Mambo nane kuhusu wabunge Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mambo nane kuhusu wabunge Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Duncan, Oct 10, 2010.

 1. D

  Duncan Member

  #1
  Oct 10, 2010
  Joined: Sep 26, 2010
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  1​
  1. Utangulizi​
  Bunge la Tanzania ni moja ya taasisi muhimu sana nchini. Umuhimu wa Bunge
  unadhihirishwa na mgawo wa fedha zinazotengwa kwa ajili ya Bunge. Kwa mwaka wa
  fedha 2009/10 kiasi cha bajeti kilichotengwa kwa ajii ya Bunge ni Sh bilioni 62. Kwa kuwa
  kuna jumla ya wabunge 320, kiasi hiki ni wastani Sh million 194 kwa kila Mbunge.
  Wabunge wengi (231) wanachaguliwa na wapiga kura kwenye majimbo yao, lakini idadi
  kubwa (88), au karibu asilimia 28 ya wabunge wote, ni wa kuteuliwa: wabunge 75 ni
  wa viti maalum na wabunge 5 wawakilishi kutoka Baraza la Wawakilishi Zanzibar. Kwa
  nyongeza Bunge linajumuisha pia wabunge 8 wa kuteuliwa na Rais mmoja wao akiwa ni
  Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
  Moja ya kazi zake kuu ni kusimamia utendaji wa Serikali. Bunge linahakikisha kwamba
  nchi inaendeshwa vizuri, huduma zinatolewa kiusahihi kwa wananchi, na kwamba fedha
  za wananchi zinatumika vizuri na zinatolewa maelezo. Wabunge wanaweza kuiwajibisha
  Serikali kwa kufanya ushiriki wa aina tatu: wabunge wanaweza kuuliza maswali ya msingi,
  wanaweza kuuliza maswali ya nyongeza na wanaweza kutoa michango wakati wa mjadala.
  Muhtasari huu unapima utendaji wa wabunge kwa kuzingati a namna walivyoshiriki kati ka
  vikao vya Bunge. Kipindi kilichopiti wa ni vikao 17 vya Bunge kuanzia mwaka 2005 hadi
  2009 (kikao cha 18 kilichoanza tarehe 26 Januari 2010 hakijajumuishwa).​
  Je, wanafanya kazi kwa ajili yetu?
  Mambo nane kuhusu wabunge Tanzania​
  Muhtasari huu umeandaliwa na Uwazi InfoShop iliyopo Twaweza/Hivos Tanzania.
  Uwazi, S.L.P. 38342, Dar es Salaam, Tanzania.
  Simu +255 22 266 4301. Faksi +255 22 266 4308.
  Barua pepe: info@uwazi.org. Tovuti : Uwazi.org
  2​
  2. Mambo nane kuhusu Bunge la Tanzania​
  Wabunge wote wana nafasi sawa ya kuuliza maswali au kutoa mchango, lakini Mawaziri
  wa Serikali kwa kawaida hawafanyi hivyo. Maswali ni nyenzo kuu ya wabunge kuchunguza
  kwa makini shughuli za Serikali. Maswali ya msingi yanawekwa kwenye maandishi na
  kuwasilishwa Serikalini kabla ya kikao husika cha Bunge. Wakati wa kikao cha Bunge,
  serikali (hasa waziri husika) anatoa majibu ya maswali hayo. Maswali ya nyongeza ni
  maswali ya ziada yanayoulizwa na wabunge kufuatia majibu ya serikali ya swali la msingi.
  Maswali haya yanaulizwa wakati wa mjadala na yanajibiwa hapo hapo. Michango ni maoni
  yanayotolewa na wabunge Bungeni ambayo sio maswali rasmi. Michango hii inaweza kuwa
  ni maoni ya kawaida au hoja inayotolewa kipindi cha mjadala au maoni juu ya muswada
  uliopendekezwa kujadiliwa.
  Muhtasari huu unawasilisha mambo nane muhimu yaliyochambuliwa kutoka kwenye
  taarifa za Bunge zilizochukuliwa kwenye Mfumo wa Mtandao wa Taarifa za Bunge kwa
  Umma (POLIS) kwenye tovuti ya Bunge la Tanzania (Parliament of Tanzania) kama
