Ma-CCM na Team Makonda wanataka kuaminisha watu kwamba sakata la mashoga lilianzishwa makusudi na Bashite ili kuwandoa watu kwenye mstari kuhusu suala la Mo!
Danganyaneni huko huko! Unless kama serikalini kumejaa vilaza ndipo wanaweza kucheza blunder kama hiyo ambayo mwisho wa siku imewafanya watafutane kwa tochi mchana wa jua kali!
Kila mwenye akili timamu anafahamu Makonda alimaanisha kwa sababu pale ndipo ilipoishia akili yake!!
Labda tu niwakumbushe kwamba, suala la Mo liilishakosa mvuto kwa sababu Watanzania ni watu wa matukio na tukio ambalo lilikuwa lina-trend ni issue ya Wema Sepetu na Amber Rutty!
So, unless kama serikalini kumejaa vilaza, ndipo ingeweza kuchukua uamuzi wa kuwatoa watu kwenye mstari kwa kutumia issue sensitive kama ya ushoga wakati suala la Mo lenyewe lilishadoda na watu walikuwa wanahangaika kutafuta video za Wema Sepetu na Amber Rutty!
Unless kama serikali imejaa vilaza ndipo ingeweza ku-stage suala la ushoga wakati wanafahamu moto wake kuzimika sio rahisi hadi hatimae wanaamua kuchukua hatua za kukiri hadharani kwamba kumbe ushoga Tanzania unaruhusiwa!
Narudia, Makonda alimaanisha! Alimaanisha kwa sababu ni mtu wa kurukia mambo bila ya tafakuri!