Msaada katika ndoa yako: Elimu asilia ya saikolojia ya mwanamke na mwanaume

monjozee

Senior Member
Sep 19, 2016
115
297
ELIMU YA BURE YA ASILI NA SAIKOLOJIA YA MWANAMKE NA MWANAMUME (Kwa kifupi).

Andiko hili, nimeliandika kwa usaidizi wa karibu wa kitabu cha Dr.JOHN GRAY kinachoitwa "MEN are from MARS, WOMEN are from VENUS".

Kumekuwa na migogoro mingi katika familia nyingi, ikihusisha malalamiko ya aidha; (a) Mwanamume hamsikilizi mwanamke.
(b) Mwanamume au mwanamke kutaka kumbadilisha mwenzake (ili wafanane kitabia, kimwenendo na kifikra).
Je, hili linawezekana? jibu ni HAPANA.

Katika kitabu chake Dr. Gray anatoa mifano (dhahania) kwa kumfananisha mwanamume kama mtu aliyetokea Sayari ya MARS,ambapo kule wanaamini sana na kuthamini vitu vifuatavyo;

Uwezo binafsi, ujasiri wa kuthubutu, kutambulika kwa kumiliki vitu na kujitofautisha katika jamii kwa kuwa na mali nyingi, kuwa mtawala (hawapendi kutawaliwa), mtu mwenye kupenda kutoa suluhisho badala ya kutafuta kwa mtu mwingine na mwisho watu wasiojali sana wala kuyapa kipaumbele mahusiano ya kimapenzi.

(Mwanaume yeyote anapaswa kuwa wa kariba hii, kwa mujibu wa Dr. Gray),na wanaamini juu ya mambo yanayoonekana (tangible objects).

Dr. Gray anamuweka mwanamke katika udhahania huo huo wa kutokea sayari ya VENUS.

Katika sayari hii, wao kama wanawake wanaokaa huku, wanathamini na kuzingatia vitu vifuatavyo;

Kuthamini hisia zake,hupenda kumbadilisha mtu ili afanane nae,kimtazamo,kiimani na kimatendo.

Pia, ni mtu anayependa kushirikisha mwenzake matukio na matatizo (sharing of events and problems), anayependa sana kuongelea matukio kuliko mawazo (ideas).Mwanamke katika sayari ya MARS anapenda sana kumshirikisha mwenzake shida zake lakini hahitaji suluhisho la haraka.

KWANINI WANAWAKE NA WANAUME HUTOFAUTIANA KATIKA NDOA?

Kutokana na maelezo ya hapo awali juu ya utofauti wa watu hawa, ni dhahiri kuwa utofauti wao hujitokeza wakati wa utatuzi wa "MATIZO".

Mfano; Mwanamke anapopata tatizo anahitaji kumweleza mwanamume,lakini kitu cha kwanza anachohitaji ni kusikilizwa,kabla ya kupewa "SULUHISHO".
Lakini kunatokea utofauti kwa mwanaume wa sayari ya VENUS,ambaye yeye hana muda wa kumsikiliza mwanamke,maana yeye mara nyingi anawaza "ideas" haruhusu sana kusikiliza matukio.

Hivyo utamkuta,badala ya kumsikiliza mwanamke, yeye hukimbilia kutoa "Suluhisho" kabla ya kumsikiliza mwanamke,ambalo ndilo "hitaji" lake kubwa.

Pili, wakati mwanamke anahitaji ukaribu na mume wake (intimacy), mwanaume yuko busy kuwaza "mzunguko wa biashara zake" kumbuka ni kawaida katika sayari ya MARS, wakati ni tofauti katika sayari ya VENUS (kwa wanawake).

Kwa upande wa mwanamume anapopatwa na tatizo, hahitaji kushirikisha mwanamke maana kumbuka kule kwao "mwanamume huheshimiwa kwa kutatua tatizo peke yake" (self-centered).

Hapa mwanamke hujaribu kumlazimisha mwanaume amueleze nini tatizo (kama wanavyofanya kule VENUS),lakini mwanamume huishia kumjibu "HAKUNA TATIZO".Majibu haya humfanya mwanamke ajione kama hapendwi, hathaminiwi na hana nafasi kwake pengine kudhani kuwa mumewe anae mwanamke mwingine ambaye humweleza matatizo yake, kumbe mwanamke hajui kuwa asili ya wanaume ni kutatuwa matatizo yao bila kushirikisha.

NINI KIFANYIKE?

Ni kila mmoja amuelewe mwenzake,amkubali na amvumilie katika utofauti huo, bila kutengeneza hisia zingine zilizo nje ya ukweli huu.

Joseph Mohonia Politician
 
Sawa kabisa na dunia ya sasa ndio maana tunashindwana kabisa wa MARS hawezi kuishi VENUS
 
Mada ni nzuri ila cha kushangaza haikupata comments nyingi tofauti na zingine ambazo sometimes zinakuwa hazina mashiko.

Tena kwa hapa bongo KE wengi wanapenda kuendekeza maisha ya kitamthilia zaidi huku wakisahau ME wengi hawana muda wa kubembeleza sana wako busy na mihangaiko ya kuingiza vipato
 
Back
Top Bottom