Mambo ya kuzingatia ukitaka kununua gari Uingereza

Ubumuntu

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
14,314
10,775
Salaam,

Katika kujadili masuala mbalimbali yanayohusu magari, nilipata kuweka moja ya mitandao wa uuzaji na ununuaji wa magari Uingereza.
Mtandao huu unaitwa Autotrader, ni moja mitandao maarufu na ya uhakika katika kununua na kuuza magari (mapya na yaliyotumika).

Sasa ndugu Bavaria alipata kuniuliza kama nimeshawahi kutumia mtandao huo kununua gari. Nikahisi pengine ana wasiwasi na mtandao huo.
Hivyo basi, kwa msaada wake na wale wengine wote ambao wanatamani kununua magari Uingereza, nikaona nitoe kidogo uzoefu wangu katika hili.

Sina uzoefu na ununuaji wa magari Japan au sehemu zingine zaidi ya Uingereza. Hivyo ninachokisema hapa pengine kinaweza kikawa kina bias. Ila naamini hakuna sehemu salama ya kununua magari kama Uingereza. Kwanini? Sababu kubwa ni uwazi wa taarifa za gari husika.

Serikali ya Uingereza kupitia mtandao wake mkuu wa idara zote za serikali Welcome to GOV.UK, imeweka mwongozo mzuri sana kwa mtu anayetaka kununua gari lililotumika Uingereza, ili kujua kama gari ni la wizi au si salama kutumika barabarani.

Angalia mwongozo huo hapa: Check a used vehicle you’re buying. Mwongozo una mambo makuu manne:

Moja, unashauriwa kumuuliza muuzaji namba ya usajili wa gari, aina ya gari na model yake. Uzuri kwenye mtandao wa Autotrader UK, gari nyingi zilizotumika uwekwa picha zenye kuonyesha namba ya usajili wa gari. Angali mfano hapa chini:

1602701550482.png

1602701573272.png

Namba ya usajili ya gari hilo ni LG68 DFU.

Pili, serikali ya Uingereza kupitia wizara ya usafiri (Ministry of Transport - MOT) ina utaratibu wa kupima ubora na uthamani wa gari kutumika barabarani. Na pia kupima kiwango cha uchafuzi wa hewa wa gari husika. Kipimo hiki kinajulikana kama MOT test. Ni kipimo cha lazima. Hivyo kwa hatua ya pili, mnunuzi baada ya kuwa umemwomba muuzaji namba ya MOT test, unapaswa kuhakiki historia ya gari husika kwenye ubora na uthamani wake. Unaweza kufanya hivyo kupitia mtandao huu: Check the MOT history of a vehicle. Utakutana na interface hii:

Screen Shot 2020-10-14 at 21.16.29.png

Kwa kuwa ushafahamu namba ya usajili wa gari unalolitaka, basi bonyeza hapo kwenye 'Start now'.

Screen Shot 2020-10-14 at 21.23.47.png

Hapo ingiza namba ya usajili ya gari unalolitaka. Kwa leo natumia mfano wa namba ya gari hilo hapo juu. Kisha utaona hivi:

Screen Shot 2020-10-14 at 21.37.14.png

Kama unavyooona hapo juu, kwa mfano wa gari hilo, MOT yake imeshakwisha mwanzoni mwa mwezi huu. Unaweza kuona hadi cheti chake cha ukaguzi na mahali ukaguzi ulipofanyikia. Hicho cheti pia kitakuonyesha kama namba ya MOT test aliyokupa mnunuzi ni ya ukweli ama siyo.

