Hii hapa post yenyewe;
Nakubaliana nawe kabisa mkuu.
Ni kweli Marekani na U.K zinatuhumiwa kuleta vurugu sehemu mbalimbali duniani ili kushinikiza maslahi yake na wamekuwa wakileta vita nchi nyingi ilimradi kama vurugu inasaidia maslahi yao.
Hata hivyo jamaa si wapuuzi kivile,ni wakoloni na wezi wazoefu tangu enzi. Wanachotazama ni mazingira ya eneo husika kama panahitajika vita au amani ili kudumisha maslahi yao.
Ukitazama Tanzania,wananchi wake wako chini mno katika kutambua na kudai haki zao.
Hali hiyo ndio inayoipa Tz sifa ya utulivu wa muda mrefu.
Watz wanahitaji basic needs fulani tu ili waione dunia ni pepo,ukiwapa hizo hata ukiwaibia they dont care.
Hii inaifanya Tz kuwa very special case.
Serikali iliyopo madarakani Tanzania hivi sasa,hasa kuanzia awamu ya tatu hadi ya nne,imekuwa ikiharibu uchumi wa watz walalahoi kufikia kiwango cha kuwastusha na wameanza kujitambua taratibu.
Serikali hii haijui kula na kipofu.
Wamarekani wanalijua hili vizuri,so usishangae wakajenga uhasama na serikali hii,kwani wanaona kwamba dalali wanayemtumia atawagharimu kutumia nguvu kulinda maslahi katika siku za usoni,mahala ambapo pasingekuwa na ulazima wowote kufanya hivyo,kama dalali huyo,angejua namna ya kula na kipofu.
Tena C.I.A wanaweza kutumia scenario hiyo kujenga trust kwa watz before it's too late,kwa kuipiga vita serikali inayochukiwa na watz wengi,wakapandikiza mtu wao katika mazingira yanayokubalika na watz,wakampa support,wakampaisha,wakamuingiza kwenye siasa zenu kisiri,mkampigia kura na kujipatia "Yeltsin" wenu,mkaanza kuongozwa kwa remote from Washington bila kujua,tena mkaridhika nae kwa kuwa kafundishwa namna ya kula na kipofu,na U.S ikatumia nguvu ndoogo kudumisha maslahi yake ndani ya Tz kwa miaka mingi hadi kitokee kizazi cha wenye macho badala ya vipofu,huku na wao wakiwa wameshaiba sana.
So,tusifikiri wakati wote mmarekani anataka vita,no,kuna wakati anataka amani kabisa ikiwa amani ndiyo tool nzuri kulinda maslahi yake kulingana na eneo husika unless eneo hilo halina umuhimu mkubwa sana kwake.
Kwa jinsi tabia ya utulivu ya watz ilivyo,tena walivyo consistent kwenye tabia hiyo,nina wasiwasi kama C.I.A wanafurahia ukandamizaji wa "mchana kweupe" unaofanywa na hawa mafisadi wetu,kwa sababu utaondoa utulivu wa watz mapema mno,bila ulazima wa kufanya hivyo.
Na utulivu wa watz ni wa wajinga,so ni tool nzuri kuwaibia.
We waachie uchumi wa kuchangia harusi,kucheza ngoma,kununua Toyota ipsum,kujenga nyumba ya vyumba viwili,kula kitimoto,bhaas,utaiba mafuta bila kuulizwa,tena watakusaidia uyabebe vizuri.
Kwa hiyo CCM huenda wako kwenye wakati mgumu sana,hawakubaliki na wananchi,hawapati support ya "mabwana wakubwa" wa dunia,kilichobaki ni hao wakubwa kuwatengenezeeni "Yeltsin" wao wampigie debe mumkubali kabla wananchi hamjajitengenezea "Yeltsin" wenu,kitu ambacho kitakuwa ni worst case scenario kwa mafisadi wote,wa ndani na nje.
Na maneno ya uzi kama huu,ikiwa mleta mada ni mwandani wa serikali,basi "wambea" tumeanza kunusa harufu kuwa serikali yetu ipo juu ya misumari ya moto,inatapatapa.
Hata huyo Putin si mjinga,KGB wake watampa mrejesho ili ajue wabongo tulipishana wapi na wazungu wenzie,halafu atafanya maamuzi akiwa influenced na factor hiyo pia.
Sidhani kama mbia wa biashara asiyekuamini ni mzuri kwako,ataishi nawe kwa tahadhari iliyopitiliza ambayo muda wowote ukijichanganya anaweza kukutia hasara kubwa.
Tabia ya ufisadi uliopitiliza ya viongozi wetu imevuka mipaka na kutoaminika hata na hawa wezi wenzao wa kimataifa.
Hata wizi nao unahitaji kuwa smart ili uwe mwizi wa kudumu.