Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 65,010
- 111,399
1. Kuachana rasmi na uwekezaji wa umeme wa Maji. Mipango yote ya umeme sasa ielekezwe kwenye gesi, nuclear, solar, geothermal, upepo n.k Umeme wa maji kutegemea mvua ni kijima na uliopitwa na wakati.
2.Viwanda vizito na vikubwa, hakuna namna tatizo la ajira hasa kwa vijana litatatiliwa nchi hii bila viwanda vikubwa na vingi. Vinginevyo vijana wataendelea kuwa bodaboda, wamachinga na vinyozi tu kwa wingi.
3. Ugatuzi wa madaraka; Hata kama katiba mpya haitapatikana milele, hii iliyopo inapaswa kurekebishwa kupeleka nguvu zaidi za kufanya maendeleo katika Halmashauri. Ni vigumu nchi hii kuendelea kwa kasi inayotakaiwa kwa mfumo centralized tulio nao ambapo waziri wa ardhi kutoka Ukonga ndiye anategemewa kutatua mgogoro wa ardhi Ushirombo.