Kwanza ! Hakikisha unalo banda la kumhifadhia huyo mbwa kama ni Wa ulinzi.
Banda inashauriwa lielekezwe upande unaochomoza jua, kwa ajili ya kukauka kwa haraka unapokuwa umelifanyia usafi kwa maana nyingine husaidia kuua wadudu( simple disinfectant)
Weka Chombo cha maji na maji muda wote, weka ubao ulio juu,juu kwa ajili ya kulalia ,kama unaeneo la kutosha mjengee chumba na sebule.
Floor yake isiwe laini saana kuepuka kuteleza, na wala isiwe rough kurahisisha usafi.na iwe na slope kidogo.
Ikiwa ni chumba na sebule ,eneo la sebule weka wavu.eneo la chumba ndo unaweza kulifunika .jenga liwe imara mbwa ana nguvu .
Ukifanikiwa hayo, tafuta mbegu bora ya mbwa, kumbuka mbwa ni aghali, na anataka matunzo.
Jiulize tena unamtaka mbwa kwa ajili ya nini?