Mambo ya "Dinner Suit" Mbugani: Diamond Platinum | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mambo ya "Dinner Suit" Mbugani: Diamond Platinum

Discussion in 'Jamii Photos' started by ngoshwe, Oct 14, 2012.

 1. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #1
  Oct 14, 2012
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  DIAMOND PLATNUMZ APIGA KAMPENI NGORONGORO CRATER......

  DIAMOND PLATNUMZ APIGA KAMPENI NGORONGORO CRATER...... | This is Diamond


  SANII wa muziki wa kizazi kipya,Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz' amewataka watanzania kulipigia kura bonde la Ngorongoro kuwa moja ya maajabu saba ya Afrika na pia kujenga tabia ya kutembelea vivutio vya utalii vya ndani.
  Akizungumza mjini Ngorongoro, Diamond ambaye alikuwa huko kujionea bonde hilo ambalo ni la kipekee ulimwenguni, amesema hakuwahi kufikiria kwamba kuna sehemu nzuri ambayo hata watanzania wanaweza kwenda kutembea na kujionea vivutio vilivyopo.
  "Hii ni mara yangu ya kwanza kufika hapa, lakini kwa kweli nimeshangazwa na jinsi palivyo pazuri, wanyama, mito ambayo inapita huku chini, mi huwa naona kwenye televisheni tu katika kile kipindi cha National Geography cha DSTV lakini sikujua kama mambo haya yapo kweli kwetu.
  "Nawaomba watanzania wenzangu waweze kutembelea Ngorongoro na vivutio vyetu vya utalii kwa sababu kuna mengi ya kujifunza, leo kama isingekuwa Afrika sidhani kama kungekuwa na kipindi kama National Geography, na gharama za kuja huku si kubwa, hatupaswi kuogopa, hivi ni vitu ambavyo vinawezekana kabisa suala ni kujipanga," amesema.
  Amesema wenzetu kutoka Ulaya wamekuwa wakijipanga kuweza kutembelea sehemu Fulani jam bo ambalo linawafanya waweze kutembelea nchi nyingi kufanya utalii.
  "Pamoja na kuja kupunguza mawazo lakini sehemu kama hii inasaidia kuelemisha, mwito wangu kwa watanzania wenzangu, mashule hata vyuo waweze kuja hapa, inakuwa rahisi zaidi kumfundisha mtoto kuhusu Simba, Twiga, au bonde la Ngorongoro kwa kumuonyesha hiki kiko hivi, nadhani kama watoto watakuwa wanasoma kwa vitendo hawawezi kushindwa mitihani yao kwa sababu kumbukumbu inabaki kichwani kwa kile walichokiona," amesema.
  Msanii huyo alikwenda Ngorongoro baada ya kumalizika kwa tamasha la Fiesta ambapo alikuwa mmoja wasanii waliofanya vizuri. Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro ilimualika Diamond huko. Ngorongoro ni moja kati ya vivutio vya Tanzania vinavyotakiwa kupigiwa kuingia katika maajabu saba ya Afrika
  [​IMG]


  [​IMG]
  [​IMG]
  [​IMG]
  [​IMG]

  [​IMG]

  [​IMG]

  [​IMG]
   
 2. Root

  Root JF-Expert Member

  #2
  Oct 14, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 26,146
  Likes Received: 12,854
  Trophy Points: 280
  Ni vizuri ila jamani picha ya sita angalia anapiga ile diamond kama ya jay z sema kwa kificho
  Hata mm pia nitaenda maana ndio mbuga pekee imebakia na kilimanjaro

  Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
   
 3. U

  Ubungo JF-Expert Member

  #3
  Oct 14, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 1,239
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Mkuu, mjini Ngorongoro ndio wapi?
   
 4. Dotworld

  Dotworld JF-Expert Member

  #4
  Oct 14, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 3,929
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  ngoshwe

  Ukiona mtu anatumia NGUVU nyingi KUANDIKA huku ametoa ulimi nje .... nafikiri kuna tatizo la kutokupitia madarasa mengi!

