Mnawezaje kukua kibiashara kwa utaratibu huu wa TRA?

WANGAMBA

Member
Jul 21, 2022
64
94
Jamani kwa utaratibu wa TRA unafanya kazi zake mnawezaje kukua kibiashara mbona wafanya biashara wengi tukijaribu kufanya biashara tra ndo ya kwanza kuwarudisha nyuma.

Makadiria makubwa fine za mara kwa mara mtu hauko hata VAT unaambiwa ulete hesabu za 2020 na hii ni 2024 list wiki mbili tu azisomeki ndiyo uzipeleke wakague.

Naombeni ushauri mnatumia njia gani ili usisumbuliwe ma TRA na offis ikue please.
 
Ua biashara fungua biashara mpya, hata kwa jina la mtoto, waache hilo deni udeal nalo taratibu
 
Kitu kimoja uweke kichwani katika biashara hapa nchini;
Kama hufahamu kabisa masuala ya kodi na namna zinavyotakiwa kufanywa basi hakikisha unatafuta tax consultant ambaye atakua akisimamia masuala yako. Kama utaona ni gharama basi hakikisha unajisomea sana masuala ya kodi na unafika TRA mara kwa mara kuelimishwa zaidi kwa lile ambalo hujaelewa lakini pia usiache kuuliza hapa JF kwani kuna wajuzi wengi wanaweza kukusaidia ushauri na namna njema ya kufanya mambo yako
 
Kwanini yasifundishwe shuleni yawekwe kwenye syllabus
 
Kwanini yasifundishwe shuleni yawekwe kwenye syllabus
Mkuu, mbona yanafundishwa? Pale chuo cha kodi zinatolewa elimu kuanzia ngazi ya cheti zipo na mitaala ya kodi ipo. Nadhani ni mgawanyo wa taaluma kwamba kila taaluma ina utaratibu wake na sidhani kama ni busara eti mwanafunzi wa sekondari ama msingi afundishwe hizo taaluma zote za kodi, udaktari, uuguzi, sheria, uhandisi, nk nk. Ni mgawanyo tu katika jamii.
 
Mkuu, duniani kote, X Revenue Authorities,hazipishani. Ukitaka kujua,ulizia kesi za Donald Trump au wacheza soka Ulaya.

Binafsi nachoweza kukushauli, acha kufanya biashara kimazoea. Tatizo tu lipo hapo kwenye kukadiria. Hio ni njia moja wapo ya rushwa kwanza.
Kama unatumia EFD,ni rahisi.
Na kingine,kwa nini TRA haijifunzi kwa waliofanikisha mifumo hiyo ya biashara? Kuuza au kununua, ni mfumo. Mwisho wa mda furani,utakachodaiwa,ni kile kinachoonekana kwenye system. Mambo ya kukadiria,hayapo.
Jenga mfumo wako wa mauzo,hata wa Excel tu,au kama unajiweza,tengeneza software yako(POS).
Ikiwezekana,ajiri mtu kwa ajili hiyo. Mmenunua bidhaa,dai lisiti,ifike ofisini. Kabla haijaanza kufutika, inachapwa na kuwekwa kwenye mfumo wako. Kama mmeuza,toeni lisiti harari(hapa na wewe ni mtu mzima jiongeze), day by day.
Na hii ikiwa ngumu, kuna watu wanadeal na mambo hayo,na ukiwa mteja wake wa kudumu,gharama zake ndogo. Muandalie lisiti anazohitaji,yeye atashughulika anavyojua,mengine wanasimamia wao. Hakuna biashara yenye unafuu linapokuja swala la mapato mkuu.
 
Mkuu, duniani kote, X Revenue Authorities,hazipishani. Ukitaka kujua,ulizia kesi za Donald Trump au wacheza soka Ulaya.