Tatu, katika kuhakikisha ukweli hizo taarifa, serikali kupitia wakala wa utoaji leseni za madereva na magari (Driver and Vehicle Licensing Agency - DVLA) imeweka utaratibu wa mnunuzi kuhakiki taarifa za gari kupitia website hii: Get vehicle information from DVLA. Hapa kazi kubwa ni kutumia namba ya usajili ya gari ili kuhakiki na kujua kama gari ni salama (ikimaanisha kama gari limepata kipimo cha ubora - MOT test) na si la wizi. Unachopaswa kufanya ni kuingia kwenye website hii

1602702221241.png

Kisha bonyeza hapo kwenye mahala pameandikwa 'Start now'. Ukifanya hivyo utapata interface ya namna hii:

1602702322686.png

Ingiza namba ya usajili wa gari. Hapa nitatumia mfano wa namba ya usajili wa gari niliyoiweka hapo juu. Na ukifanya hivyo itatokea kama hivi:

Screen Shot 2020-10-14 at 21.07.21.png

Kama taarifa za aina ya gari uliloona namba hiyo ya usajili ni sahihi, basi chagua 'Yes', kisha bonyeza 'Continue'. Na utapata interfaces hizi
1602702611509.png

Screen Shot 2020-10-14 at 21.10.38.png

Hapo taarifa za msingi zote za gari utaziona.

Na jambo la nne na la mwisho, ni kuhakiki kama gari imeshawahi kurudishwa kiwandani kutokana na tatizo kubwa la kiusalama ama siyo. Kama kuna limeshawahi kurudishwa ni vizuri tu kuachana na hilo gari, hata kama unaweza kuwasiliana na mtengenezaji ili akusaidie bure katika kukabiliana na tatizo husika. Unaweza kuhakiki kama gari limeshawahi kurudishwa kupitia mtandao huu: Check if a vehicle, part or accessory has been recalled. Hapa namba ya usajili wa gari ni muhimu pia.

Cheki utakavyoona ukiingia kwenye mtandao huo:

Screen Shot 2020-10-14 at 21.44.45.png

Ingiza namba ya usajili wa gari na utaona hivi:

Screen Shot 2020-10-14 at 21.46.35.png

Kwa mfano wa hili gari, inaonyesha halijawahi kurudishwa kiwandani kwa suala lolote kubwa la kiusalama.

Ukishafanya hayo yote na ukaridhika na uhakiki, basi hapo ni kuendelea mpango wa ununuzi. Mwombe muuzaji akupatie kitu inaitwa 'log book'.
Mfano wake unakuwa hivi:

1602706133770.png

1602706134122.png

Kama nakumbuka sahihi, hiyo nyekundu ndiyo inatumika sasa. Log book ni cheti cha usajili wa gari; kwa umaarufu inajulikana kama V5C, ambayo inaonyesha nani anapaswa kulisajili na kulilipia kodi gari husika. Log book inapaswa kuwa na serial namba hapo juu na watermark iliyoandikwa 'DVL'. Sasa kutokana na wizi wa magari, serikali kupitia polisi imetoa angalizo kwamba kama log book ina serial namba kati ya BG8229501 hadi BG9999030 au BI2305501 hadi BI2800000, basi hiyo log book ni ya kimagumashi, na uwezekano ni kuwa gari ni la wizi. Hivyo achana na hilo gari haraka sana. Ukiweza wataarifu polisi wa Uingereza.

Log book itakuwa na taarifa zote za gari. Na itakuwa na taarifa za namba ya engine na chassis . Ni vizuri kuzihakiki hizi pia kwa kulinganisha kilichoandikwa kwenye log book. Kama uko mbali, mwombe muuzaji hata apige picha na kukutumia ili uone.

Nafikiri haya niliyoyaweka ndiyo mambo ya msingi kwa mtu anayetaka kuhakiki taarifa za gari lililotumika Uingereza. Mambo mengine wadau wengine wanaweza kuongezea.
 
