Mambo niliyojifunza katika ndoa

Mambo niliyojifunza katika ndoa

Grand Canyon

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2020
Posts
547
Reaction score
1,193
Ndoa inajengwa kwenye msingi wa ukweli, uwazi na kuaminiana.

Ni jambo jema mke/mume kujua kazi yako, unapofanyia kazi na hata kipato chako, lakini kuna mambo ukiyaweka wazi tatizo litatokea.
Mfano wapenzi hupenda kuuliza maswali kama vile: uliwahi kudate wanawake wangapi? Kama idadi ni kubwa na ukataja atataka ajue ni akina nani? Ikitokea amewajua hilo linakuwa tatizo. Utaulizwa kwa nini ulimwacha yule ukanioa mimi? Mbona ni mrembo kuliko mimi?

Kwa hiyo ikiwa hajui historia yako ya kimapenzi: Tafadhali usimweleze. Ukilazimika kumweleza hakikisha huyo mtu hamjui na anaishi mkoa au nchi ya mbali.
 
Kama ni hayo tu uliyo yataja, basi nitoshe tu kusema kwamba bado kuna mengi sana ambayo haujajifunza kuhusu ndoa na taratibu utayafahamu na kujifunza karibu kila siku hadi siku ya mwisho wa uhai wako.
 
Bado najifunza,huu mwaka wa 3 tu!
 
Siwez kuuliza hayo maswal japokuwa ntatamani sana kumuuliza, ifike wakati tufahamu kuwa kwenye safar ya mapenzi kuna ajali ndogo ndogo kama hy point ya mada
 
Bado najifunza,huu mwaka wa 3 tu!
Miaka mitatu haitoshi mkuu, kuna waliokaa kwenye ndoa hadi wamestaafu na bado wanaendelea kujifunza aiseeee.
Ndoa sio Jambo la kujadili kirahisi na kujiona mjuvi chief...
 
Hili ni somo la mwezi mmoja baada ya ndoa, ngoja hata mwaka, there is a lot to learn!
 
Nina mwaka wa 9 katika ndoa ,kitu nilichofanikiwa Nikutokumweleza mke wangu mahusiano yaliopita ,wala yeye kumuuliza maisha yake yaliyopita ,na kama anasikia nilikuwa na husiano ni kwa watu ,ila sijawai mthibitishia kwa kinywa chango ,wala kumweleza maisha yangu ya mahusiano kabla yake ...
Hili limenisaidia sana tena sana ,kuepusha migogoro au wivu wa kipuuzi. maana hata mie sitaki kujua alikuwa ana date na nani au maisha yake ya mahusiano yalikuweje n.k ,nachoangalia tuko wote ....vishiiii....

Wakati mwingine hizi stori za kwamba ulikuwa na nani sijui na nani huwa zinaacha majeraha sana katika mioyo ya watu ,na wakati mwingine ikitokea mhusika ana mjua au mko karibu au ikatokea siku anakutana nae .ndipo tabu huanza
 
Uko sahihi.
 
Sawa ni agano sasa kwanini makundi haya wanaosali wasiosali mashekhe kwa wachungaji japo siyo wote hawafurahii hilo agano?
Samahani mkuu, mimi sijaongelea dini, mashehe, wachungaji na wanao sali and usinilazimishe nitoke nje ya mada.
Hapa tunazungumzia NDOA
 
Back
Top Bottom