  zilivyopatikana mwezi Januari 2010. Data kamili na mpangilio wa ngazi za ushiriki wa
  wabunge wote umewasilishwa kwenye Kiambatisho namba 1.​
  Ukweli wa 1: Bunge la Tanzania liko wazi​
  Bunge la Tanzania linafanya vizuri kuhakikisha taarifa zinapatikana kwa wananchi. Tovuti
  ya Bunge inapatikana na kutumiwa kiurahisi, ina taarifa za hivi karibuni na ina taarifa
  husika nyingi na muhimu. Katika nyanja nyingi inadhihirisha nia ya dhati na jitihada za
  Mheshimiwa Samuel Sitta, Spika wa Bunge, ambaye anaeleza kwenye tovuti ya Bunge
  kuwa:​
  “Bunge la Tanzania linahakikisha linaingiza taarifa za sasa na kurekebisha zilizomo
  kwenye POLIS ili kuhakikisha wadau wote na wananchi kwa ujumla wanapata
  taarifa za kutosha za shughuli za Bunge. Zaidi ya hilo, ni makusudio ya Bunge
  kurekebisha na kuufanya mfumo huu kuwa chanzo cha uhakika cha taarifa za
  Bunge.” (tafsiri yetu)​
  Taarifa zote katika muhtasari huu, zikiwemo taarifa za bajeti zilizonukuliwa kwenye
  utangulizi, zilichukuliwa kiurahisi tu kwenye tovuti ya Bunge.​
  3​
  Ukweli wa 2: CCM ni chama Kinachochangia zaidi Bungeni​
  Tangu uchaguzi wa mwaka 2005, idadi ya ushiriki wa wabunge kwenye mijadala ya vikao
  vya Bunge ni 19,039. Ndani ya idadi hiyo maswali ya msingi yalikuwa 3,922 na maswali ya
  nyongeza yalikuwa 5,882. Jumla ya michango ya wabunge ilikuwa 9,235.
  Katika idadi yote ya ushiriki wa wabunge Bungeni, michango ya ushiriki 15,410 ilitoka
  kwa wabunge wa CCM wakati michango ya ushiriki 2,150 ilitolewa na wabunge wa CUF
  na michango ya ushiriki 1,337 ilitolewa na wabunge wa CHADEMA. UDP chama chenye
  mbunge mmoja Bungeni kilitoa michango ya ushiriki 142. Mchango mkubwa wa CCM ni
  dhahiri kuwa unatokana na idadi kubwa ya wabunge iliyo nao. Wabunge 277 (au 87% ya
  wabunge wote) ni wa CCM, ukilinganisha na wabunge 31 (10%) wa CUF, wabunge 11 (3%)
  wa CHADEMA, na 1 (0.3%) wa UDP.​
  Ukweli wa 3: Wabunge wa upinzani wanashiriki zaidi kuliko wa chama tawala​
  Mchoro namba 2 unaonesha matokeo ya utendaji wa vyama tofauti vilipopimwa wastani
  wa ushiriki kwa kila mbunge. Kwa kuangalia uchangiaji wa maswali ya msingi, CHADEMA
  inashika nafasi ya kwanza ikiwa na wastani wa maswali ya msingi 19 kwa kila mbunge.
  CHADEMA pia inashika nafasi ya kwanza kwenye maswali ya nyongeza ikiwa na wastani
  wa maswali 36 ya nyongeza kwa kila mbunge. UDP (chenye mbunge 1) kinashika nafasi ya
  juu kabisa kwenye eneo la kutoa michango Bungeni. Chama tawala( CCM) kinashika nafasi
  ya mwisho katika kila aina ya ushiriki Bungeni kikiwa na wastani wa maswali ya msingi 12,
  maswali ya nyongeza 17 na wastani wa michango 26 kwa kila mbunge.​
  4​
  Ukweli wa 4: Wabunge waliochaguliwa wanachangia zaidi kuliko walioteuliwa​
  Katika nyanja zote, wabunge wa kuchaguliwa wamewazidi kiutendaji wabunge wa
  kuteuliwa, isipokuwa wabunge wa viti maalumu wana utendaji mzuri zaidi kwenye kutoa
  michango Bungeni. Wabunge kutoka Baraza la Wawakilishi Zanzibar na wale walioteuliwa
  na Rais wanaushiriki mdogo sana Bungeni.​
  5​
  Ukweli wa 5: Wabunge wanaume wanashiriki zaidi kuliko wabunge wanawake​
