Mambo ya kuzingatia unapotaka kuhamia au kuishi unapokuwa nchini Marekani

Bullshit

JF-Expert Member
Nov 30, 2016
1,300
1,495
Mambo muhimu ya kuzingatia au kufanya unapokuwa unaishi nchini Marekani.

Epuka kuishi kwenye miji ya anasa na panga nyumba yenye gharama nafuu.

Miliki usafiri wako mwenyewe achana na kutegemea usafiri wa umma

Fanya kazi moja na tumia weekend yako kujumuika na ndugu, jamaa na marafiki

Zingatia kufanya kazi na acha kubadili kazi mara kwa mara (wamarekani hawapendi kuzoea kazi ya sehemu moja ndomana kila mwaka wanafanyakazi wanakuwa ni wapya) ila kuna faida zake kudumu kwenye kazi muda mrefu.

Ishi au apply kwenye nyumba za serikali (nyumba za serekali uwa zina gharama nafuu ni vizuri kama unafamilia kubwa ukaomba kupatiwa nyumba ya serikali).

Zingatia sheria za nchi(unauwezo wa kufanya unachotaka kuishi unavyotaka ila isiwe kinyume na sheria)

Pendelea kutumia huduma zinazo tolewa na serikali kama vile: shule, usafiri, hospitali, bima, wi fi nk..

Omba kadi ya bure ya chakula kutoka serikaili (ikiwa huna kipato cha kukidhi mahitaji yako<serikali hutoa kadi ya kununua chakula bure).

Pendelea kujiunga kwenye mashirika mbali mbali yanaotoa misaada mbali mbali.(mashirika ni mengi yanayo shughuli matatizo ya watu nchini Marekani na wanatoa misaada mbali mbali kwa wanafamilia,mfano kuwapeleka watoto shule, kuwanunulia chakula, nguo nk...)

Nunua vitu vyenye gharama nafuu au ambavyo zimetumika (kuna maduka ambayo ununua vitu hapo na kuviuza hapo hapo ni vizuri kupendelea kununua bidhaa zako hapo kama vile meza, sofa, laptop nk..ila maduka haya yanatumia cash na sio ya public sana).

Hakikisha unamiliki kadi za maduka yote unayotembelea kununua bidhaa zako (maduka makubwa yanatoa kadi ya mteja,ukiwa na kadi yao ina maanisha wewe ni mteja wao na uwa wanapunguza bei kwa kila bidhaa utakayo nunua.mfano umenunua kitu $50 ila ikiwa una kadi utanunua mfano kwa $ 45)

Pendelea kunua vitu vya mkopo (Wamarekani ni watu wana amini sana vitu vya mkopo, mfano unataka kununua nymba, gari, kwa pesa kadhaa si vyema ukalipa yote ni bora ukope uwe unalipa kidogo kidogo kwa kila mwezi. Sio kutoa yote kwa mkupuo)

Kuwa mtu wa watu, mchangamfu, usijifanya kujua sana na usichokijua uliza.

NB: Tukutane next post. Unaweza kuchagia pia na unaruhusiwa kuuliza.
 
Mkuu mimi naomba kujua utaratibu wa kuingia marekani kutokea tz ili hali sina ndugu wala rafiki huko.
Gharama za usafiri kutoka tz,sehemu nafuu kwa kuishi na jinsi ya kupata visa ya muda mrefu.
Nitashukuru sana na kwa faida ya wote
 
Unaemzungumzia ni raia au Ana greencard, undocumented au mkimbizi sababu kama ni raia yote unayoyasema atapata ila kama sio raia kwa mujibu ya mabadiliko ya sasa ya bwana trump Nyumba unazosema hatapata,benefits za mtu wa kipato cha chini hatapata labda awe mkimbizi ,hata mwenye greencard akitumia hizo benefits baadaye atakapoomba uraia zinaathari kwake .Kwa mtanzania ambaye hajui taratibu anaweza fikiria hizo benefits ulizosema ni kwa kila mtu hata ambaye sio raia.
 
Nimepata kitu
Maana kuna rafiki yangu huko
Ameniambia niende sasa nimepata cha kujifunza
 
Daah wewe jamaa unaleta habari ambazo Mtanzania anayeishi Marekani hawezi kusema hivi vitu kabisa wala kumwambia dungu yake au kumpeleka huko ndio maana hata hapa jamiiforum bila wewe kusema haya ingekuwa giza tu

Endelea kufunguka
Vipi swala kutembea usiku sana

Vipi kuhusu hii systematical racism ambayo waafrika wanaisema sana

Gun shooting unatakiwa kuikwepa vipi?

