Mambo ya kuzingatia unaopoingia mkataba wa Bima

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,325
33,131
[FONT=ArialMT, sans-serif]Neno Bima si geni masikioni mwa watu wengi. Ni mkataba wa biashara ambapo mtu mmoja, ama kikundi cha watu, taasisi au shirika, ili mradi kikifanya hivyo kwa mujibu wa sheria, huchukua jukumu la kutoa ahadi ya kulipa hasara itakayotokana na uharibifu wa mali, upotevu wa mali, kifo, au hasara nyingineyo yoyote anayoipata mkataji wa bima anayeingia mkataba na mtoaji wa bima yaani yule anayekubali kuwa tayari kufidia hasara hiyo.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]
Kuna aina nyingi za bima, lakini zilizo kubwa zaidi ni mbili: Ya kwanza ni Bima ya kinga ya mal,i ambayo mara nyingi hutokana na makubaliano ya kulipwa fidia mkata bima aliyepoteza mali yake kutokana na uharibifu, unaotokana na majanga ya asili kama vile mvua, matetemeko, mafuriko, na pia mambo mengineyo kama moto, ajali na wizi. Aina ya pili kubwa ni ile inayoitwa Bima ya Kinga ya maisha, ambayo ni malipo ya fidia yanayotolewa kutokana na kifo cha mkata bima ama mtu aliyewekewa bima ya aina hiyo.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]
Kundi jingine katika kuzigawa bima ni lile la bima za hiari na za lazima. Bima za hiari ni kama vile unavyokata bima ya kuilinda biashara. [/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Ingawa tumeona kuwa, aina kuu mbili za bima ni zile za kinga ya majanga dhidi ya mali na pia bima ya maisha, ndani ya bima hizi au katikati yake, zimezuka aina nyingi tu za bima kiasi kwamba hakuna ajuaye aina za bima zipo ngapi, hasa kwa wingi wake kwa sababu hata wewe na mimi tunaweza kuanzisha aina tofauti-tofauti za bima, zikiwemo zile ambazo hazijawahi kuwepo kabisa, ili mradi tu zimefuata sheria husika. [/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]
Mfano, baada ya bima kubwa za mwanzo, ambazo nyingi zilianzia kwa kampuni ya Lloyd’s ya Uingereza, zilikuja bima tofauti-tofauti kulingana na nyakati, mahali na mazingira. [/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Ukiachilia mbali bima za ajali, moto, maisha, bima zilizobuniwa baadaye ni kama vile bima za elimu, mafuriko, kilimo, na kadhalika. [/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Katika nchi zilizoendelea zimeanzishwa bima kama zile za hasara anazopata mtu kama vile sherehe inaharibika (mfano kumlipa mwenye sherehe endapo chakula cha harusi kimeibiwa au mlevi harusini kuwapiga waalikwa). Katika nchi za Magharibi kuna bima pia unayoweza kukata na kulipwa fidia iwapo mbwa wako anaibwa au paka unayemfuga kufa, nakadhalika) na hata kufidiwa iwapo umekata bima kukinga nyaraka zinazopotea kwa kompyuta kuingiliwa na virusi au kufidiwa gharama pale ambapo unafeli mtihani na ulishaingia gharama za kulipia elimu.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]
Mkataba wa Bima: Unavyofanana na Mikataba mingine kisheria[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Mkataba wa bima unaanza kwa makubaliano baina ya mkatishaji Bima-yaani muuzaji (Insurer) wa Maktaba wa makubaliano ya bima (Policy) na mkataji bima-yule anayenunua bima hiyo (insuree). Kwa kawaida mkataji bima, mathalani mmiliki wa gari au nyumba, ndiye humfuata muuzaji wa bima na kuangalia aina ya bima zinazotolewa, kuchagua ile inayomfaa, kuangalia masharti ya bima, pamoja na ada ya kila mwezi au mwaka (au kipindi chochote cha malipo watakachokubaliana) na kiwango cha fidia anachostahili kulipwa linapotokea janga lililokatiwa bima. [/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Hata hivyo, si mara zote, mnunuaji bima ndiye anayeenda ofisini kwa muuza bima, mara nyingi tu imetokea wale wanaouza bima wakazunguka mitaani au kujitangaza kupitia vyombo vya habari na mawasiliano kuwa wanauza bima hii. Hata hivyo, ukweli ni kuwa haijalishi nani kamfuata mwingine, mkataba wa bima ni kama mikataba mingine kisheria kwa sababu kunapotokea utatuzi wa mgogoro baadaye, kikubwa kinachoangaliwa zaidi ni makubaliano yaliyomo ndani ya mkataba husika.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Mkataba wa Bima hupata nguvu kisheria pale anayenunua bima kujikinga na hasara anaukubali mkataba wa muuza bima na kulipa ada inayomuwezesha kuanza kulipwa pale janga husika linapotokea. [/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]
