Siwezi kumlaumu huyu dada, "kisa mkasa" hiki ni ushahidi au ni picha yenye kaonyesha jamii yetu ni ni jamii ya aina gani. Jamii yetu imejaa watu wasiojitambua na wasiopenda kuyakabiri matatizo. Kama msomi wa kiwango cha shahada ya uzamili ana fikra za hivi tutegemee nini. Pamoja na kuwa na kazi fikra zake yeye ni kuhongwa. Mtu wa aina hii atakataa vipi kutoa "pete" kama mwombaji ana pesa. Ndio maana mabinti na madada wengi mmejigeuza kuwa vyombo vya starehe badala ya kuwa "Mama". Siku zote nguvu ya mwanamke ipo kwenye ushawishi ndio maana wote tu mashahidi kwa yaliyomkuta Samson kwa Derira. Unashindwa vipi kutumia ushawishi "kumshape" mumeo ktk namna uipendayo.