  Wabunge wanaume wanashiriki zaidi kuliko wabunge wanawake katika nyanja zote za
  ushiriki (mchoro 4). Hata ukichukua wabunge wanawake waliochaguliwa majimboni tu
  hali haibadiliki sana.​
  Wastani wa ushiriki wa wabunge, kwa jinsia​
  Ukweli wa 6: Wabunge 72 hawajawahi kuuliza swali la msingi hata moja​
  Njia kuu ya kuanzisha mjadala juu ya mada fulani ni kuwasilisha maswali ya msingi. Kama
  mchoro namba 5 unavyoonesha, wabunge 72 hawajawahi kuuliza swali moja la msingi.
  Wabunge hawa wengi ni wa CCM. UDP na CUF pia wana mbunge mmoja mmoja ambao
  hawajawahi kuuliza swali moja la msingi.​
  6​
  Ukweli wa 7: Slaa, Msindai na Lubeleje wanaongoza kushiriki Bungeni​
  Ili kubaini utendaji wa jumla wa wabunge, aina tatu za ushiriki wa wabunge Bungeni
  zilichanganywa na kukokotolewa ili kuweka alama za utendaji wa pekee. Mjumuisho huo
  ulifanyika kwa kujumlisha idadi ya awamu (ushiriki) ambao mbunge aliuliza swali la msingi
  au swali za nyongeza au alitoa mchango, ikimaanisha pia kwamba swali la msingi lina
  umuhimu sawa na swali la nyongeza na mchango uliotolewa wakati wa mjadala.
  Kama mbinu hii ikitumika, Dk. Wilbrod Slaa anapata nafasi ya juu kabisa ya utendaji
  Bungeni kuliko wabunge wote akiwa na jumla ya ushiriki wa 268: ameuliza maswali ya
  msingi 33, maswali ya nyongeza 106 na michango 129. Wa pili ni Mgana Msindai akifuatiwa
  na George Lubeleje (Jedwali 1).
  Ukweli wa 8: Mwinyi, Lowassa na Aziz wako mwisho katika ushiriki Bungeni​
  Wabunge watatu wa kuchaguliwa hawajawahi kuchangia mijadala ya vikao hata mara
  moja kwa mujibu wa POLIS. Hawa ni Dk. Hussein Mwinyi, Edward Lowassa na Rostam
  Aziz. Kuna mbunge mwingine, Frederick Werema ambaye pia hajawahi kuchangia lakini
  hajawekwa kwenye Jedwali namba 2 kwa sababu aliteuliwa hivi karibuni tarehe 27 Oktoba
  2009, kama Mbunge kutokana na cheo chake (Mwanasheria Mkuu wa Serikali).
  7​
  3. Hitimisho
  Muhtasari huu umetumia taarifa zinazopatikana kwa urahisi kwenye tovuti ya Bunge
  la Tanzania kupima kiwango cha ushiriki wa wabunge kwenye vikao rasmi vya Bunge.
  Umegundua tofauti kubwa ya viwango vya ushiriki miongoni mwa wabunge. Ikumbukwe
  kwamba hiki ni kiashiria kimoja tu cha utendaji wa wabunge; wajibu mwingine muhimu
  wa wabunge ni pamoja na kufanya kazi kwenye kamati za Bunge na kushirikiana na
  wananchi kwenye majimbo yao. Hata hivyo, muhtasari huu unatoa picha muhimu kwa
  umma kujadili namna wabunge wanavyowakilisha maslahi ya wananchi. Pia muhtasari
  unatoa fursa kwa kila chama cha siasa na kila mbunge kujitathmini zaidi namna ambayo
  wamekuwa wakihudumia maslahi ya wananchi kwenye majimbo yao. Uwazi kwa wote na
  midahalo ya huru ni muhimu katika kuimarisha demokrasia na uwajibikaji nchini.​
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Oct 10, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 419,797
  Trophy Points: 280
  Tatizo la uchambuzi wako ukiondoa eneo la viti maalumu hauna tija kwa siku za usoni kwa sababu baadhi ya wabunge uliowataja hawatarudi bungeni au watarudi bila ya wapigakura kuwa na takwimu ulizonazo.

