ni umri wa kama kiwanja kiwe kimejengwa, na kama ni tayari basi nenda step nyingine ya kumiliki kama ni Gari au kuongeza nyumba na hakikisha vinaenda sambamba na ongezeko la familia.

40 - 45 = Ni umri wa masahihisho, kama hukuwahi kununua kiwanja au kujenga basi hapa pambana afe kipa afe beki,kama umegundua mkeo hazai fanya mchakato kwingine kama ni mwanaume na kama mwanamke umegundua mumeo ndio mwenye shida basi tafuta nje umletee mtoto. Kifupi ni umri wa masahihisho.Ila kwa wale ambao wameenda vizuri huko nyuma basi hapa kama ni wale watoto wapo kwenye level tofauti za elimu,kwahiyo ni muda wa kuwawekea malengo ya kimasomo watoto wao.

45 -50 = Kwa yule ambaye hakukosea huko nyuma,basi umri huu ni wa kuanza kuwatengenezea mazingira watoto wako,kama ni shuguli zako ni kuanza kuwahusisha,huku wewe ukijiweka pembeni taratibu na kuangalia fulsa za umri wako. Lakini kwa wale waliokosea hapa ni kupitia zile hatua za 35 -40.

50 - 60 = Ni kujiandaa na maisha mapya ya kustaafu au kujiweka mbali na shughuli za shulba.Na kama ulijitenga na msikiti/kanisa huu ndio muda wako.

60 - 70 = kula matunda yako huku ukiangalia misingi ya wanao inaendaje.

70 - 80 = kula matunda.

80 - n.k = kumsikilizia bwana sir god anasemaje.
 
Habari wana jamvi,

Ni mambo gani ya msingi kufanya kabla hujafikisha miaka 28 kwa vijana wa 20-27 yatakayokufanya uwe na maisha yanayopaswa kuishi mtu anayejitambua na mwenye malengo na future yake.
naaminifu nipo Asilimia flan ktk maisha....lkn nashangaa sana elimu zenu......hazichangi vizur....ama IQ ndogo

umetaja age hiyo angalau na hiyo 40 uwe somewhere....kwa nini ktk age za utotoni huangaliii mafanikkio anayofikia mtoto by age?

Sometimes je aliepata walimu na mtaala sahihi wkt wa makuzi Yake huyoi??

Tuna calculate sana when we are 50 tuwe hivi je huko nyuma je! hujui good future Ina determine background nzur?
 
Maisha ni kama JF wazee na vijana wanachangia, akili yako ikikutuma umezeeka utakuwa hivyo.
 
ukifika 30s huna gari na nyumba,hata kama ni ya tembe!basiiiiii kwisha habari yako!but kama ni mwaamke upo above 29,sahau kuhusu ndoa!!!!labdaaa kuzalishwa!!!!
 
Ngoja niwape mchanganuo wa umri na kile unachotakiwa ANGALAU UWE NACHO KIBONGOBONGO.

20 - 25 =Iwe kama ni kielimu hujafikia malengo yako,sitisha mara moja tafuta kazi/biashara ya kufanya,pigana kufa na kupona ili kama vipi urudi shule kwa pesa yako.

25 - 30 = Hakikisha uwe na angalau na SHUGHULI RASMI kama umeajiliwa au umejiajili.

30 - 35 = Uwe na angalau kama sio nyumba basi kiwanja,tena ujitahidi uwe umeoa/umeolewa kama sio kuishi nae,tena si mbaya ukawa umeshatengeneza familia,kwa maana ya kuwa na watoto kama mungu kakuwezesha.

35 - 40 = Ni umri wa kama kiwanja kiwe kimejengwa, na kama ni tayari basi nenda step nyingine ya kumiliki kama ni Gari au kuongeza nyumba na hakikisha vinaenda sambamba na ongezeko la familia.

40 - 45 = Ni umri wa masahihisho, kama hukuwahi kununua kiwanja au kujenga basi hapa pambana afe kipa afe beki,kama umegundua mkeo hazai fanya mchakato kwingine kama ni mwanaume na kama mwanamke umegundua mumeo ndio mwenye shida basi tafuta nje umletee mtoto. Kifupi ni umri wa masahihisho.Ila kwa wale ambao wameenda vizuri huko nyuma basi hapa kama ni wale watoto wapo kwenye level tofauti za elimu,kwahiyo ni muda wa kuwawekea malengo ya kimasomo watoto wao.

45 -50 = Kwa yule ambaye hakukosea huko nyuma,basi umri huu ni wa kuanza kuwatengenezea mazingira watoto wako,kama ni shuguli zako ni kuanza kuwahusisha,huku wewe ukijiweka pembeni taratibu na kuangalia fulsa za umri wako. Lakini kwa wale waliokosea hapa ni kupitia zile hatua za 35 -40.

50 - 60 = Ni kujiandaa na maisha mapya ya kustaafu au kujiweka mbali na shughuli za shulba.Na kama ulijitenga na msikiti/kanisa huu ndio muda wako.

60 - 70 = kula matunda yako huku ukiangalia misingi ya wanao inaendaje.

70 - 80 = kula matunda.

80 - n.k = kumsikilizia bwana sir god anasemaje.
Daaah apo umesomeka vizuri saaanaa mdau wangu yaaanii ndo inapaswa iwe lakin wengine watabisha kamakawaida yawabongo
 
Habari wana jamvi,

Ni mambo gani ya msingi kufanya kabla hujafikisha miaka 28 kwa vijana wa 20-27 yatakayokufanya uwe na maisha yanayopaswa kuishi mtu anayejitambua na mwenye malengo na future yake.
Uwe umeshahama nyumbani kwenu na unafanya kazi kwa bidii na maarifa
 
Maisha hayana formula,mafanikio au matatizo yanakuja muda wowote,kitu muhimu ni wewe kuchagua vipaumbele vyako na kuhakikisha unavipigania kwa uwezo wako wote na jitahidi pia kumshirikisha Mungu katika mambo yako.
 
babu wa loliondo alitoboa akiwa 67.cha msingi usikate tamaa.pambana kila uchao.maisha hayana kanuni.bora uzima mkuu.niamini mimi tuu
 
Kwa jinsi 'mafanikio' sikuhizi yalivyo huo umri bado ndo kunakucha kwenye harakati za kielimu,maendeleo ya kazi, kuanzisha familia perhaps, kwa ufupi 20's na 30's kwa kijana ni miaka ya kufanya kazi kwa bidii nguvu unayoo ndo mda wa kujijenga
Maisha ni 'aspect' nyingi na unavyoishi ndo unavyoyajenga ndo unaishi maisha yako,so choose wisely ,work hard,enjoy..achana na zile mambo utaenjoy ukiwa.....enjoy everyday
 
Back
Top Bottom