Attachments

  • Screen Shot 2020-10-14 at 21.25.18.png
    Screen Shot 2020-10-14 at 21.25.18.png
    25.2 KB · Views: 7
  • 1602705081291.png
    1602705081291.png
    172.5 KB · Views: 8
Mkuu 5 bado mpya sana, pita CMC. Anyway ingia autotrader chagua then nitumie link. Tutaanzia hapo.
Mmh basi ngoja niombe poh mapema ngoja nibaki na 4 kwanza ila nitaomba usaidizi wako pindi nkiwa tayari pls
 
Nzi Hilo gari ambalo umeweka mfano wake siwez kuagiza kupitia be forward au SBT Japan??
Wabongo wengi ambao wanaagiza Magari ya ulaya na marekani wanapitia Sana Japan sijui ni kwasabb zipi pia ningependa kujua kuhusu gharama za kuagiza gari za European cars kutokea Japan na ulaya kwenyewe
 
Mcheki RRONDO atakusaidia zaidi
 
Nzi Hilo gari ambalo umeweka mfano wake siwez kuagiza kupitia be forward au SBT Japan??
Wabongo wengi ambao wanaagiza Magari ya ulaya na marekani wanapitia Sana Japan sijui ni kwasabb zipi pia ningependa kujua kuhusu gharama za kuagiza gari za European cars kutokea Japan na ulaya kwenyewe
Japan zipo. Magari mengi ya Ulaya yana assembly plants Japan. Hata Toyota,Nissan,Honda wana assembly plants UK na sehemu nyingine Ulaya.
 
Salaam,

Katika kujadili masuala mbalimbali yanayohusu magari, nilipata kuweka moja ya mitandao wa uuzaji na ununuaji wa magari Uingereza.
Mtandao huu unaitwa Autotrader, ni moja mitandao maarufu na ya uhakika katika kununua na kuuza magari (mapya na yaliyotumika).

Sasa ndugu Bavaria alipata kuniuliza kama nimeshawahi kutumia mtandao huo kununua gari. Nikahisi pengine ana wasiwasi na mtandao huo.
Hivyo basi, kwa msaada wake na wale wengine wote ambao wanatamani kununua magari Uingereza, nikaona nitoe kidogo uzoefu wangu katika hili.

Sina uzoefu na ununuaji wa magari Japan au sehemu zingine zaidi ya Uingereza. Hivyo ninachokisema hapa pengine kinaweza kikawa kina bias. Ila naamini hakuna sehemu salama ya kununua magari kama Uingereza. Kwanini? Sababu kubwa ni uwazi wa taarifa za gari husika.

Serikali ya Uingereza kupitia mtandao wake mkuu wa idara zote za serikali Welcome to GOV.UK, imeweka mwongozo mzuri sana kwa mtu anayetaka kununua gari lililotumika Uingereza, ili kujua kama gari ni la wizi au si salama kutumika barabarani.

Angalia mwongozo huo hapa: Check a used vehicle you’re buying. Mwongozo una mambo makuu manne:

Moja, unashauriwa kumuuliza muuzaji namba ya usajili wa gari, aina ya gari na model yake. Uzuri kwenye mtandao wa Autotrader UK, gari nyingi zilizotumika uwekwa picha zenye kuonyesha namba ya usajili wa gari. Angali mfano hapa chini:

View attachment 1600343

View attachment 1600344

Namba ya usajili ya gari hilo ni LG68 DFU.

Pili, serikali ya Uingereza kupitia wizara ya usafiri (Ministry of Transport - MOT) ina utaratibu wa kupima ubora na uthamani wa gari kutumika barabarani. Na pia kupima kiwango cha uchafuzi wa hewa wa gari husika. Kipimo hiki kinajulikana kama MOT test. Ni kipimo cha lazima. Hivyo kwa hatua ya pili, mnunuzi baada ya kuwa umemwomba muuzaji namba ya MOT test, unapaswa kuhakiki historia ya gari husika kwenye ubora na uthamani wake. Unaweza kufanya hivyo kupitia mtandao huu: Check the MOT history of a vehicle. Utakutana na interface hii:

View attachment 1600421

Kwa kuwa ushafahamu namba ya usajili wa gari unalolitaka, basi bonyeza hapo kwenye 'Start now'.

