Mambo ya kushangaza kuhusu kujamba

dirtyboy

JF-Expert Member
Sep 16, 2017
377
666

Kwanini tunajamba? kwanini "ushuzi" unanuka? Kujamba inaweza kuwa kitendo cha aibu kwa wengi wetu,lakini inaweza kukufanya ujisikie vizuri kujua kwamba ni tendo la kawaida sana kwa mwili wa binadamu kutenda. Kila mtu anajamba,hata Sky Eclat nae hujamba.

1. Kujamba ni nini hasa?
Kujamba kunasababishwa na kubanwa kwa hewa,ambayo inaweza kutoka mwilini kwa njia nyingi. Baadhi ni hewa tuliyoimeza wakati wa kula au kunywa. Hewa ingine husababishwa na gesi kuingia kwenye utumbo wetu kutoka kwenye damu, na baadhi ya gesi huzalishwa na kemikali katika utumbo au bakteria.Kwa kawaida "ushuzi" unakua na asilimia 59 ya gesi ya nitrogen, asilimia 21 ni hydrogen, asilimia 9 ni carbon dioxide, asilimia 7 methane na asilimia 4 ni oygen.

Asilimia moja tu ya "ushuzi" inaweza kuwa hydrogen sulfide na mercaptans,ambayo ndio ina sulfur ndani yake,sulfur ndo hufanya "ushuzi" utoe harufu mbaya Kujamba huambatana na sauti,hii ni kutokana na "vibration" katika njia ya haja kubwa.Ukubwa wa mlio wa kujamba hutegemea "presha" inayosukuma gesi itoke nje na pia ugumu wa misuli ya njia ya haja kubwa.

2. Kwa nini Ushuzi hutoa Harufu mbaya?
Harufu mbaya ya ushuzi hutegemea na ulaji wa mtu, vyakula vyenye sulfur kwa wingi ndio husababisha hili. Vyakula vyenye sulfur kwa wingi ni kama maharage, kabichi, soda na mayai.

images (6).jpeg


3. Watu hujamba hadi mara 14 kwa siku
Mtu wa kawaida hutoa hata nusu lita ya ushuzi kwa siku 😂😂. Inasemekana mtu akijamba mfululizo kwa kipindi cha miaka 6,anaweza kuzalisha nishati ya kutosha kutengeneza bomu la atomiki.😎

4. Ushuzi husafiri kwa mwendo wa futi 10 kwa sekunde
Harufu ya ushuzi huanza kusikika sekunde 10-15 baada ya mtu kujamba,hiyo ni kwa sababu inachukua muda mrefu kwa harufu kufikia pua. (Kwa mtu mnene kama Kiduku Lilo inaweza chukua hata nusu saa😂😂)

5. Kujizuia Kujamba Inaweza Kuhatarisha Afya Yako
Madaktari hawajakubaliana moja kwa moja kama kujizuia kujamba ni hatari kiafya.Baadhi ya wataalam wanafikiri kujamba ni sehemu muhimu katika mfumo wa mmeng'enyo wa chakula,hivyo kujizuia kujamba haitakuletea madhara.Wengine wanadhani kwamba kujizuia kujamba kunaweza kusababisha tumbo kujaa gesi, na pia inaweza sababisha kikundu(hemorrhoids).

kujamba-2-300x174.jpg


6. Kwa Baadhi ya Tamaduni, Kujamba Sio Ishu
Wakati tamaduni nyingi zikichukulia tendo la kujamba lifanywe kistaarabu, kuna baadhi ya tamaduni hawaoni haya kujamba hadharani, na pia hufurahia tendo hilo. Mfano kabila la Yanomami huko America ya Kusini,kwao husalimiana kwa kujamba,na China unaweza kupata kazi ya kunusa ushuzi! Katika Roma ya zamani, Mfalme Claudius akihofia kwamba kujizuia kujamba inaweza kuwa hatari kiafya, alipitisha sheria kwamba ni ruhusa kujamba kwenye "banquets".

Swali kwako.

Je, ulishawahi kujamba sehemu ambayo ukahisi hukustahil kufanya hivyo iwe kwa bahati mbaya au kukusudia?
 
Niliendaga kijijini BK huko nipo mdogoo. Wakati wa kula sasa kiherehere changu kikanipeleka kula kwa wakubwa badala ya kula na watoto wenzangu.Wakati wa kula mtu mzima akajamba kofi nikapewa mimi dah! Halafu na kufokewa juu.Baada ya msosi mama akanifuata kunibembeleza. Nikamwambia siwezi kukaa huku tuondoke.Ndani ya siku mbili tu tukarudi Mwanza.

Yaani wakubwa starehe yenu halafu makofi mtupige sie! Tamaduni za ajabu sana!
 
Niliendaga kijijini BK huko nipo mdogoo.Wakati wa kula sasa kiherehere changu kikanipeleka kula kwa wakubwa badala ya kula na watoto wenzangu.Wakati wa kula mtu mzima akajamba kofi nikapewa mimi dah! Halafu na kufokewa juu.Baada ya msosi mama akanifuata kunibembeleza.Nikamwambia siwezi kukaa huku tuondoke.Ndani ya siku mbili tu tukarudi Mwanza.
Yaani wakubwa starehe yenu halafu makofi mtupige sie! Tamaduni za ajabu sana!
😂😂 Mku umenikumbusha jirani yetu mmoja kipindi chanyuma , aliku akiwaadhibu wanae wasiposema "afya ya baba" pindi anapojamba
 
Niliendaga kijijini BK huko nipo mdogoo. Wakati wa kula sasa kiherehere changu kikanipeleka kula kwa wakubwa badala ya kula na watoto wenzangu.Wakati wa kula mtu mzima akajamba kofi nikapewa mimi dah! Halafu na kufokewa juu.Baada ya msosi mama akanifuata kunibembeleza. Nikamwambia siwezi kukaa huku tuondoke.Ndani ya siku mbili tu tukarudi Mwanza.

Yaani wakubwa starehe yenu halafu makofi mtupige sie! Tamaduni za ajabu sana!
ila ulikuwa na adabu angekuwa mtoto mwingine angesema sio Mimi, kwetu mtoto alisingiziwa na huyo Mzee walikuwa wazee wengi nayeye alikuwa na Baba yake, asubuhi yake huyo Mzee kamfuata twende ukale chakula mtoto ulinitoa aibu kamchinjia na kuku kabisa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom