Mambo saba yanayoleta mahaba katika ndoa

As Salafiyyu91

JF-Expert Member
Jan 11, 2014
2,537
2,530
Wakuu,

Kuna baadhi ya mambo wanandoa wengi wamekuwa wakiyachukulia kuwa ni mambo madogo ila kiuhalisia ukiyafanya sio mambomadogo yafuatayo ni mambo saba yanayoleta mahaba katika ndoa.

1- Mtolee salaam mumeo/mkeo na umpe mkono kila anaporudi kutoka kazini au matembezini.

2- Muulize mumeo/mkeo unapenda nikuite kwa jina gani?Muite kwa jina alipendalo.

3- Jenga tabia ya kumpiga busu mumeo/mkeo mara kwa mara.

4- Kaa na mumeo/mkeo wakati wakula au kuleni pamoja.

5- Kilaukitoka matembezini mletee zawadi hata kama kidogo.

6- Wafanyie wema wazazi wa mumeo/mkeo kama unavyowafanyia wazazi wako.

7- Akipendeza mumeo/mkeo mwambie hongera/umependeza mume wangu/mke wangu na umbusu"ndoa idumu.

Tuma ujumbe huu kwa wanandoa kwani shetani amekazana kuvunja ndoa zetu.
 
Mahaba ili yanoge wala haina formula...unaweza ukaambiwa utembee kichurachura kila unapomuona lakini jamaa bado atazingua tu
 
Lakini pia kuomba samahani(wanaume hapa mjitahidi jmn,hata nyie huwa mnatukosea), kutoa poleh na kusema ahsantee
Yanasaidia sana
 
nasikia unaweza kumfanyia hayo na mengine mazuri lakini kuchepuka haachi, hasa wanaume sijui wamelogwa na nani?
Tatizo nyinyi wadada mnathani kuchepuka kwamba tunawakomoa. Sisi tuko busy tu na mambo yetu wala hatuna lengo la kutaka kuwaumiza. Ajali kazini tu.
 
Mahaba ili yanoge wala haina formula...unaweza ukaambiwa utembee kichurachura kila unapomuona lakini jamaa bado atazingua tu

Wew ndo unasena hayana formula lakin wanaowafanyia Haya waume zao wao ndo wanajua ukweli was mambo
 
Lakini pia kuomba samahani(wanaume hapa mjitahidi jmn,hata nyie huwa mnatukosea), kutoa poleh na kusema ahsantee
Yanasaidia sana
Hapo sasa ndo inaingia dhana ya upendo hakikisha unaishi kwenye ndoa na mtu ambaye mnapendana sio wew unampenda alafu yeye hakupendi kwasababu Mara nyingi mtu hujiepusha kumkwaza Yule ampendae na ikitokea basi humuomba msamaha
 
hayo mambo nayaonaga kwenye maigizo ila kiuhalisia magum
Hapana tatzo wanawake wengi huwa hawawafanyii haya waume zao alafu haya yanafanywa na house girl mwisho wa siku jamaa anachepukia kwa HG badilikeni!!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom