Mambo muhimu kuhusu google adsense | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mambo muhimu kuhusu google adsense

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Yona F. Maro, Feb 27, 2011.

 1. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #1
  Feb 27, 2011
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  GOOGLE ADSENSE NI NINI ?


  Ni mfumo wa Matangazo kwa njia ya mtandao unaihusisha matangazo kwenye kurasa za tovuti , programu , blogu , majukwaa na huduma zingine za mawasiliano haswa kwenye mtandao .


  Google Adsense ina aina 2 za matangazo kuna yale ya maandishi pekee yaani Text na yanayotembelea kama picha na video yote ni mazuri na yote yana gharama zake .


  GOOGLE ADSENSE NA MAISHA YAKO
  Kwa kutumia Google Adsense unaweza kupata karibu laki 9 na zaidi kila mwezi na ukasahau kufanya shuguli zingine , Adsense inaweza kufunga Akaunti yako muda wowote au blogu yako muda wowote ule usipozingatia Masharti yao , kwahiyo usitegemee sana ,


  GOOGLE ADSENSE INAFANYAJE KAZI
  Kama unatovuti yako ukiweka matangazo ya mfumo wa adsense utalipwa kutokana na wingi wa watu wanaitembelea tovuti hiyo na jinsi watu watakavyo gonga click matangazo hayo.


  Mfano mrahisi ni Bwana JUMA ana kampuni yake inaitwa MAISHA , badala ya kutengeneza matangazo makubwa kwenye magazeti pamoja na kufungua tovuti ataenda kuongea na google au wawakilishi wa google atatoa tangazo lake atasema jinsi anavyotaka liangaliwe kwa mfano idadi ya nchi au maeneo ndani ya nchi husika , Matangazo ya MAISHA yanaweza kuonekana kwenye blogu ya YONA inayoitwa Naombakazi.com na tovuti nyingi za watu mbalimbali zilizokuwa na huduma za Adsense .


  Kwahiyo juma atafaidika kwa tovuti yake kutembelewa na watu wengi kutokana na kutangaza kupitia adsense na watu wanaotembelea NAOMBAKAZI kuona kiunganishi cha tovuti yake.


  NOTE > Kufuatilia masharti na maelezo mengine ni muhimu sana kwa mfano unatakiwa usiwaambie watu wagonge matangazo yako waache wa gonge click wenyewe ukifanya hivyo unaweza kufungiwa .


  SWALI MUHIMU
  Je ukubwa wa Tovuti au Blogu au umaarufu ndio kuongeza kipato cha Adsense ?


  Jibu ni hapana utaweza kupata mapato zaidi kutokana na jinsi ulivyoweka matangazo yako na jinsi watu wanavyogonga matangazo hayo hapo ulipoweka kwenye kurasa za tovuti au blogu yako


  USAJILI WA GOOGLE ADSENSE UKOJE
  Wale wanaotumia huduma za Gmail ambayo ni mali ya Google ni rahisi kujisajili ili kutumia mfumo wa Adsense kwenye blogu na tovuti zao unaweza kutembelea www.google.com/adsense


  NOTE>Kila mtu anahaki ya kuwa na Akaunti yake ya Adsense na kufuatilia malipo yake mwenyewe na kulipwa yeye.


  KUKUBALIWA NA PIN NUMBER
  Usajili wa Goolge Adsense hauwezi kukamilika kama huna PIN NUMBER na kujaza vitu vingine vya kuthibisha jinsi unavyolipa kodi , kama uko nchi za ulaya kuna namba unatakiwa kuandika ndio utapewa PIN NUMBER .


  Kama uki nje ya ulaya kama Tanzania , unaweza kutumiwa PIN NUMBER kutumia DHL ambapo utaingiza namba hiyo kukamilisha mfumo wa usajili au unaweza kuwatumia google kitambulisho au aina nyingine ya utambulisho kuthibitisha uwepo wapo kama kadi ya benki au passport.


  NOTE> Bila pin Number hutoweza kutambulika kwenye mfumo wa google adsense na malipo yako hutopatiwa .


  MALIPO YA GOOGLE ADSENSE
  Google huwa inalipa wenye Adsense kwenye tovuti zao kila mwisho wa mwezi kwa mfumo wa cheki , benki au western Union kutegemea na nchi ambayo mtu yupo , malipo hulipwa pale kunapokuwa na kiasi cha pesa kuanzia dola 100 kwa mwezi ambapo dola 17 hutumika kama gharama za kusafirisha cheki kama uko nchi ambayo wanatuma cheki .


  Kwahiyo unavyofanya kazi hii ya matangazo hakikisha unapata hela nyingi zaidi ili uweze kulipa gharama za benki na usafirishaji wa cheki yako , angalau uweze kuwa na dola za kimarekani 700 kila mwezi .


  NOTE > Malipo ya kila mwezi hulipwa mwezi unaofuatia kama yalifikia zaidi ya dola 100 za kimarekani  MALIPO YANAVYOTUMWA
  Kwa nchi ya Tanzania malipo ya Google Adsene huja kwa njia ya DHL ambapo hufika kila tarehe 2 kila mwezi , malipo yakifika kwenye ofisi za DHL wateja hupigiwa simu na kupelekewa au kama unaweza kufuatilia mwenyewe kutumia tracking number ya DHL kujua kama mzigo umefika au la .


  Jambo la kujua ni kwamba watu wengi hufikiri cheki zinatumwa kwa njia za posta za kawaida hapana ni DHL .


  UTARATIBU WA KIBENKI
  Unatakiwa uwe na Akaunti kwenye benki yoyote Tanzania kwa sababu cheki za google huandikwa jina la mtu au kampuni kwahiyo lazima uwe na Akaunti kama uko Tanzania .


  Ukishaweka cheki kwenye Akaunti yako huchukuwa siku 21 za kazi ili kuweza kulipwa malipo kwenye Akaunti yako na gharama zingine za kibenki .
  Kutokana na gharama nyingine za kibenki ina maanisha ukiwa na shilingi laki 5 kwa mwezi ujiandae kutoa alfu 70 kama gharama za kushugulikia Cheki yako kwenye benki yako.


  NOTE > Watu wengi hukata tamaa mapema na huishia njiani kwahiyo wanapoteza hela zao nyingi na watu wanatangaza kwenye tovuti au blogu hizo bure .


  Kumbuka unavyofungua blogu ukaweka adsense matangazo yataendelea kuwa hapo na watu wataona wanavyotafuta vitu mbalimbali kwenye mtandao kwahiyo usikate tamaa mapema .


  ZINGATIA NA UWE MAKINI NA MATAPELI
  Hapo juu nimesema kila mtu ana haki ya kuwa na Akaunti yake ya Adsense na kulipwa kwa jina lake hela yake mwenyewe , kuna watu wa nchi za nje haswa Uganda wanapenda kuwalaghai watu wa Kenya na Tanzania kwamba washirikiane kuendesha Mfumo wa Adsense kwenye tovuti zao na kugawana Hela nusu kila mwisho wa mwezi .


  Usikubali kuingia kwenye mtego huu , unatakiwa uwe na Akaunti yako unayoweza kuitolea maelezo na inayolipwa kwa jina lako kwenye nchi yako unaporuhusu hivyo faida haiendi nchini mwako inaenda Uganda kwa jina la Raia wa Uganda ambaye atatumia jina bandia ili asimwone akisha kutapeli hela zako .
  Hata kama unapata hela kidogo mfano dola 1 kwa siku usikate tama utaweza kuongeza vitu kwenye tovuti yako haswa kwa lugha ya kiingereza na kifaransa na kuweza kupata hata dola 50 kwa siku moja jinsi unavyoendelea kukuwa .


  CHANGAMOTO ZA MFUMO HUU
  Baadhi ya maeneo Adsense haifanyi kazi kutokana na aina ya matangazo yaliyofungiwa kutokana na mila na desturi za maeneo hayo .


  Mfumo wa Adsense uko zaidi kwa lugha ya kiingereza na nyingine za kimataifa bado haijasambaa sana kwenye lugha zingine ndogo ndogo kama Kiswahili ingawa mtu anaweza kutangaza pia  Benki nyingi haswa za afrika hazitambui mfumo wa google adsense kwahiyo baadhi ya watu wanapata tabu pale wanapoenda kuingiza cheki zao kwenye Akaunti na kudhani ni utapeli badala yake nyingi hutumwa kupitia CITIBANK ambayo huduma zake ziko juu sana .


  Nchi nyingi hazina mfumo wa kulipa kodi kwa njia ya mtandao kwahiyo unakuta wanachama wote wa google adsense wanalipa kodi kwenye nchi ya marekani kwa kwa kila malipo ya adsense nchi nyingi zinapoteza malipo hayo kutokana na mifumo yao .


  Kwa sasa nchi ya Kenya na Uganda wamefanya mazungumzo na google kwahiyo ukiwa nchi hizo malipo yako unapata baada ya siku 3 kila mwezi kwa njia ya western union au kuingiziwa fedha kwenye Akaunti yako moja kwa moja .


  Kama unaswali lolote kuhusu Google Adsense ntaweza kukusaidia .

  YONA F MARO
  University of Strathmore - Nairobi Kenya
   
 2. Cestus

  Cestus JF-Expert Member

  #2
  Feb 27, 2011
  Joined: Jan 23, 2011
  Messages: 1,000
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  umetumwa au?hku c sehem ya madalali!
   
 3. SamJet

  SamJet Senior Member

  #3
  Feb 28, 2011
  Joined: Jul 22, 2009
  Messages: 165
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  This information is helpful.
  I use Google adsense since i was sixteen( now 19-) and now nalipwa kama...........
  Najua mbongo kuamini ni ngumu.
  Pia malipo so kwa DHL tu unaweza kulipwa ukiwa na credit card (sio debit card) directly to yo account.
   