View attachment 1600423

Hapo ingiza namba ya usajili ya gari unalolitaka. Kwa leo natumia mfano wa namba ya gari hilo hapo juu. Kisha utaona hivi:

View attachment 1600432
Kama unavyooona hapo juu, kwa mfano wa gari hilo, MOT yake imeshakwisha mwanzoni mwa mwezi huu. Unaweza kuona hadi cheti chake cha ukaguzi na mahali ukaguzi ulipofanyikia. Hicho cheti pia kitakuonyesha kama namba ya MOT test aliyokupa mnunuzi ni ya ukweli ama siyo.

Tatu, katika kuhakikisha ukweli hizo taarifa, serikali kupitia wakala wa utoaji leseni za madereva na magari (Driver and Vehicle Licensing Agency - DVLA) imeweka utaratibu wa mnunuzi kuhakiki taarifa za gari kupitia website hii: Get vehicle information from DVLA. Hapa kazi kubwa ni kutumia namba ya usajili ya gari ili kuhakiki na kujua kama gari ni salama (ikimaanisha kama gari limepata kipimo cha ubora - MOT test) na si la wizi. Unachopaswa kufanya ni kuingia kwenye website hii

View attachment 1600390

Kisha bonyeza hapo kwenye mahala pameandikwa 'Start now'. Ukifanya hivyo utapata interface ya namna hii:

View attachment 1600399

Ingiza namba ya usajili wa gari. Hapa nitatumia mfano wa namba ya usajili wa gari niliyoiweka hapo juu. Na ukifanya hivyo itatokea kama hivi:

View attachment 1600408

Kama taarifa za aina ya gari uliloona namba hiyo ya usajili ni sahihi, basi chagua 'Yes', kisha bonyeza 'Continue'. Na utapata interfaces hizi
View attachment 1600413
View attachment 1600416

Hapo taarifa za msingi zote za gari utaziona.

Na jambo la nne na la mwisho, ni kuhakiki kama gari imeshawahi kurudishwa kiwandani kutokana na tatizo kubwa la kiusalama ama siyo. Kama kuna limeshawahi kurudishwa ni vizuri tu kuachana na hilo gari, hata kama unaweza kuwasiliana na mtengenezaji ili akusaidie bure katika kukabiliana na tatizo husika. Unaweza kuhakiki kama gari limeshawahi kurudishwa kupitia mtandao huu: Check if a vehicle, part or accessory has been recalled. Hapa namba ya usajili wa gari ni muhimu pia.

Cheki utakavyoona ukiingia kwenye mtandao huo:

View attachment 1600436
Ingiza namba ya usajili wa gari na utaona hivi:

View attachment 1600437

Kwa mfano wa hili gari, inaonyesha halijawahi kurudishwa kiwandani kwa suala lolote kubwa la kiusalama.

Ukishafanya hayo yote na ukaridhika na uhakiki, basi hapo ni kuendelea mpango wa ununuzi. Mwombe muuzaji akupatie kitu inaitwa 'log book'.
Mfano wake unakuwa hivi:

View attachment 1600463

View attachment 1600464
Kama nakumbuka sahihi, hiyo nyekundu ndiyo inatumika sasa. Log book ni cheti cha usajili wa gari; kwa umaarufu inajulikana kama V5C, ambayo inaonyesha nani anapaswa kulisajili na kulilipia kodi gari husika. Log book inapaswa kuwa na serial namba hapo juu na watermark iliyoandikwa 'DVL'. Sasa kutokana na wizi wa magari, serikali kupitia polisi imetoa angalizo kwamba kama log book ina serial namba kati ya BG8229501 hadi BG9999030 au BI2305501 hadi BI2800000, basi hiyo log book ni ya kimagumashi, na uwezekano ni kuwa gari ni la wizi. Hivyo achana na hilo gari haraka sana. Ukiweza wataarifu polisi wa Uingereza.

Log book itakuwa na taarifa zote za gari. Na itakuwa na taarifa za namba ya engine na chassis . Ni vizuri kuzihakiki hizi pia kwa kulinganisha kilichoandikwa kwenye log book. Kama uko mbali, mwombe muuzaji hata apige picha na kukutumia ili uone.

