Mambo Muhimu katika sheria ya ndoa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mambo Muhimu katika sheria ya ndoa!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Calnde, Aug 30, 2011.

 1. Calnde

  Calnde JF-Expert Member

  #1
  Aug 30, 2011
  Joined: Oct 7, 2008
  Messages: 1,373
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Kufuatia swala la ndoa siku hizi kuwa fashion, nimeona ni vyema kuangalia mambo machache muhimu katika sheria yetu ya ndoa. Karibu kwa

  mchango na mawazo yako. Kumbuka sheria ya ndoa ni ile ya Mwaka 1971 (Act No 5 of 1971).
   
 2. Calnde

  Calnde JF-Expert Member

  #2
  Aug 30, 2011
  Joined: Oct 7, 2008
  Messages: 1,373
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Maana halisi ya ndoa.

  Ndoa ni muunganiko wa hiari kati ya mume na mke ambao wamekusudia kuishi pamoja siku zote za maisha yao. Ni muhimu kusema ndoa ni kati

  ya mume na mke na sio mume na mume au mke na mke. Katika nchi ambazo wanaruhusu mahusiano ya jinsi moja kisheria, basi mahusiano hayo

  huwa hayaitwi ndoa bali 'Civil Partnerships'! Na ni lazima iwe ya hiari! Wanaume ving'ang'anizi mdake hilo.

  Section 9.-(l) Marriage means the voluntary union of a man and a woman, intended to last for their joint lives.
   
 3. Calnde

  Calnde JF-Expert Member

  #3
  Aug 30, 2011
  Joined: Oct 7, 2008
  Messages: 1,373
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Umri wa kuoa ni miaka 18 kwa mwanaume na miaka 15 kwa msichana. Lakini mahakama inaweza kutoa kibali kwa mvulana na msichana mwenye

  miaka kumi na nne kuoana pale tuu ambapo mahakama inaona ni vyema kufanya hivyo. hii ni kwa mujivu wa kifungu cha 13 cha sheria ya ndoa
   
 4. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #4
  Aug 30, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Kuna watu humu walikuwa hawajui kuwa mahusiano ya kimapenzi ni hiari.

  Mwaka jana niliandika mada humu kuhusu kuhisi demu wangu kumegwa alipoenda kumpeleka mwanae nchi nyingine kwenda kumuona baba yake. Watu walinistaajabisha sana! Eti wakawa wanahoji kwa nini nilimuachia aende?

  Alaa! Zaidi ya mimi kupinga yeye kwenda ningemzuiaje sasa kama alikuwa kanuia kufanya hivyo kwa gharama yoyote ile? Ningemfunga kamba asiweze kutembea? Kifikra watu tumetofautiana sana. Sasa kumbe hata sheria yetu ya ndoa inalitambua hilo la hiari!

  Kwenye mahusiano ya kimapenzi huwezi ukamzuia mwenza wako kufanya kitu ambacho anataka zaidi ya kupinga kwa maneno. Huwezi ukamchapa viboko au ukamdunda mangumi (ingawa wapo wafanyao hivyo lakini hayo yote hayasaidii chochote kama mtu kanuia kufanya kitu) na kudhani eti indo umefanikiwa kumkataza. Akiamua kufanya kitu atafanya tu.

  Sasa cha msingi ni wewe utachukua hatua gani baada ya yeye kukiuka matakwa yako. Nilikuwa sahihi mwaka jana na bado niko sahihi leo hii na nitaendelea kuwa sahihi kuwa mapenzi si utumwa wala utwana. Mapenzi ni hiari!
   
 5. Calnde

  Calnde JF-Expert Member

  #5
  Aug 30, 2011
  Joined: Oct 7, 2008
  Messages: 1,373
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Consumation of marriage.

  Ili kwamba ndoa iwe ni halali lazima iwe 'consumated'. Hili neno nimeliweka hapa linatokana na neno consumation. Consumation simply means being

  able to have sex for the first time in marriage within reasonable time. Ikiwa mtaoana na kwasababu zozote zile mkashindwa kufanya tendo la ndoa

  in 'reasonable time' sio kwamba ndoa hiyo itavunjwa bali ni kwamba haijawahi kufungwa kabisa! So be careful to see that u r fit otherwise utakuwa

  unapoteza muda!
   
 6. Calnde

  Calnde JF-Expert Member

  #6
  Aug 30, 2011
  Joined: Oct 7, 2008
  Messages: 1,373
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Mahusiano yoyote yale na hasa ndoa ni hiari. Hupaswi kumlazimisha mtu. Ndo maana sheria yetu ilipoona ukorofi wa wanaume wakiafrika na ubabe

  wetu ikaweka wazi kuwa ndoa ni hiari. Kutokana na tabia iliyokuwepo miaka ile sheria ikatamka wazi kuwa ni kosa kumchapa mwenza wako viboko.

  S. 66. For the avoidance of doubt, it is hereby declared that, notwithstanding any custom to the contrary, no person has any right to inflict corporal

  punishment on his or her spouse.
   
 7. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #7
  Aug 30, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Awesome! I was right back then and I am still right today and I will still be right forever more. Love/ romantic relationships are not and can't be forcible.
   
 8. Calnde

  Calnde JF-Expert Member

  #8
  Aug 30, 2011
  Joined: Oct 7, 2008
  Messages: 1,373
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Presumption of marriage. S 160 of law of marriage Act.

  Sasa hili litawagusa wanaume ambao wanapenda kukaa na mabinti za watu na kuwazalisha watoto bila kuwaoa. Sheria inasema katika kifungu

  nilichokitaja hapo juu kwamba ikiwa mwanamume na mwanamke wataishi pamoja kwa miaka miwili au zaidi, na kutambulika na watu

  wanaowazunguka kama mume na mke (reputation of marriage) basi watu hao mahakama inaweza kuwachukulia kuwa ni mume na mke!

  Implications zake

  Mara nyingi kama sio zote kifungu hichi kinatumika pale ambapo watu wa namna hii wamegombana na wanaachana. Mahakama itawatreat kama

  wanandoa wanaoachana na hivyo taratibu nyingine zitafuata ikiwemo kugawana mali, baba kutunza mke na watoto pamoja na majukumu mengine
   
 9. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #9
  Aug 30, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Kweli mkuu,

  Ila katika hiari hiyo naamini mtu hana ruhusa kusababisha maumivu ya aina yoyote kwa mpenzi wake (to inflict any kind of pains on your spouse). Hapa siongelei kuchapana makonde (corporal punishment)!!
   
 10. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #10
  Aug 30, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Hiyo sehemu (blue) inatakiwa kufutwa. Kwa vile ndoa ni muungano wa hiari basi hakuna maana kuweka vinzingiti kwamba mtu asiwe na uwezo wa kubadili mawazo na kuhamishia hiari yake mahali pengine!!
   
 11. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #11
  Aug 30, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Hapo tupo ukurasa mmoja kaka. Intentional infliction of emotional pain and mental distress is not right whatsoever in any relationship.
   
 12. Calnde

  Calnde JF-Expert Member

  #12
  Aug 30, 2011
  Joined: Oct 7, 2008
  Messages: 1,373
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Ni Jukumu la Mwanaume kumtunza mke wake! Maisha yamebadilika siku hizi na wanawake wanatunza wanaume. Lakini sheria yetu ya ndoa katika kifungu cha 63 kinamtaka mwanaume amtunze mke wake kwa kumpatia makazi, makazi, chakula nk. Mwanamke atakuwa na jukumu hilo tuu ikiwa mumewe ni incapacitated na hivyo hawezi kufanya kazi. Mwanaume acha ugumu tunza mkeo otherwise wenzio watakusaidia.
   
 13. Calnde

  Calnde JF-Expert Member

  #13
  Aug 30, 2011
  Joined: Oct 7, 2008
  Messages: 1,373
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Na kwa sababu hito kifungu cha 64 kinampa mwanamke haki ya kukopa kwa jina la mwanaume (yaani mume atakuja kulipa), kutumia fedha za mumewe au kuuza mali inayohamishika ili kupata pesa kwa ajili ya 'mahitaji yake muhimu' na ya mtoto. Ukimnyima mkeo pesa anaweza kuuza simu yako au hata gari lako ili apate pesa ya chakula au kulipa ada ya mtoto. Ni halali kabisa pale ambapo mume na mke wanaishi pamoja, au wametengana na mume anapaswa aendelee kumtunza au pale ambapo mume amemtelekeza mke
   
 14. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #14
  Aug 30, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Sikubaliani na hicho kipengele. Kinahitaji marekebisho.
   
 15. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #15
  Aug 30, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Hicho kifungu nacho kinahitaji kurekebishwa na kusema ni jukumu la wote wawili kutunzana. Na siyo mmoja atunzwe tu ilhali hana disability yoyote na anaweza kufanya kazi kama wengine na kujipatia riziki halali.
   
 16. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #16
  Aug 30, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Sasa yule demu wako alieyeenda Canada alikuacha mzima kwa hayo maeneo?????
   
 17. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #17
  Aug 30, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Sheria inasemaje kuhusu majukumu ya huyo mwanamke anayetakiwa kutunzwa kama glass???
   
 18. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #18
  Aug 30, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Umeona na wewe kaka,

  Yaani kwanza ni jukumu lako kumtunza mtoto wa watu...na halafu sheria inampa mamlaka ya kuuza phoenix yako ili eti akalipie matumizi yake na mtoto.

  Hii sheria inahitaji marekebisho ya haraka sana.

  Ndio maana mimi napendekeza kwamba ndoa ziwe katika mfumo wa corporate union. Kila mtu awe na shea zake ili mambo yakienda mrama ajue anachoambulia!!
   
 19. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #19
  Aug 30, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Hayo madhila niliweza kuya pre-empt kabla hata hajafunga hiyo safari yake ya Toronto kwa hiyo nilikuwa pouwa kabisa. Ila nilimaindi kwa muda mfupi.
   
 20. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #20
  Aug 30, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Pole sana kaka,

  Huo ndiyo ukubwa na kuishi kwingi ni kuona mengi,

  Hayo ungeyaona wapi kama ungeisha ukiwa njiti??????!!!!!
   
Loading...