  Mimi natofautiana nawe unapolipa Bunge maksi za juu kitija na kuipima tija hiyo kwa vigezo vya muda wa kuongea bungeni wakati hata ni jinsi gani huwa wanapiga kura huwa ni siri ukiondoa kikao cha bajeti ambacho ni mara moja kwa mwaka.

  Sasa mchango sahihi wa mbunge kitija ni jinsi anavyopiga kura wala siyo muda wa kuchangia kwa sababu kuchangia yawezekana hakuna tija na mwingine anaweza kuwa kimya lakini kura yake huielekeza kwenye maeneo yenye tija kwenye jamii.

  Nguvu zetu tuzielekeze katika kudai Bunge lililowazi katika upigaji kura na kauli zako hizi nilizozinukuu zathibitisha hujatafakari changamoto zilizopo mbele yetu:-


   
 3. Al-Watan

  Al-Watan JF-Expert Member

  #3
  Oct 10, 2010
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,632
  Likes Received: 13,423
  Trophy Points: 280
  Kuna mbunge mmoja mkongwe alishaulizwa kwa nini haulizi maswali bungeni ? Alijibu, kwake yeye maswali si muhimu kwa sababu maswali ni kama show na kuwajulisha wananchi tu, na kama ni kuwajulisha wananchi hata yeye anaweza, badala ya kuendeleza show ya maswali na hata kuleta picha ya msuguano na mawaziri, yeye anaendeleza zaidi lobbying za backroom bila publicity ya maswali na majibu, lakini jimboni mwake wananchi wanaona maendeleo.

  Sijui kama alikuwa anasema kweli au ni kujitetea tu, lakini kwa msingi wa maoni ya mbunge huyu, maswali yana maana kwa kuwapa wananchi habari tu, zaidi ya hapo mtu anaweza kufanya kazi na wizara husika moja kwa moja bila maswali mengi.

  Utafiti huu ni mzuri kwa kuanzia, lakini ingependeza kama ungehusisha vitu vingi zaidi ya maswali tu. Kwa mfano, wabunge walitoa ahadi gani na zipi zimetekelezwa, wabunge wanatumia muda kiasi gani majimboni mwao, bungeni na kwingineko, wabunge wanatoa ushirikiano kiasi gani kwa taasisi zisizo za kiserikali n.k
   
 4. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #4
  Oct 10, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Backdoor lobbying siyo mojawapo ya majukumu ya mbunge, na hiyo ni namna mojawapo ya rushwa; mbunge huyo hajui wajibu wake. Kazi ya mbunge ni kuhakikisha kuwa serikali inafanya majukumu yake sawasawa. Serikali hiyo ikifanya majukumu yake yote sawasawa kunakuwa hakuna haja ya kuwa na backdoor lobbying. Kwa vile mipango yote ya serikali inaidhinishwa na bunge, basi kuchangia kwenye mijadala ya bunge kuhusu mipango hiyo ya serikali na utekelezaji wake ndiyo jukumu kubwa la mbunge.
   
 5. Al-Watan

  Al-Watan JF-Expert Member

  #5
  Oct 10, 2010
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,632
  Likes Received: 13,423
  Trophy Points: 280
  Labda backdoor lobbying inatoa a more negative image, alichosema ni kwamba alikuwa anawabana mawaziri na kuuliza maswali ya maendeleo kama wenzake wanavyofanya bungeni, ila yeye hakupendelea theatrics za bungeni ambazo nyingine zilileta hata uhasama kati ya mawaziri na wabunge, yeye alipenda zaidi kuongea na viongozi na watendaji moja kwa moja na ingawa humsikii bungeni, mipango ya maendeleo ilikuwa inaenda jimboni, tena pengine kuliko hata hao wanaojibizana na mawaziri bungeni.

  Sitetei kutokuuliza maswali, najua kuuliza maswali bungeni ni muhimu sana hata kama ni kwa kutaka kuwajulisha wananchi tu serikali inafanya nini.

  Ninachosema ni kwamba utafiti unaoanzia na kuishia na idadi ya maswali yaliyoulizwa na nani kauliza maswali mengi unaweza kumuonyesha mbunge ambaye haulizi maswali bungeni lakini anafanya kazi moja kwa moja na serikali kama hawezi kazi, wakati mbunge anayeuliza miswali mingi bila kufanya kazi wala kufuatilia sembuse kuleta maendeleo kwa wananchi jimboni akaonekana anajua kazi.

  Tafiti ziangalie matokeo ya kazi za wabunge, sio show za nani anajua kuuliza maswali bungeni.
   
Loading...