Mambo muhimu ya kuzingatia katika uendeshaji wa kampuni

Swali langu lingine je kwa none residents kama partner wangu atumia index gani kumtambulisha kama mlipa kodi
 
Nataka kufungua kampuni ndogo ndogo ambazo zitakuwa na biashara tofauti tofauti na hizo kampuni nataka ziwe na kampuni moja (holding company) ambayo itazisimamia na kumiliki hisa humo. Je hii imekaaje? Ipi ndio inatakiwa ianze kufunguliwa kabla ya mwenzie? Na katika suala la tin na kodi inakuwaje?
 
Kwenye kufungua kampuni non resident atatumia passport, then issue za Brela zikisha sasa mtakuaja TRA ambako ndio wanatoka namba ya mlipa kodi. Kama huyo mgeni amepewa kibali cha ukazi naye anaweza kupewa TIN kama yeye. Ila kampuni itapewa TIN yake ambayo kwa sasa itakuwa sawa na namba ya usajili kutoka Brela.
 
Nataka kufungua kampuni ndogo ndogo ambazo zitakuwa na biashara tofauti tofauti na hizo kampuni nataka ziwe na kampuni moja (holding company) ambayo itazisimamia na kumiliki hisa humo. Je hii imekaaje? Ipi ndio inatakiwa ianze kufunguliwa kabla ya mwenzie? Na katika suala la tin na kodi inakuwaje?
Naomba ni kushauri kampuni moja inaweza kufanya na kusajili kazi mpaka 40. kwahiyo kama unataka kufanya kazi tofauti tofauti kwa majina tofauti unaweza kusajili Kampuni halafu ukawa na majina tofauti kutokana na biashara yako ambapo mmiliki ni Kampuni hiyo kubwa. Nazo zikiwa unaweza kuzifanya kuwa kampuni pia.

Kwenye maswala ya TIN kuna kitu kinaitwa Branch TIN unaweza kuwa na TIN ya kampuni ambapo unapewa TIN za matawi kutokana na biashara yako ilipo. TIN ni ile ile ya kampuni ila inaweza kuonyesha moja iko tawi lako la Kariakoo au tawi la tegeta, nyingie tawi la msimbazi, n.k...

Kumbuka swala la kodi la kampuni unajikadiria ila ni lazima kila mwaka upeleke hesabu zilizokaguliwa wa wakaguzi wa hesabu hiyo ni kwa ajili ya corporate. Kuwa na matawi kutavutia wewe kuwa nakulipa SDL asilimia 4% na WCF 1% ya Gross Salary.

Kitu cha kuwaza ni kuwa matakwa ya kisheria yapo mengi kwenye kampuni kwahiyo wakati unachukua maamuzi angalia garama za leseni mbalimbali na gharama za uzalishaji kama zinalipa. Ahsante
 
Kuna mabadiliko kidoog kwa mwaka huu hasa kuwa PAYE na SDL itakuwa inaenda online. Ila kitu kizuri kwenye SDL kuna mabadiliko kuwa mtu laziima awe na wafanyakazi 10 ingawa kiasi kimebakia kile cha asilimia 4. Kwenye umeme kutumika kulipia Kodi ya majengo (Property Tax) maswali na majibu kutoka sehem husik a nitaweka hapo chini
 
1629839931171.png
 
Habari!,
Kwanza nianze kwa kutoa shukurani zangu kwako pamoja na wadau wengine kwa maswali wanayouliza ambayo yamepelekea kupanua sana huu mjadala.
Mimi na maswali kadha wa kadha kuhusu biashara ya kukopesha yaani Microfinance Services Provider (Entity/Companies)
Kwa walaka wa BOT ili mtu afungue Kampuni ya namna hii mtaji ni kuanzia ni 20m na isipungue hapa kwa kipindi chote cha uendeshaji wa biashara hii.
Swali
1. mtu hawezi kuingia ubia na Kampuni ambayo tayari ina leseni ya biashara hii kwa kupata hisa na kufungua branch katika eneo tofauti ambapo itaonekana kuwa ni tawi la biashara mama hapa utaratibu wako utakuwaje.
2. Mtu anaweza kufungua Kampuni hii bila kuwa na mtaji wowote na baada ya kukamilisha documents zote zinazotakiwa akaanza kutafuta watu wenye mitaji ambao atawashawishi kuweka pesa zao ili kuanza kufanya biashara, kama ni ndiyo ikitokea ukatumia miaka minne kupata watu wa kuweka pesa zao upande wa gharama yaani TRA na BRELA itakuwaje hapo.
Nitangulize shukurani zangu kwako pamoja na wadau wote hapa jukwaani.
 
