Mambo ya kuzingatia hasa kwa mgeni ukiwa ndani ya jiji la Dar es Salaam

Ben Zen Tarot

JF-Expert Member
Dec 13, 2014
3,910
6,704
DAR ES SALAAM Ni jiji kubwa la kibiashara nchini Tanzania, jiji linalopatikana East Afrika pembezoni mwa bahari ya hindi. Ni jiji ambalo lina zaidi ya watu milioni 3.

Nahaya ndo Mambo ya kuzingatia zaidi ukiwa hapo..

1: Ukiwa ndani ya daladala umekaa dirishani usitoe simu na kujifanya eti unataka kuchart au unapiga picha walai nakwambia utabaki mikono mitupu. Kizazi cha panya road bado kinasurvive.

2: Kama upo barabarani na ukasikia mtu anakusarimia na anakusogerea kutokea nyuma yako usimwitikie nasema USIMWITIKIE..

3: Mzee mwenzangu ukikuta watu wanapigana we waache jari Mambo yako, NARUDIA TENA JARI MAMBO YAKO.

4: Kwa wiki ya kwanza jifanye kolo tembea na wenyeji wako mzee mwenzangu hasa wale wanaofahamika pale.

5: Unapotembea usitembee kiustaarabu au kiheshima saaana bali jaribu kutembea kama gangster yaani tembea kama mhuni fulani ivi wa kitaa watu watakuona ni mwana hawatakusogelea.

6: Kwenye kuvuka barabara jifanye Ronaldo, najua hawawezi kukugonga ila jifunze jinsi ya kuvuka magari mengine tumia staili ya kudribo.

7: Ukiona kundi la watu wanakimbia usisubiri na wewe kimbia kisha uliza je kuna usalama

8: sehemu yenye msongamano wa watu shikilia simu yako kwa nguvu mkononi, asiweke kwenye bag au mfukoni.

9: Ukitaka kuulizia mwelekeo;, anza na neno samahani naomba kuu... au tafadhali...

Nje ya hapo utawachukia watu bure, Dar watu wanahasira...

10: Usicheze cheze kila mziki unaousikia, usimwongeleshe mtu ndani ya daladala watakujua usije ukajulikana wa mkoani mana ndo wanavyosema, acha wao ndo wakuanze.

11: Usinunue simu iliyofungashwa kwenye boksi maana mwisho wa siku utajikuta umenunua sabuni.

12: Na mwisho Dar es salaam ni jiji lililojaa comedian bila shaka utafurai ukiwa unakatiza mitaa ya uswahilini.

Dar es Salaam ni mji mzuri sana na mtam pia endapo tu utafata mfumo unavyotaka.

Sio sehemu mbaya ni sehemu inayotaka uwe SMART Na mwenye BUSARA
 
DSM hii imejaa washamba kibao kuanzia Uswahilini hadi ushuwani

Utofauti ni kuwa utanunua Dada poa na kaka poa kwa bei ndogo.
 
Mwezi ujao nitakuwa huko mjini, nitakuwa kigangster kama ulivyo shauri...

Hata jina nitabadalisha "That Gangster"
Karibu mkuu, ukienda sehemu za kula bata kama upo na gari pale ulipopark ukikuta watu wasalimie alafu waachie hata buku gari yako utaikuta salama, lakini pia kama uko kwa mguu na unatoka kiwanja hasa usiku mnene vua shati ( wahuni sio watu)
 
Back
Top Bottom