Nafikiri haya niliyoyaweka ndiyo mambo ya msingi kwa mtu anayetaka kuhakiki taarifa za gari lililotumika Uingereza. Mambo mengine wadau wengine wanaweza kuongezea.
Nashukuru kwa uzi kaka.

Umezidi nipa "confidence".

Ntarudi kwa mrejesho nikikamilisha mchakato.
 
Magari ya ulaya yenyewe tanatumia miles badala ta kilometres unaweza kuta gari inasoma 98,000 miles ukija kufanya conversion ni 156,800 km
 
Na kwenye dashboard ukijichanganya trafiki wanakula kichwa tu kwenye zile 50
 
Magari ya ulaya yenyewe tanatumia miles badala ta kilometres unaweza kuta gari inasoma 98,000 miles ukija kufanya conversion ni 156,800 km
Dah,hii jamaa zangu wawili wamelia sana...waliingia kichwa kichwa,zina zaidi na km 350,000...performance hovyo
 
Salaam,

Katika kujadili masuala mbalimbali yanayohusu magari, nilipata kuweka moja ya mitandao wa uuzaji na ununuaji wa magari Uingereza.
Mtandao huu unaitwa Autotrader, ni moja mitandao maarufu na ya uhakika katika kununua na kuuza magari (mapya na yaliyotumika).

Sasa ndugu Bavaria alipata kuniuliza kama nimeshawahi kutumia mtandao huo kununua gari. Nikahisi pengine ana wasiwasi na mtandao huo.
Hivyo basi, kwa msaada wake na wale wengine wote ambao wanatamani kununua magari Uingereza, nikaona nitoe kidogo uzoefu wangu katika hili.

Sina uzoefu na ununuaji wa magari Japan au sehemu zingine zaidi ya Uingereza. Hivyo ninachokisema hapa pengine kinaweza kikawa kina bias. Ila naamini hakuna sehemu salama ya kununua magari kama Uingereza. Kwanini? Sababu kubwa ni uwazi wa taarifa za gari husika.

Serikali ya Uingereza kupitia mtandao wake mkuu wa idara zote za serikali Welcome to GOV.UK, imeweka mwongozo mzuri sana kwa mtu anayetaka kununua gari lililotumika Uingereza, ili kujua kama gari ni la wizi au si salama kutumika barabarani.

Angalia mwongozo huo hapa: Check a used vehicle you’re buying. Mwongozo una mambo makuu manne:

Moja, unashauriwa kumuuliza muuzaji namba ya usajili wa gari, aina ya gari na model yake. Uzuri kwenye mtandao wa Autotrader UK, gari nyingi zilizotumika uwekwa picha zenye kuonyesha namba ya usajili wa gari. Angali mfano hapa chini:

View attachment 1600343

View attachment 1600344

Namba ya usajili ya gari hilo ni LG68 DFU.

Pili, serikali ya Uingereza kupitia wizara ya usafiri (Ministry of Transport - MOT) ina utaratibu wa kupima ubora na uthamani wa gari kutumika barabarani. Na pia kupima kiwango cha uchafuzi wa hewa wa gari husika. Kipimo hiki kinajulikana kama MOT test. Ni kipimo cha lazima. Hivyo kwa hatua ya pili, mnunuzi baada ya kuwa umemwomba muuzaji namba ya MOT test, unapaswa kuhakiki historia ya gari husika kwenye ubora na uthamani wake. Unaweza kufanya hivyo kupitia mtandao huu: Check the MOT history of a vehicle. Utakutana na interface hii:

View attachment 1600421

Kwa kuwa ushafahamu namba ya usajili wa gari unalolitaka, basi bonyeza hapo kwenye 'Start now'.

View attachment 1600423

Hapo ingiza namba ya usajili ya gari unalolitaka. Kwa leo natumia mfano wa namba ya gari hilo hapo juu. Kisha utaona hivi:

View attachment 1600432
Kama unavyooona hapo juu, kwa mfano wa gari hilo, MOT yake imeshakwisha mwanzoni mwa mwezi huu. Unaweza kuona hadi cheti chake cha ukaguzi na mahali ukaguzi ulipofanyikia. Hicho cheti pia kitakuonyesha kama namba ya MOT test aliyokupa mnunuzi ni ya ukweli ama siyo.

