Mambo ya Kuzingatia kabla ya kufuga mbwa

Mambo ya Kuzingatia kabla ya kufuga mbwa

Wasalaam wakuu,
Poleni na harakati za hapa na pale za kuikata keki ya Taifa ila nilikuwa na langu tatizo husika na kichwa cha habari hapo juu ningetamani kupata ya kiundani kuhusu swala hili.

Nawasilisha.
Mkuu; unapotaka kufuga mbwa zingatia yafuatayo:
1. Unamfuga kwa malengo gani? Kujifurahisha tu au pambo la nyumbani i.e. Pet dogs?
2. Ulinzi wa nyumbani au ulinzi wa mifugo yako?
Kama umechagua lolote kati ya hayo hapo juu, basi ujipange kwa yafuatayo:
1. Nyumba/Banda atakalokuwa anaishi i.e. asiachwe kuzurura la sivyo ujiandae kwa makesi mahakamani.
2. Chakula chake. Zingatia huyo ni jamii ya wanyama walao nyama (Carnivore). Mbwa aliyekomaa(Adult) hulishwa mara moja tu kwa siku lakini ale ashibe kabisa.
3. Huduma za lazima za kiafya e.g. Chanjo ya kukinga ugonjwa wa kichaa cha mbwa(Rabies), Kumwogesha (Dipping ni nzuri zaidi kuliko spraying) kwa dawa ya kuogesha mifugo mfano Albadip, Paranex n.k.
3. Mafunzo: Kama ni kwa ajili ya ulinzi afunzwe amri ya kukamata, kuachia, kusitisha au kutafuta. Kama ni wa pambo tu la nyumbani afunzwe kutulia kwenye eneo lake e.g. Kwenye kochi au kitanda chake, asile hovyo na kunya/kukojoa hovyo.
Maelekezo ya aina ya mbwa itakayo kufaa kwa malengo yako umeshapewa hapo juu. Kwa ufupi ni kwamba kumiliki mbwa ni sawa na kumiliki bunduki. Mbwa ni silaha bora zaidi kwa matumizi ya nyumbani.
5. Ni muhimu sana wewe mfugaji na Familia yako muwe wavumilivu kwa kero au changamoto zitakazoweza kujitokeza.
e.g. Anaweza kutapika, au akizaa huwalisha watoto wake kwa kuwatapikia chakula alichokula yeye, anaweza kupata maradhi kama wanyama wengine n.k.
 
Kwanaza kabisa napenda kukukaribisha kwenye ulimwengu wawapenda na ufugaji wa mbwa. 2 napenda kujuwa unahitaji kufuga mbwa kwa malengo gani? 3 unahitaji mbwa wa aina gani. 4 hapo unapotaka kumfugia pamezungushiwa uzio au pako wazi?nijibu hapo kwanza ilituweze kwenda sawa.
 
Kuhusu mbwa kula sana ni uongo mbwa anakula kiasi na sio sana. Mbwa mkubwa anakula mlg 500 chakula kilicho bora na kisafi, usiogope kusema mbwa anakula sana
 
Mkuu mm nina mbwa jike mama yake nilimnunua polisi kule Kurasini. Lkn akazaa ktk generation ya 2 hv ya mchanganyiko wa mbwa fulani hv kiuhalisia sijui ni breed gani, hvy kumzaa mbwa nilienae hapa kwangu kwa sasa. Hivyo hy si pure German shepherd. Nataka apandwe ikibidi na pure G. S au mbegu bora zaidi. Je kupandisha mbwa jike kwa mbwa hao ulionao inawezekana? Na je una mbwa aina gani? Na Dar hapa wapatikana wapi? Mimi nipo Chadibwa beach hk Kigamboni.
Mi sa hivi nnae rottweiler tuu. ku mix breed inawezekana lakini we unataka nini kikubwa? Sababu kumix kama hunatarget ya maana ni kujisumbua tu. Mi sipo dar nipo Dom
 
Kuhusu mbwa kula sana ni uongo mbwa anakula kiasi na sio sana. Mbwa mkubwa anakula mlg 500 chakula kilicho bora na kisafi, usiogope kusema mbwa anakula sana
Milligram 500 = Nusu Gram! Natumaini umemaanisha Gram 500 ambayo ni NUSU kilo.
Au mlg ina maana ingine?
 
