Mambo ya kuzingatia kabla hujaanzisha biashara

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,595
215,272
Ninaongelea hizi biashara ndogo ambazo hazihitaji uwekezaji mkubwa au kuajiri wataalamu wa kukusaidia mambo ya marketing, accounts ana vitu vingine.

1. Angalia unachoweza kufanya kutoka moyoni mwako, mfano kushona, kupika, kusafisha nyumba na kupamba. Wewe mwenyewe ni mzuri kiasi gani katika wazo lako? Ikitokea uliowaajiri wakusaidie wamepata dharura unaweza kuingia front na siku isiharibike? Jibu likiwa ndiyo jiongeze.

2. Usiweke mawazo ya faida kwanza. Weka wazo la kutoa huduma katika jamii. Hiki ninachotaka kufanya kinahitajika katika hii jamii? Ni wangapi wameanza? Mimi nitakuja na tofauti gani? Ukiwa na wazo hili, hata ukipata dharura utawaza huduma kwa wateja wako.

Usifungue ofisi ili upate pa kuvalia suti na kuweka kiyoyozi. Huduma kwa jamii inaleta faida yenyewe. Mfano mzuri ni Shishi Food, anafanya kitu anachokijua na anatoa huduma kwa jamii.
 
Back
Top Bottom