Ndugu akikuita unaenda tu je hapo ubalozi hawawezi kuzingua kuhusu viza tu maswali?

Je unaweza kufanya kazi bila kibali kwa kuibia ?
 
Unaemzungumzia ni raia au Ana greencard, undocumented au mkimbizi sababu kama ni raia yote unayoyasema atapata ila kama sio raia kwa mujibu ya mabadiliko ya sasa ya bwana trump Nyumba unazosema hatapata,benefits za mtu wa kipato cha chini hatapata labda awe mkimbizi ,hata mwenye greencard akitumia hizo benefits baadaye atakapoomba uraia zinaathari kwake .Kwa mtanzania ambaye hajui taratibu anaweza fikiria hizo benefits ulizosema ni kwa kila mtu hata ambaye sio raia.

Marekani hizi si tu kwa undocuments,ila nyumba hata kama wewe sio raia unaweza ku apply misaada mingi inalenga watu wenye vipato vya chini.
HII IJAWAI KUBADILIKA.
Haki ambayo rais anayo na hasie raia hana ni kupiga kura na kufanya kazi sererkali,lakini swala la kusoma bado liko vile vile,kwenda jeshin,makazi na vitu vingine,raia vilevile hawezi ku apply schoolarship akasomeshwe,anapata mkopo kutoka serekali,hii hata mgeni unaweza kukopa pesa za masomo kutoka serekali...

Mabadiliko ambayo anawezabkukuathiri kuomba uraia kama vile wewe ni mtu unategemea misaada ya serekali tu na uwezi kujitegemea,nais hii imelenga wazee kupewa uraia marekani maana wanaitaji vijana wenye nguvu na wenye uwez wakujitegemea
 
Yaan ni ishi marekani afu ninunue vitu used na je nikija bongo ntaanzaje kuvimba

Ikiwa wewe unaishi marekani unataka kufikia malengo yako achana na vitu vya anasa.
Lakn kama umekuja kutembea kaa muda basi huu ujumbe aukuhusu
 
Ikiwa wewe unaishi marekani unataka kufikia malengo yako achana na vitu vya anasa.
Lakn kama umekuja kutembea kaa muda basi huu ujumbe aukuhusu
Hivi kwa nini watanzania wengi wanaoishi marekani hawafikii malengo yao hasa wakija huku bongo kwao inakua ni shida sana yani wanakua na moto siku za kwanza halafu baadae wanakua watia huruma sana,kuna nini cha ziada nchini marekani ambapo ndugu zetu wanashindwa kutoka
 
Daah wewe jamaa unaleta habari ambazo Mtanzania anayeishi Marekani hawezi kusema hivi vitu kabisa wala kumwambia dungu yake au kumpeleka huko ndio maana hata hapa jamiiforum bila wewe kusema haya ingekuwa giza tu

Endelea kufunguka
Vipi swala kutembea usiku sana

Vipi kuhusu hii systematical racism ambayo waafrika wanaisema sana

Gun shooting unatakiwa kuikwepa vipi?

Ndugu akikuita unaenda tu je hapo ubalozi hawawezi kuzingua kuhusu viza tu maswali?

Je unaweza kufanya kazi bila kibali kwa kuibia ?

Unaruhusiwa kutembea usiku muda wote,lakn ni vyema ukawa na gari ya kutembelea

Mimi nasikiaga dunia kuna ubaguzi ila sijawahi kubagulia au kushuhudia ubaguzi.sina experiece na hili swala
Mimi naishi na watu wa aina yote na ninafanya kazi na kila aina ya rangi,nmefanya kazi sehemu mbali mbali lakn sijawah kushuhudia hilo

Huwezi kukwepa shooting ila tu nakushauri achana kutembea na watu amabo hawaeleweki,epuka sehemu za hatar wewe kutembea

Kitu cha kwanza marekani wanatakiwa kujua unaenda kufanya nini na unafikiwa wapi au kwa nani,.vile vile wanaangalia una kias gani mfukoni.

Kufanya kazi bila kibali inawezekana ila inaitaji network.njia nyingine ambayo unaweza kufanya kazi bila kibali ni kutumiadocument za mtu mwingine.
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Back
Top Bottom