Binafsi nachoweza kukushauli, acha kufanya biashara kimazoea. Tatizo tu lipo hapo kwenye kukadiria. Hio ni njia moja wapo ya rushwa kwanza.
Kama unatumia EFD,ni rahisi.
Na kingine,kwa nini TRA haijifunzi kwa waliofanikisha mifumo hiyo ya biashara? Kuuza au kununua, ni mfumo. Mwisho wa mda furani,utakachodaiwa,ni kile kinachoonekana kwenye system. Mambo ya kukadiria,hayapo.
Jenga mfumo wako wa mauzo,hata wa Excel tu,au kama unajiweza,tengeneza aoftwaye yako(POS).
Ikiwezekana,ajiri mtu kwa ajili hiyo. Mmenunua bidhaa,dai lisiti,ifike ofisini. Kabla haijaanza kufutika, inachapwa na kuwekwa kwenye mfumo wako. Kama mmeuza,toeni lisiti harari(hapa na wewe ni mtu mzima jiongeze), day by day.
Na hii ikiwa ngumu, kuna watu wanadeal na mambo hayo,na ukiwa mteja wake wa kudumu,gharama zake ndogo. Muandalie lisiti anazohitaji,yeye atashughulika anavyojua,mengine wanasimamia wao. Hakuna biashara yenye unafuu linapokuja swala la mapato mkuu.
Safiii
 
Tengeneza mazingira ya kibiashara yanakufanya uonekane ni mfanyabishara wa level w
ya chini hata kama una Mtaji wa bilioni moja kaa chini fikiri nimemanisha nin
 
Mamlaka ya mapato Tanzania ni chombo muhimu sana ktk kuijenga nchi kisiasa, kiuchumi, kijamii na kiutamaduni. TRA wana majukumu makubwa ya kukusanya mapato ili kufanikisha ulipaji wa gharama mbalimbali Za kuendesha Serikali (Matumizi,Miradi,Ulipaji madeni yanayokopwa nje na ndani).

Kimsingi sheria Za kodi za Tanzania ni photocopy ya sheria Za kodi toka ktk mataifa yaliondelea kiuchumi kama Uingereza hivyo ni sheria ngumu kwa kuzingatia utofauti wa mifumo ya kiuchumi,Elimu na uwezeshaji.

Miaka michache iliopita Wafanyabiashara,wajasiliamali na Wawekezaji walipitia kwenye ubatizo wa moto kutokana na approach Za ubabe, maguvu. Vilivyoenda sambamba na Uporaji mali,Rushwa na ukosefu wa uadirifu,Makadirio kandamizi.

Maafisa wengi wa TRA na wengine kupitia TASK FORCE walitajirika sana kupitia ukandamizaji,Unyongaji biashara,Uharamia wa kimamlaka..Ufungaji biashara,Ukwapuaji fedha kwenye akaunti za wafanyabiashara. Michakato hii ilipekekea wafanyabiashara wengi kufirisika,kufunga biashara,kujiua,Kukimbia nchi,Kuhamisha biashara na uwekezaji wao.

Mambo yamerudi yamerudi upya sasa..Maafisa kodi,Mameneja na waandamizi wamevaa koti na mavazi mapya ya Tax force. Wafanyabiashara wameanza kuishi kama digidigi, hofu, wasiwasi, huzuni na kukosa tumaini. Maafisa wamegeuka miungu watu. Mfanyabiashara anaamka anakuta EFD zimefungwa,akaunti zimezuiwa.

Kimsingi ktk makusanyo yanayofanyika,Wafanyakazi wasio waadirifu wana chukua robo na zaidi ya mapato kupitia Rushwa na mirungura. Ndio maana wengi wa watumishi ktk TRA wanaishi na kufanya uwekezaji mkubwa (Majumba, Magari, Apartments, Mitambo, Shares, Bonds, Extravagants life) kinyume na uhakisia wa vipato halali. Wengi wanafanya uwekezaji haramu na kutakatisha fedha kupitia ndugu,jamaa,marafiki kukwepa mikono ya dola na kujulikana.

Simu zinapigwa asubuhi,Mchana na jioni..akifika anapewa mkeka wa makadirio Vitisho, usumbufu, ubabe. Mwisho wa siku Rushwa, Mirungura, Vilio.