  Alafu hapo anaandika Jina lake TU kwenye kitabu cha wageni!

  Hivi huyu jamaa ameishia Darasa la Ngapi?

  [​IMG]
   
 5. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #5
  Oct 14, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,905
  Likes Received: 2,324
  Trophy Points: 280
  Sasa huyo si limbukeni?
  Kwani anajua kwamba kavaa dinner suit?
  Juzi tu alikuwa akiflassh mpododo kama hana akili nzuri.

  Ndo mambo ya kuiga bila kusoma au kuelewa hayo.
   
 6. M

  Mengulu Member

  #6
  Oct 14, 2012
  Joined: Oct 13, 2012
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tatizo ni mifumo tunayoitumikia.Huyu Kijana hajapata miongozo sahihi ili kuweza fikia kilele cha mafanikio.Hana meneja mwenye utimamu kabisa
   
 7. snowhite

  snowhite JF-Expert Member

  #7
  Oct 14, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 14,174
  Likes Received: 2,136
  Trophy Points: 280
  wakiambiwa wawaulize wenye fani zao wanaona ni ujinga,ndo mana anweza kuvua pichu jukwaani since hajui inamchora yeye ni nani,sasa hili la dinner suit mbugani na lenywe mh!
   
 8. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #8
  Oct 14, 2012
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Ni dhahiri kuwa anafanya shooting ya video au picha maalum hapo, kwa hiyo suala la amevaa suti mbugani halihusiki hata kidogo
   
 9. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #9
  Oct 14, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,463
  Trophy Points: 280
  huyu jamaa tunamchukulia 'way serious' than he deserve
   
 10. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #10
  Oct 14, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  Hivi anajua kuandika huyu
   
 11. Nicole

  Nicole JF-Expert Member

  #11
  Oct 14, 2012
  Joined: Sep 7, 2012
  Messages: 4,284
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  duh dinner sut mbugan? Mie nimefanya tour kibao mbugan tarangire, manyara, kinapa cjaona watalii wakipiga suti, labda ni kwa ajil ya tangazo bt hajawa realistic!
   
 12. Wingu

  Wingu JF-Expert Member

  #12
  Oct 14, 2012
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,326
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Umeona ehh suti mbugani huyu dogo hajijui
   
 13. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #13
  Oct 14, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,463
  Trophy Points: 280
  Mbona mnamsakama hivyoo?

  wabongo wangapi wanazijua hata hizo dinner suits?
  au kuvaa suits often?
   
 14. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #14
  Oct 14, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,033
  Trophy Points: 280
  mbung'o hang'ati suti.......
   
 15. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #15
  Oct 14, 2012
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,937
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Dah umesema kweli..haka ni kaugonjwa ketu wabongo. Hatujui tutokelezee vipi na wapi..
   
 16. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #16
  Oct 14, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,463
  Trophy Points: 280
  wengi suti siku ya harusi na siku ya kifo

  utaalamu tutatoa wapi?
   
 17. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #17
  Oct 14, 2012
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,937
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Ukizingatia Dar joto..sasa akipata kachansi sehemu ina baridi inabidi atumie hata kama sio mahala pake
   
 18. MadameX

  MadameX JF-Expert Member

  #18
  Oct 14, 2012
  Joined: Dec 27, 2009
  Messages: 7,847
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Kweni hawana wapambe wakuwashauri kwenye hizi swaga
   
 19. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #19
  Oct 14, 2012
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,937
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Hayo mambo wanaweza wenzetu. huwa wanaajiri wataalamu kwa ajili hiyo. itabidi tuanzishe fasheni polisi ya kibongo
   
 20. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #20
  Oct 14, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,605
  Likes Received: 6,175
  Trophy Points: 280
  Obviously "mashikolo mageni", but, can he live?
   
Loading...