Mkataba wa Bima unafanana na mikataba mingine kwa sababu matakwa ya kisheria ili kuufanya mkataba huo utambuliwe mara nyingi ni yale yale kama mikataba mingine. Katika hili, vipengele vya mikataba ilivyoaininishwa katika Sheria ya Mikataba ya Tanzania, huhusika moja kwa moja, zaidi ya matakwa yalivyo katika Sheria ya Bima ya Tanzania ya 1996 na sheria zinginezo husika. Mathalani, wanaoingia mkataba ni lazima wawe na akili timamu (kwa vile kampuni inaweza pia kukata bima na hatuwezi kusema kama ina akili timamu, basi wakurugenzi au wakala wanaoingia mkataba kwa niaba yake wawe na akili timamu). [/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Pili, wahusika wa mkataba huu lazima wawe wana umri wa mtu mzima (yaani miaka 18 na kuendelea) kama inavyotaka sheria nchini. [/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]
Katika hili la umri, mtoto ambaye hajafikia umri wa miaka 18 anaweza kukatiwa bima kwa niaba yake na mtu mzima. [/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Tatu, Mkataba wa bima lazima uingiwe kwa madhumuni halali na si haramu ili upate nguvu ya kisheria. Huwezi mathalani kukata bima ya kukukinga na maradhi ukiwa katika biashara ya ukahaba kwa sababu biashara ya ukahaba ni haramu kisheria. [/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Badala yake, mtu anaweza kukata bima ya kulinda na maradhi akiwa katika biashara halali kama nesi anayehudumia wagonjwa katika zahanati.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]
Dhana ya Uaminifu Kamilifu/Ufahamifu Halisi : Msingi Mkuu wa Bima Zote[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Mkataba wa Bima una tofauti kubwa na mikataba mingine kuhusiana na mambo fulani fulani kiasi kwamba ,Sheria za Bima imekuwa eneo linalojitegemea kabisa, tofauti na sheria nyingine.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Kikubwa kabisa kinachoutofautisha mkataba wa Bima na mikataba mingine ni dhana ya uaminifu kamilifu/Ufahamifu Halisi ambayo imetokana na neno maarufu la Kilatini ambalo kila mwanasheria wa bima lazima alifahamu-uberrimae fidae au “utmost good-faith” kwa kimombo. Msingi huu wa “uaminifu kamilifu” ndio mama wa bima zetu. Ni dhana muhimu sana ambayo wahusika wa mkataba wa bima (muuzaji na mnunuzi wa bima) lazima waifahamu na wajulishane wakati wanapoingia mkataba huu kwa sababu hata wanapofichana bado itazuka pale unapotokea mgogoro baina yao baadaye, hasa wakati wa kudai malipo ambapo mara nyingi mnunuzi wa bima (yule anayedai fidia) huweza kulia kwa sababu wauza bima wengi wanaitumia kuepuka kulipa fidia ambazo wanaona hazistahili. [/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]
Kwa kifupi tu, katika dhana hii wahusika wa bima wanapaswa kuelezana ukweli wote kuhusu mambo muhimu yahusuyo jambo lililokatiwa bima, jambo ambalo mara nyingi yule anayenunua bima anakuwa anashawishika kutoeleza ukweli mtupu kuogopa kulipa malipo makubwa zaidi kama ada.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Mathalani, mtu unapokata bima ya afya basi ni vema na inashauriwa sana uieleze kampuni ya bima kuhusu mambo yote muhimu kuhusu aina ya maisha unayoishi, historia ya kiafya na kadhalika ili imuweke katika uelewa mzuri kama akukatie bima au asikukatie au kama anakukatia basi akulipishe ada kiasi gani. [/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]
Hili lina mantiki kisheria na kibiashara kwa sababu muuza bima naye anaangalia maslahi ya kutokata bima ambazo atalipa fidia watu wengi mno au kumkatia mtu ambaye anajua kuna uwezekano akafariki ndani ya miezi sita tu, huku chanzo cha fungu lililopo la fidia husika ni dogo au limekadiriwa kuhimili wastani fulani wa maisha ya wanunuaji mikataba hii. [/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]
Inakuwa rahisi kwake kujua kama unavuta sigara paketi nzima kwa siku au la ili kukadiria unaweza kupata saratani (kansa) au la. Inakuwa rahisi kwake kuamua kukukatia bima ya ajali kama anajua hali ya barabara ambayo basi lako linasafiri, umakini na rekodi ya ajali ya vyombo na madereva wako, mwendo-kasi ambao vyombo vyako hutumia barabarani, upya na ubora wa mabasi yako, nakadhalika. Unapaswa kuwa kweli katika mambo hayo na mengineyo yatakayomfanya atoe uamuzi sahihi, na inaweza kukufanya ukose kulipwa fidia au ulipwe kidogo zaidi kwa sababu unakuwa umekiuka msingi huu wa dhana ya Uaminifu kamilifu.[/FONT]



CHANZO: NIPASHE
 
Back
Top Bottom