Karibu kwa maswali yako ambayo kwa ujunla unataka kuwa kwenye Microf finance uzuri umeshajua mambo yanayotakiwa katika kufungua hiyo ni ya msingi sana . Sasa majibu yako
1. Kuingia ubia au kuwa mbia maana yake kwa ufupi sana nawe unakuwa mwenye hisa ingawa kuna aina mbili kuu kampuni inaweza kukupa hisa yaani kwa kununu nakuwekeza fedha na pili kwa kutoa huduma ambapo inatumika form ya kugawanya hisa namba 55 (b). Sasa ukishakuwa mbia maamuzi ya kupanua na kuwa na tawi ni kutokana kwa mujibu wa sheria kuwa ili muwe umekuwa na mtaji kiasi gani muweze kufungua na vileve mpango biashara wenu unasemaje.
2. Unaweza kabisa kufungua kampuni na ukagawa share kidogo na nyingine ukaziacha ili wakipatikana wawekezaji unaweka nao utawagawia kwa kutumia form 55 a ila mwanzoni lazima uwe na watu wasiopungua wawili na kama hii ni private haitatakiwa kuwa na watu zaidi ya 20. Kwa sasa kwanza mfumo umeshaunganishwa kati ya TRA na Brela kwa hiyo ukisajili tu Brela number yako ya usajili ndio inakuwa TIN number yako. Hivyo unategemewa ndani ya miezi mitatu tu baada ya kusajili uwe umefika TRA umefanya makadirio ya mapato na kama ni , tunategemea utakuwa umesifuri nayo unaweka sifuri, ila tunategemea utakuwa umepanga ofisi au huyu mtu mpya ana ofisi kwahiyo tunategema kodi hodhi (withholding tax) ya pango ya asilimia 10 na Ushuru wa Stampu (Stamp Duty) ya 1% na baada ya mwaka kuisha kutengeneza mahesabu yaliyokaguliwa (Audited financial) hata kama ni sifuri hesabu kwa siku hizi zinawekwa kwa njia ya mtandao. Kwa ufupi huo ndio utaratibu. Ila hapo ngoja niweke angalizo kwamba taarifa hizi zimetolewa kwa lengo la elimu tu kwa kuwa mambo haya ni ya kitaalamu(Professional) basi Waataalamu husika ni vyema ukatufuta huduma zao ili wakusaidie hatua kwa hatua. KARIBU
 
Ahsante kwa majibu mazuri, kwa mfano sasa nimepata hisa kwa kutumia fomu namba 55 b,
Na mkaelewana na Kampuni husika kufungua tawi hapa utaratibu ukoje kwa maana ya BRELA na TRA
 
Hapo ni rahisi tu unaenda TRA unapat Branch TIN unakuwa na tawi
 
Kwa watu wa forex wakitaka kufungua kampuni inakuaje? Je wanalipa VAT? je kodi inakuaje ikiwa natumia my own capital?
Hii biashara ya forex kuna uwezekano mkubwa sana ya kusajiliwa kamba kampuni ya kawaida ila kwa kiasi kikubwa kwa nchi yetu hii kitu iko chini ya CMSA website yake www.cmsa.go.tz nilishawahi kuwaulizia kuhusu Forex Brokerage wako very much openned mind na wao wanataka kuona jinsi gani wanaweza kufanya kukuwa hasa na broker wa Tanzania ambao wao wanawacontrol ili kuweza kuwezesha uwekezaji hapa ndani. Tulikuwa na mazungumzo yenye tija na brokerage ambao wako tayari wamesajiliwa wanaweza kuongeza kwenye portifolio.Kwenye swala la VAT kuna kiwango cha chini kwa kampuni kusajiliwa kwenye level hiyo moja ni kwamba lazima uwe na mauzo ya zaidi ya 100m na kama unatoa service za kitaalamu basi hata kama ujafikia huko unaweza kusajiliwa. Kodi nyingine utalipa kutokana na faida ya biashara, kama unawafanyakazi zaidi ya 10 sasa utalipa Skills Development Levy (SDL), WCF na NSSF kipande kinachokuangukia kama mwajiri. PAYE wewe ni agent tu anayekatwa ni mfanyakazi ila wewe kama mwajiri unalazimika kupeleka sio garama kwako ni garama za mfanyakazi. Naamini nimeelezea na nimekupa mwanga. Angalizo maelezo haya ni kwa elimu na ufahamu wa jumla ukitaka
 
Ahsante sana, weledi wako kwenye haya mambo ni mkubwa sana.
Ofisi zenu zinapatikana wapi au mawasiliano mtu akihitaji msaada binafsi anawapataje.
Karibu na Ahsante ni madhumuni yetu kuwatumiakia watu wa Mungu kwa njia hii tuliopewa kutumikia katika fani hii kwahiyo sifa na utukufu ni za kwake. Na zimrudie yeye
 
Jambo la Muhimu sana kwa sasa kwa wale waliokuwa VAT registered hakikisha unapopata risiti imeandikwa T Jina , TIN Na VRN kama inavyosema section 86 ya VAt hapo chini nimeiweka kwa undani.
 
Habari mkuu?

1. Nnafanya biashara lets say ya kuendesha semana mbali mbali nje ya nchi (mostly online)! Sasa kwa mfano nimefanya semina nikalipwa dola 400 je natakiwa kulipia VAT kwa ya biashara kama hiyo?

2. Lets say baada miezi 12 nikawa na mapata ya 20mil kutokana na hiyo biashara je natakiwa lipa kodi ipi? VAT?

3. Kwa kampuni iliyo sajiliwa je kodi natakiwa lipa kila baada ya miezi mingapi?
 
Kufikia kuwa registered VAT lazima mauzo yako ghafi yawe 100m au azadi na uaweza kuwaregistered kama unatoa huduma za kitaalamu (Professional Services). Kama uko chini ya hapo unatakiwa kufanyiwa makadirio kama mtu binafsi na kulipa kodi kila robo ya mwaka hivyo hivyo kwa kampuni ila kampuni inauwezo wa kujifanyia makadirio yake yenyewe
 
Kutakuwa na mabadiliko katika kufile VAT ila katika mambo muhimu kwenye haya mabadiliko ni kuwa hakikisha risiti za manunuzi ziko kwenye mfumo mpya wa 2.1 protocol na pili kama utakuwa unadai kwenye VAT ya mwezi wa pili itabidi uombe refund ya hiyo hela haitawezekana kucarry forward hiyo amaount. Kwa uelewa zaidi angalia tangazo la tra hapo chini.
 
Attachments

  • Introduction of upgraded VAT electronic filing system.pdf
    477.4 KB · Views: 10
Back
Top Bottom