NINI KIFANYIKE
1: TRA lazima wapanue na kuongeza wigo wa walipa kodi (TRA must widen Tax base).Hili litasaidia sana kuepusha ku suffocate biashara chache zilizopo kwa kuzingatia idadi ya watu na mahitaji ya nchi sasa na baadae.

2: Wafanyakazi waongezwe, TRA is advised to recruit more staff to facilitate down top approach compliance sensitization. TRA inahitaji taaluma mtambuka kusaidia ktk kujenga mahusiano, kuelimisha, ni wakati wa kuwa na Relationship Officers, Relationship Managers, Transformations Officers, Business Advisors, Commercial Consultants. Wenye wigo wa kusaidia weredi ktk compliances badala ya kuwa wakusanya madeni kama Yono au Majembe, Adili..Court brokers..

Wafanyabiashara ni business partners/Affilliates wa nchi,TRA. Sio wezi, Majambazi, Maharamia. They deserve respect, honour, proffessional treatments. Consultative approached zitumike kudai kodi.

3: Review employee rotational strategy. Wafanyakazi wanakua aggressive kuomba na kupokea rushwa pindi wakihamishiwa kwenye vitengo vyenye fulsa dhidi ya vitengo/kanda/Mikoa mikavu.

4:SHERIA ZA KODI ZIFANYIWE MAREKEBISHO ILI KUENDANA NA UHALISIA WA BIASHARA NA MAZINGIRA YA NCHI. Mfano, VAT, PAYEE, SDL, Corporate Tax, Income Tax.

5: Corporate Tax ishushwe kufikia 20% ili kuwezesha ukuaji wa biashara,makampuni,uwekezaji.

6: Kuwe na Category rasmi za kibiashara ktk mifumo ya kodi na kodi zitofautiane. SME, Large Enterprises, Congromerates. Multinational Enterprises, Foreign State Owned Enterprises.

7: Kutokana na unyeti wa kazi ya ukusanyaji mapato na kulindima kwa vitendovya matumizi mabaya ya madaraka,Rushwa na Ufisadi kuundwe idara maaalumu ya ufuatiliaji wa maadili wa watumishi wa TRA nje ya mfumo wa TRA. Ama kuwe na vitengo ktk taasisi kama JWTZ, TAKUKURU ,DPP, etc.

8: Taratibu za kisheria (Mahakama) zifuatwe ktk utekelezaji wa maamuzi ya kufunga biashara,Kufunga Akaunti,Uchotaji fedha toka kwenye akaunti za wafanyabiashara kwa maguvu na ubabe.

9: Consultative Approach zitumike kuwajenga,Kuwasaidia na kuwainua wafanyabiashara ili kuwafanya kuwa more compliants (Voluntary)..Wakue ktk viwango vya ulipaji,waneemeke na kazi wafanyazo..Biashara sio mateso,jehanamu..

10:Misamaha ya kodi zisizolipika itolewe kusaidia kufufua biashara zinazokufa sababu ya malimbikizo makubwa ya kodi,penati na faini..Tuinue uchumi,Tukuze uchumi..

11:Tax incentives na Tax Holidays kwa SME..

12:Mikopo isio ya Lazima isikopwe na wanasiasa kuepuka mzigo mkubwa kwa walipa kodi wachache..Tukope kwenye miradi yenye tija endelevu..Sio miradi ya kisiasa..Makamishna wa kodi wawepo kwenye team za ukopaji kusaidia kutetea na kupigania uhalisia wa viwango na mizigo ya ulipaji..

13:Nguvu kubwa mnoo itumike kwenye kudhibiti upotevu wa mapato kupitia taasisi mbalimbali (CAG report).Hatua kali zichukuliwe kuwatia moyo wafanyakazi na wafanyabiashara wanao kosa usingizi kufanya biashara kwa jasho na damu ili kulipa kodi..
 
Back
Top Bottom