Mambo muhimu kuhusu yaliyomo sayari ya Mars

Makanyaga

Makanyaga

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2007
Messages
3,043
Likes
538
Points
280
Makanyaga

Makanyaga

JF-Expert Member
Joined Sep 28, 2007
3,043 538 280
Mambo muhimu kuhusu yaliyomo sayari ya Mars

Source: Mambo muhimu kuhusu sayari ya Mars
Sayari ya Mars imekuwa ikiwashangaza, kuwasisimua na kuwavutia binadamu kwa miaka mingi.

Maelfu ya miaka iliyopita, binadamu walikuwa wakishangaa na kujiuliza nini kinapatikana katika sayari hiyo inayopatikana umbali wa kilomita milioni 54.6 kutoka kwa dunia (maili milioni 34).

Sana, kutokana na muonekano wake wa rangi nyekundu sawa na ya chuma iliyoshika kutu, binadamu waliihusisha na moto au damu.

Jina Mars linatokana na mungu wa vita wa Warumi.

Kutokana na ufanisi wa kisayansi, binadamu kwa sasa amefanikiwa kufahamu mengi kuhusu sayari hii.

Sayari hii ina mandhari ya kushangaza: utayapata maeneo sawa na ya nyika duniani, maeneo ya jangwa kutokana na upepo mkali, mashimo makubwa yanayotokana na volkano, milima ya volkano na maeneo ya ukubwa sawa na taifa la Luxembourg yaliyojaa milima (machungu) ya mchanga.

Haya yote yamefunikwa na vumbi ya rangi moja.

Ni eneo ambalo huwa hakuna mvua kamwe. Hakuwezekani kuwa na mvua kwani maji, iwapo yangekuwepo, hufusha na kuwa mvuke mara moja.

Katika sayari ya Mars, wakati sawa na wa kutua kwa jua duniani, anga hujaa rangi ya buluu. Dunia huonekana tu kama nukta tu miongoni mwa nyota angani.

Ni mandhari ya kupendeza sana hasa kwa wanaopenda utalii - ikizingatiwa kwamba binadamu hajatalii sana sayari hiyo, kuna uhakika kwamba iwapo utafanikiwa kufika huko, kila utatapoenda utakuwa binadamu wa kwanza kufika huko.

Utakuwa kama Wazungu waliokuwa wanatalii Afrika karne ya 19, ambapo walikuwa Wazungu wa kwanza kutazama milima, mito, nyika na misitu ya kupendeza barani. Lakini kumbuka kwamba hakuna oksijeni.

Utafikaje huko
Kwa karne nyingi, imekuwa ndoto tu lakini inakaribia kutimia. Iwapo mambo yote yatakwenda sawa, mjasiriamali mmiliki wa Space X Elon Musk anapanga kutuma kundi la kwanza la watalii kwenye sayari hiyo kufikia 2022.

Lakini gharama yake itakushangaza pengine. Tiketi ni $10bn! Lakini iwapo huwezi kupata pesa nyingi kiasi hiki, usife moyo. Kuna njia nyingine ya kiteknolojia ambayo taasisi ya safari za anga za juu ya Marekani Nasa inatafakari - kutumia miwani ya kisasa na roboti. Roboti ndiyo itakuwa Mars, wewe uwe papa hapa duniani lakini itakuwa ikikupeperushia picha za uhalisia kutoka sayari hiyo.

Vivutio sayari ya Mars
Kivuti kikuu ni mlima wa Olympus Mons. Mlima huu una urefu wa maili 14 (kilomita 22), na ndio mlima wa volcano mrefu zaidi katika Mfumo wa Jua. Kwa kulinganisha tu, urefu wa mlima huu ni mara tatu urefu wa mlima mrefu zaidi duniani, Mlima Everest.

Sawa na ilivyo kwa milima mirefu ya volkano duniani, mlima huu kilele chake kimefunikwa na mawingu - lakini si ya maji, bali ni ya vumbi.

Haijabainika iwapo mlima huu bado hulipuka, lakini inakadiriwa kwamba wakati mmoja ulilipuka na kurusha matope na mawe makubwa ya moto angani.

Ukisafiri kusini magharibi kutoka kwa mlima huu, utapata Valles Marineris.