 4. Zing

  Zing JF-Expert Member

  #4
  Feb 28, 2011
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 1,780
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  mhhh since 16 yaani hata ingekuwa umesomea europe bado hata kisheria tu nadhani 16 ni ille gal ? tujuekama si usanii wako tu na where are you.?
  in east africa by 16 mtu ndo anamaliza Advanced secondary education. Sasa by that time tayari ulikuwa unajua adssense . mhhhh au wewe ndo yule muhindi wa bangalore???? umesoma story ya mtu kwenye net unajifanya ni wewe.

  Ebu tupe web adress yako tuone hiyo site. Ukitaka kuwa muongo inabidi uwe na akili sana ili uongo wako ukubalikehata kwenye akili.

  Wewe ni msanii or an artist. teh teh teh.


  Yaani hata hujui kudanganya alafu unasema unajua wabongo hawawezi kuamini. Probability ya ulichonadika kuwa kweli ni 0.000000001
   
 5. SamJet

  SamJet Senior Member

  #5
  Feb 28, 2011
  Joined: Jul 22, 2009
  Messages: 165
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  ha, wabongo kamini tabu,
  tzpage.com
  searchsafari.com
  sirikali.com blog, search engine under construction(sam.co.tz).
  Ngoja nikuambie, while i was 18 mwakajana baba alipokea barua yangu toka google ya 'membership pin na info about changing dolar ac to euro ac' Hakuamini nlipo muambia nlikua natumia adres yake na TIN ya his company(japo google dont use tin fo tz)
   
 6. SamJet

  SamJet Senior Member

  #6
  Feb 28, 2011
  Joined: Jul 22, 2009
  Messages: 165
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  kama unataka nikuoneshe jgg. Nipe email yako. File la adsense a\c yangu sema tu. I am in Arusha. A student form six pcb
   
 7. Zing

  Zing JF-Expert Member

  #7
  Mar 3, 2011
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 1,780
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0

  Acha usanii bwana
  Au nyie ndo wale mnarudisha reverse umri ili mfaidike na mambo fulani fulani kumbe ni wakubwa tu.

  Mambo unayosma kwa mazigira ya mtoto wa miaka 16 ulaya uwezekano wake wa kutokea pia ni mdogo mdogo sasa ndo iwe kwa tanzania.

  Wadangaye wengien mie nimechomoa.
   
 8. Chamoto

  Chamoto JF-Expert Member

  #8
  Mar 3, 2011
  Joined: Dec 7, 2007
  Messages: 2,078
  Likes Received: 1,115
  Trophy Points: 280

  Usimbishie bwana kuwa na adsense siyo kitu cha ajabu.
  Mimi nilianza haya mambo miaka nane iliyopita baadae
  nikamfundisha mdogo wangu ambaye alikuwa na miaka 15
  kuweka hizo adsense code kwenye wordpress blog.
  Kwahiyo mimi sishangai.

  Samjet keep it up ila naona hiyo searchsafari.com imekuwa
  parked kama unataka kuiuza let me know.
   
 9. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #9
  Mar 3, 2011
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,121
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  16 sio hatari sana, acha kumbishia jamaa. Hiyo searchsafari cuould be worth a couple of thousand dollars mzee! Mimi nina vijisite vyangu, ila viko TZ focused so traffic ngumu kupatikana.
   
 10. D

  Derimto JF-Expert Member

  #10
  Mar 3, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 1,305
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hapa suala ni kwamba mtu ametoa elimu kwa manufaa ya wengi na watu huchangia kulingana na upeo wao na uhalisi wao kwa ambao tayari wameshapitia uzoefu halufu wewe unaanza kumkanda mtu bila hata kumpa pumzi wewe kama unaona haifai hakuna mtu amekulazimisha kuamini we ni mtu mzima na una akili zako unajua kuchambua mambo kwa kina kama unataka tumia ushauri wake na kama hautaki uache! na kama unaona elimu ni ghali basi jaribu ujinga.

  Yuo guyz keep it up elimisheni watu kwa manufaa ya wengi na hata wengine wataweza kuwa pm.ili kuomba msaada wasaidieni achaneni na haya majungu ya ma litle thinkers wachache walioko humu ndani
   
 11. T

  TANZANIABORA Member

  #11
  Mar 3, 2011
  Joined: Feb 18, 2011
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu nashukuru sana kwa maelezo haya. Ni ya muhimu sana na nimekuwa nikijiuliza baadhi ya maswali ambayo majibu nimepata hapa. nikikwama nitakujulisha kamanda!

  Together we can!
   
 12. Slave

  Slave JF-Expert Member

  #12
  Mar 4, 2011
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 5,223
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
   
 13. James alamba

  James alamba Senior Member

  #13
  Jan 1, 2017
  Joined: Dec 23, 2016
  Messages: 179
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 45
  Kwaiyo ata kama nimesajiri tovuti yangu kwa co.tz pia naweza lipwa mkuuu
   
Loading...