kama ni ulinzi haswa tafuta kwanza aina ya Pitbull(sikumbuki kama waliisha ruhusiwa kuingia) au rottweiler
hakikisha wanakula wanashiiba nasema tena wanashiba
Kwa ambaye hajawahi kufuga kabisa sishauri haina hizo za Mbwa kabisa ni hatari kwake na family mara 10 aanze na Germany Shepherd
 
Mi sa hivi nnae rottweiler tuu. ku mix breed inawezekana lakini we unataka nini kikubwa? Sababu kumix kama hunatarget ya maana ni kujisumbua tu. Mi sipo dar nipo Dom
Malengo makuu hasa ni kuimarisha ulinzi wa hapa kwangu. Changamoto ya maeneo ya nyumba za beach ni kusumbuliwa na vibaka/wadokozi/wezi kwn kwa mtu anaeelekea beach njia kuu lazima apite ktk geti langu ss wamekuwa na tabia ya kuchungulia. Mwaka 2016 niliwahi ibiwa karibu kila kitu cha ndani, sio kwamba sikuwa na mbwa laa hasha. Walukuwepo mbwa wawili wasio na mikia na walikuwa mbwa wakorofi mnoooo nilinunua kampumi moja hv ya ulinzi. Bahati mbaya wale mbwa walinizoea mm tu, hivyo kuna siku sikuwepo na familia yangu ilitoka kidg mbwa wakabaki bandani tu. Wezi wakaiba ilikuwa mchana kabisaa. Ss nikawarejesha nilikowanunua na kurudishiwa pesa zangu kwa 75% ndo nikanunua German shephard ambaye nimempeleka shamba Mbande.
Kwa sasa nataka niongeze wawe wawili au watatu wa aina yyt ile tena maana vibaka wameongezeka zaidi. Utanisaidiaje kwa hili
 
Ningekushauri ununuwe mbwa wadogo wakiwa na miezi 3 au 4 na umwite mwalimu awafundishie hapo hapo nyumbani itakupa matokeo mazuri sana. Me nilifanya hivyo na matekeo yake nimeyaona
Nina gsd 2 wanasaidia sana ktk swala la ulinzi kwakweli
 
Tafuta fimbo ya muanzi au mpera akijifanya jeuri unatandika hadi anajua yeye ni mgeni tu hapo nyumbani
hahahaha..ukimchapa mbwa lazma uwe muangalifu sana maana anaweza akakungata
 
Mrejesho tafadhari. Nafikiria na mimi kufuga majibwa.
 
Utaratibu wa kufuga mbwa wa kienyeji ni huu
Tengeneza banda alaf chakula uwe unampa mara 1 tu kwa siku kiwe cha kutosha, Kama ni saa 4 usiku bas kila siku umpe chakula muda huohuo, mboga iwe nyama, au dagaa uchemshe tu bila kuweka chochote, zingatia kumbadilishia chakula
saa 06:00 hakikkisha umemrudhisha kwenye banda, zingatia usafi wa banda na kumuosha kwa dawa kila baada ya wiki 2

Hapo unatua na mbwa mzuri kwaajili ya ulinzi
 
Utaratibu wa kufuga mbwa wa kienyeji ni huu
Tengeneza banda alaf chakula uwe unampa mara 1 tu kwa siku kiwe cha kutosha, Kama ni saa 4 usiku bas kila siku umpe chakula muda huohuo, mboga iwe nyama, au dagaa uchemshe tu bila kuweka chochote, zingatia kumbadilishia chakula
saa 06:00 hakikkisha umemrudhisha kwenye banda, zingatia usafi wa banda na kumuosha kwa dawa kila baada ya wiki 2

Hapo unatua na mbwa mzuri kwaajili ya ulinzi
Mbwa wa kienyeji ndo yukoje huyo?
 
kwa Pitbul na Rotweiler mkuu kama maisha yako ni ya uswahilini na uwezo wako mdogo sikushauri.Hawa ukiwabadilishia chakula ghafla ukawa unawapa makande watakuvumilia siku ya kwanza ya tatu wanaweza kukuua wewe mwenyewe hata kuua mwanao.
Sijui nchini kwetu nchi zingine kuwafuga hadi uwe na kibali
 
Back
Top Bottom