Hili ni bonde kubwa kwenye ikweta ya sayari ya Mars. Bonde hili linakadiriwa kuwa na umbali wa kilomita 4,000 ambao ni karibu na upana wa taifa la Marekani kutoka mashariki hadi magharibi.

Katika baadhi ya maeneo, bonde hili lina kina cha karibu kilomita saba (futi 23,000) - karibu mara nne kina cha bonde maarufu la Marekani ambalo kwa Kiingereza hufahamika kama Grand Canyon.

Kufikia sasa, haijabainika bonde kubwa kiasi hiki liliundwa.

Bonde hili la Valles Marineris lina mchanga wenye marangi mbalimbali ya kupendeza ambao umejipanga kwa safu mbalimbali. Inadhaniwa kwamba huenda mchanga huu ulitokana na mashapo au machenga ambayo yalijikusanya chini ya ziwa au mto wa barafu, au kutokana na kujikusanya kwa majivu ya volcano.

Kinyume na bonde la Grand Canyon Marekani, ambalo liliundwa na mmomonyoko uliochota mchanga na kuyachonga mawe, kuna uwezekano kwamba bonde hili la Mars lilitokana na kutengana kwa maeneo mawili makubwa ya 'ardhi' ya Mars. Kila upande wa bonde hilo unaweza kuingia kwa ule mwingine, kana kwamba mtu anajaza mchezo wa fumbo.

Rangi ya anga

Ukafanikiwa kujipata kwenye bonde hili, na uwe unataka kuangalia kutua kwa jua, utashangaa kugundua kwamba anga lake halitakuwa ya rangi nyekundu - bali ya samawati. Hii inatokana na wepesi wa anga la sayari ya Mars, ambalo ni asilimia moja tu ya uzito wa anga la Dunia.

Anga la Dunia huwa rangi ya samawati mchana kutokana na miali ya jua kutawanywa na molekuli za hewa. Hili huwa halitendeki sana sayari ya Mars, hivyo mchana anga huwa la rangi ya manjano iliyokaribia hudhurungi. Lakini jua linapotua, ambapo miali yake huwa haina nguvu sana ndipo anga la Mars hugeuka na kuwa rangi ya buluu.

Sayari ya Mars pia ina jambo jingine la kushangaza. Katika maeneo mengi, chini ya vumbi lake jekundu, kuna mawe ya rangi ya samawati na kijani kutokana na madini kama vile chuma. Vumbi hilo linapobebwa na upepo au kutokana na kupita kwa sayari ndogo, huwa kunafichuliwa mandhari ya kupendeza ya mikolezo tofauti ya rangi ya samawati.

Hali ya hewa
Kiwango cha joto cha kadiri katika sayari ya Mars ni nyuzi joto takriban -56C (-69F). Hii ni sawa na hali ya baridi maeneo ya ndani kabisa ya Antarctica, anasema mtaalamu wa biolojia na anga za juu katika Chuo Kikuu cha Washington, David Catling.

Ndipo uweze kufurahia, itakubidi kukaa karibu na ikweta ya Mars, ambapo huko kiwango cha joto kinaweza kufikia takriban 35C (95F), na hakuna upepo sana. Kutokana na wepesi wa anga lake, upepo mkali huko utahisi kana kwamba ni upepo tu Ingawa huwa kuna unyevu na ukungu usiku katika sayari hiyo, mchana hali ni kavu sana.

Kutokana na hali kwamba sayari hiyo inapatikana karibu mara moja unusu mbali na jua ukilinganisha na Dunia, hakuna haja ya kuvalia miwani ya kukinga dhidi ya mwanga wa jua.

Huko, kuwasha moto pia ni ngoma kwani hakuna mimea na anga lake asilimia 96 ni kaboni daoksaidi - kemikali inayotumiwa kwenye mitambo mingi ya kuzima moto.

Tofauti na Dunia, ambapo mawingu na anga hufanya kazi kama blanketi na kuzuia joto kuondoka usiku, sayari ya Mars hakuna mawingu na anga lake ni jepesi sana. Matokeo yake ni kwamba, sawa na inavyofanyika jangwani, usiku huwa kuna baridi kali sana. Baridi hii inaweza kufikia nyuzi -73C (-99F) usiku karibu na ikweta kwenye sayari hiyo.

Kuna viumbe walio hai?
Viumbe wote walio hai duniani huwa wana maji ndani yake. Hivyo, wataalam wamekuwa wakiamini kwamba iwapo kuna viumbe Mars, lazima wawe kwenye maeneo yaliyo na maji.

Kwa miongo mingi, wanasayansi walitafuta ishara za kuwepo maji Mars bila mafanikio.

Lakini mwaka 2011, walifanya ugunduzi huo. Waligundua michirizi ya maji yaliyokuwa yakitiririka kutoka kwa milima na mabonde ya Mars. Inadhaniwa kwamba huenda mito, yenye maji yenye chumvi labda huchipuza kutoka chini ya 'ardhi' kwenye hazina kubwa ya maji.

Binadamu hubadilika?
Kutokana na kiwango cha chini ya nguvu mvuto, uzani wa vitu huwa tofauti sayari ya Mars. Binadamu wa kilo 100 hivi, uzani wake Mars unaweza kuwa karibu na kilo 38 hivi.

Ukafanikiwa kutua kwenye Mars, utakuwa ukiitazama Dunia na kuiona kama tone au kituo angani. Dunia utaiona ikiwa sawa na tunavyoiona sayari ya Zuhura mapema asubuhi, au jioni angani, anasema Catling.
 
dudus

dudus

JF-Expert Member
Joined
Feb 28, 2011
Messages
9,294
Likes
9,211
Points
280
dudus

dudus

JF-Expert Member
Joined Feb 28, 2011
9,294 9,211 280
Naanza kuamini lile simulizi la jamaa uliwahi kuletwa uzi humu. Aliona Jua likizama kwenye chenchem ya matope. Itakuwa Sayari hii aliliona likizama.
 
N

Nyanjomigire

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2013
Messages
2,670
Likes
2,136
Points
280
Age
55
N

Nyanjomigire

JF-Expert Member
Joined Jan 28, 2013
2,670 2,136 280
Mara kuna Carbon, mara kuna maji which means kama kuna maji lazima kuna Oxygen na kama hakuna Oxygen hao wa kwenda huko wataishije bila Oxygen????

Halafu umbali wote huo, over 50 million km, hicho chombo kusafiri hadi kufika huko ni lini na watu watakaokuwa wakisafiri kwenye hicho chombo wata-survive namna gani kwa muda wote wa safari???

Huu utafiti bado haujawa, nashauri uendelee labda kuna sayari zingine haukuwa mpango wa Mungu kuweka viumbe waishimo. You can't initiate contest with God.
 
Ngushi

Ngushi

JF-Expert Member
Joined
Jul 8, 2016
Messages
8,088
Likes
15,471
Points
280
Ngushi

Ngushi

JF-Expert Member
Joined Jul 8, 2016
8,088 15,471 280
Hivi wakuu huwa najiuliza Mara nyingi sana huyu Elon musk kutumia hela nyingi kiasi hicho kufanya tafiti kwenye hizo anga za mbali yeye anafaidika nini?
 
Mkaruka

Mkaruka

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2013
Messages
10,576
Likes
8,759
Points
280
Mkaruka

Mkaruka

JF-Expert Member
Joined Feb 5, 2013
10,576 8,759 280
Hivi wakuu huwa najiuliza Mara nyingi sana huyu Elon musk kutumia hela nyingi kiasi hicho kufanya tafiti kwenye hizo anga za mbali yeye anafaidika nini?
Ukisikia Risk Takers ndio hao sasa.

Imagine mwanzoni baada ya kugundua PayPal akawauzie eBay na kuwa billionnaire.

Halafu hela zote nusu akawekeza kwa kununua hisa Tesla nyingine akaanzisha SpaceX na SolarCity halafu akaanza kuishi kwa kukopa mpaka kodi ya nyumba.

Yaani ndio maana anavuta bangi ya marekani huyu mtu.
 
sengobad

sengobad

JF-Expert Member
Joined
Aug 13, 2017
Messages
1,217
Likes
706
Points
280
sengobad

sengobad

JF-Expert Member
Joined Aug 13, 2017
1,217 706 280
Hivi wakuu huwa najiuliza Mara nyingi sana huyu Elon musk kutumia hela nyingi kiasi hicho kufanya tafiti kwenye hizo anga za mbali yeye anafaidika nini?
We unadhani Bill gate kuwasaidia wakulima wa Tanga anafaidika na nini?
 
kwa-muda

kwa-muda

JF-Expert Member
Joined
Sep 5, 2018
Messages
1,162
Likes
1,982
Points
280
kwa-muda

kwa-muda

JF-Expert Member
Joined Sep 5, 2018
1,162 1,982 280
Hivi wakuu huwa najiuliza Mara nyingi sana huyu Elon musk kutumia hela nyingi kiasi hicho kufanya tafiti kwenye hizo anga za mbali yeye anafaidika nini?
Ana wawekezaji wenzetu tofauti na sisi uwa wanawekeza wakiona kitu kitazalisha mbeleni. Halafu kumbuka ana mkataba na jeshi la Marekani kuwa kampuni ya space X ndiyo inapeleka vyombo kama satelite zao na kuziweka angani.
Huo utafiti anaofanya akianza peleka watalii atarudisha gharama zake
 
UNIVERSE

UNIVERSE

JF-Expert Member
Joined
Mar 2, 2015
Messages
444
Likes
281
Points
80
UNIVERSE

UNIVERSE

JF-Expert Member
Joined Mar 2, 2015
444 281 80
Hivi wakuu huwa najiuliza Mara nyingi sana huyu Elon musk kutumia hela nyingi kiasi hicho kufanya tafiti kwenye hizo anga za mbali yeye anafaidika nini?
Nafikiri anafanya tu kwa passion hasa kutokana na kuwa ni kitu alichovutiwa nacho toka utotoni. Hivyo kwa sasa anatumia pesa tu bila kutarajia chochote. Ila kwa sasa wanamkataba na NASA wa ku-supply vifaa kwenye international space station pia wamerusha satellites kadhaa angani kama payloads kwa kutumia rocket yao ya falcon 9.

Hizo safari zote wahusika wanatoa pesa kwa spaceX. Mkataba wake na NASA unathamani ya zaidi ya $1bn usd. Hivyo kuna matumaini ya kuingiza pesa nyingi siku zinazogoma.
 
kwa-muda

kwa-muda

JF-Expert Member
Joined
Sep 5, 2018
Messages
1,162
Likes
1,982
Points
280
kwa-muda

kwa-muda

JF-Expert Member
Joined Sep 5, 2018
1,162 1,982 280
Nafikiri anafanya tu kwa passion hasa kutokana na kuwa ni kitu alichovutiwa nacho toka utotoni. Hivyo kwa sasa anatumia pesa tu bila kutarajia chochote. Ila kwa sasa wanamkataba na NASA wa ku-supply vifaa kwenye international space station pia wamerusha satellites kadhaa angani kama payloads kwa kutumia rocket yao ya falcon 9.

Hizo safari zote wanatoa wahusika wanatoa pesa kwa spaceX. Mkataba wake na NASA unathamani ya zaidi ya $1bn usd. Hivyo kuna matumaini ya kuingiza pesa nyingi siku zinazogoma.
Hawezi kuwa anafanya tu kwa kutumia ela wakati kuna investors ambao wamewekeza pesa yao, wazungu hawatazami faida ya hapa wanatazama faida kwa miaka ijayo
 
UNIVERSE

UNIVERSE

JF-Expert Member
Joined
Mar 2, 2015
Messages
444
Likes
281
Points
80
UNIVERSE

UNIVERSE

JF-Expert Member
Joined Mar 2, 2015
444 281 80
Hawezi kuwa anafanya tu kwa kutumia ela wakati kuna investors ambao wamewekeza pesa yao, wazungu hawatazami faida ya hapa wanatazama faida kwa miaka ijayo
Sawasawa hicho ndicho nilichomaanisha na ndio maana wameanza taratibu kufanya safari za kuingiza pesa. Mwaka uliopita wamefanya safari 19, zote zikiwa za kibiashara. Siku chache zilizopita wametangaza kukamilika kwa prototype ya BFR au starship kama wanavyoita kwa sasa. BFR inatarajiwa kuwa roketi kubwa na ya kisasa zaidi na hio ndio itakwenda Mars. Mwishoni mwaka mwaka huu safari ya kwanza ya majaribio ya starship itafanyika. Hivyo wanatarajia kuongeza mapato maradufu na wameanza hivyo toka mwaka jana. Lakini Ikumbukwe kuwa kampuni ina zaidi ya miaka kumi na safari nyingi za mwanzo za majaribio zilifeli na ilipoteza mamilioni hadi Elon Musk kukaribia kukata tamaa.
 
kwa-muda

kwa-muda

JF-Expert Member
Joined
Sep 5, 2018
Messages
1,162
Likes
1,982
Points
280
kwa-muda

kwa-muda

JF-Expert Member
Joined Sep 5, 2018
1,162 1,982 280
Sawasawa hicho ndicho nilichomaanisha na ndio maana wameanza taratibu kufanya safari za kuingiza pesa. Mwaka uliopita wamefanya safari 19, zote zikiwa za kibiashara. Siku chache zilizopita wametangaza kukamilika kwa prototype ya BFR au starship kama wanavyoita kwa sasa. BFR inatarajiwa kuwa roketi kubwa na ya kisasa zaidi na hio ndio itakwenda Mars. Mwishoni mwaka mwaka huu safari ya kwanza ya majaribio ya starship itafanyika. Hivyo wanatarajia kuongeza mapato maradufu na wameanza hivyo toka mwaka jana. Lakini Ikumbukwe kuwa kampuni ina zaidi ya miaka kumi na safari nyingi za mwanzo za majaribio zilifeli na ilipoteza mamilioni hadi Elon Musk kukaribia kukata tamaa.
Mwaka jana hisa za kampuni zake ndo zilishuka kidogo lakini kwa miaka yote investors wanamuamini sana. Na kampuni nyingine ile inayo develope hyperloop
 
UNIVERSE

UNIVERSE

JF-Expert Member
Joined
Mar 2, 2015
Messages
444
Likes
281
Points
80
UNIVERSE

UNIVERSE

JF-Expert Member
Joined Mar 2, 2015
444 281 80
Mwaka jana hisa za kampuni zake ndo zilishuka kidogo lakini kwa miaka yote investors wanamuamini sana. Na kampuni nyingine ile inayo develope hyperloop
Hivi mkuu SpaceX iko katika soko lao la hisa? Naona kama bado hivi. Kwa upande wa Tesla hii iko kwenye soko la hisa na mwaka jana hisa zilishuka baada ya Musk ku-tweet kwamba anachanzo cha kuaminika cha pesa za kuweza kuiondoa Tesla kwenye soko la hisa kitu ambacho mamlaka ya kusimamia masoko ya hisa ya marekani ilipinga ila hatimaye waliyamaliza na musk kuvuliwa nafasi ya uwenyekiti, amebaki kama CEO wa Tesla tu.
 
kwa-muda

kwa-muda

JF-Expert Member
Joined
Sep 5, 2018
Messages
1,162
Likes
1,982
Points
280
kwa-muda

kwa-muda

JF-Expert Member
Joined Sep 5, 2018
1,162 1,982 280
Hivi mkuu SpaceX iko katika soko lao la hisa? Naona kama bado hivi. Kwa upande wa Tesla hii iko kwenye soko la hisa na mwaka jana hisa zilishuka baada ya Musk ku-tweet kwamba anachanzo cha kuaminika cha pesa za kuweza kuiondoa Tesla kwenye soko la hisa kitu ambacho mamlaka ya kusimamia masoko ya hisa ya marekani ilipinga ila hatimaye waliyamaliza na musk kuvuliwa nafasi ya uwenyekiti, amebaki kama CEO wa Tesla tu.
Jamaa anakula cha Arusha ndo tatizo sometimes anakuwa hai sana had anaropoka.
Ila jamaa ana roho ngumu mfano project yake ya solar ambazo zinakuja na warranty ya maisha
 
Forum statistics

Threads 1,250,894
Members 481,523
Posts 29,749,882