Tatu, katika kuhakikisha ukweli hizo taarifa, serikali kupitia wakala wa utoaji leseni za madereva na magari (Driver and Vehicle Licensing Agency - DVLA) imeweka utaratibu wa mnunuzi kuhakiki taarifa za gari kupitia website hii: Get vehicle information from DVLA. Hapa kazi kubwa ni kutumia namba ya usajili ya gari ili kuhakiki na kujua kama gari ni salama (ikimaanisha kama gari limepata kipimo cha ubora - MOT test) na si la wizi. Unachopaswa kufanya ni kuingia kwenye website hii

View attachment 1600390

Kisha bonyeza hapo kwenye mahala pameandikwa 'Start now'. Ukifanya hivyo utapata interface ya namna hii:

View attachment 1600399

Ingiza namba ya usajili wa gari. Hapa nitatumia mfano wa namba ya usajili wa gari niliyoiweka hapo juu. Na ukifanya hivyo itatokea kama hivi:

View attachment 1600408

Kama taarifa za aina ya gari uliloona namba hiyo ya usajili ni sahihi, basi chagua 'Yes', kisha bonyeza 'Continue'. Na utapata interfaces hizi
View attachment 1600413
View attachment 1600416

Hapo taarifa za msingi zote za gari utaziona.

Na jambo la nne na la mwisho, ni kuhakiki kama gari imeshawahi kurudishwa kiwandani kutokana na tatizo kubwa la kiusalama ama siyo. Kama kuna limeshawahi kurudishwa ni vizuri tu kuachana na hilo gari, hata kama unaweza kuwasiliana na mtengenezaji ili akusaidie bure katika kukabiliana na tatizo husika. Unaweza kuhakiki kama gari limeshawahi kurudishwa kupitia mtandao huu: Check if a vehicle, part or accessory has been recalled. Hapa namba ya usajili wa gari ni muhimu pia.

Cheki utakavyoona ukiingia kwenye mtandao huo:

View attachment 1600436
Ingiza namba ya usajili wa gari na utaona hivi:

View attachment 1600437

Kwa mfano wa hili gari, inaonyesha halijawahi kurudishwa kiwandani kwa suala lolote kubwa la kiusalama.

Ukishafanya hayo yote na ukaridhika na uhakiki, basi hapo ni kuendelea mpango wa ununuzi. Mwombe muuzaji akupatie kitu inaitwa 'log book'.
Mfano wake unakuwa hivi:

View attachment 1600463

View attachment 1600464
Kama nakumbuka sahihi, hiyo nyekundu ndiyo inatumika sasa. Log book ni cheti cha usajili wa gari; kwa umaarufu inajulikana kama V5C, ambayo inaonyesha nani anapaswa kulisajili na kulilipia kodi gari husika. Log book inapaswa kuwa na serial namba hapo juu na watermark iliyoandikwa 'DVL'. Sasa kutokana na wizi wa magari, serikali kupitia polisi imetoa angalizo kwamba kama log book ina serial namba kati ya BG8229501 hadi BG9999030 au BI2305501 hadi BI2800000, basi hiyo log book ni ya kimagumashi, na uwezekano ni kuwa gari ni la wizi. Hivyo achana na hilo gari haraka sana. Ukiweza wataarifu polisi wa Uingereza.

Log book itakuwa na taarifa zote za gari. Na itakuwa na taarifa za namba ya engine na chassis . Ni vizuri kuzihakiki hizi pia kwa kulinganisha kilichoandikwa kwenye log book. Kama uko mbali, mwombe muuzaji hata apige picha na kukutumia ili uone.

Nafikiri haya niliyoyaweka ndiyo mambo ya msingi kwa mtu anayetaka kuhakiki taarifa za gari lililotumika Uingereza. Mambo mengine wadau wengine wanaweza kuongezea.
Uzi mzuri sana,umeeleza vzr mno.
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom