Mambo makuu yaliyojiri utawala wa Magufuli, November 2015 hadi March 2019

Freed Freed

JF-Expert Member
Jun 27, 2017
6,230
6,469
1. Ununuzi wa ndege na ufufuaji upya wa ATCL.

2. Kutekwa, kupotea, kujeruhiwa na hata kuuawawa kwa watu mbalimbali. Rejea miili ikiokotwa virobani.

3. Hamahama ya wapinzani.

4. Mgogoro wa kodi na makampuni.

5. Ujenzi wa miundombinu mbalimbali nchini. Haijawahi kutokea kasi ya ujenzi wa aina hii tangu Uhuru.

6. Kutoweka migomo kote nchini, sio vyama vya wafanyakazi, mashirika, vyuoni yote kmyaaa.

7. Kupigwa marufuku mikutano na maandamano ya kisiasa. Tufanye kazi hadi 2020.

8. Sakata la Tundu Lisu na umbeya wake Ughaibuni.

9. Kikokotooo, jamani kikokotoooo jamaniiiii.

10. Vitambulisho vya Wamachinga.

11. Watu kupokonywa aridhi isiyoendelezwa.

12. Kamatakamata na kuswekwa ndani wapinzani.

13. Ufunguzi wa viwanda mbalimbali nchini vya viwango tofauti.

14.Serikali kuu kuhamia Dodoma. Baadhi ya wizara zimeshahama.

15. Usambazaji umeme vijijini kwa kasi.

16. Elimu bure(Elimu msingi) japo vyuo vikuu mikopo imepungua.

17. Kutoweka kwa nyongeza ya mshahara na madaraja kote serikalini.

18. Fungafunga Mabenki.

19. Sakata la Bureau de change.

20. Mdororo sekta za biashara mbalimbali.

21. Fungiafungia vyuo vikuu sanii.

22. Kupungua kwa ajira serikalini.

23. Tumbuatumbua watumishi wazembe.

24. Korosho, koroshoooooooooo.

25. NOA zetu jamanii, Makinikia, Prof Urosooo.

26. Vitambulisho vya wamachinga/ wajasriamali wadogo.
 
Bila Shaka wewe Ni friends of magu n kaga..m..e...
Kwamba namba nane..hujaona uzito wake??? Umeshindwa kusema kupigwa risasi kwa lissu na mpka Sasa Hakuna kinachoendelea?? Na huo umbea umeujuaje Kama na ww sio mbeya????

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maelfu ya wanafunzi elimu ya juu kukosa mikopo ,kesi za uhujumu uchumi kwa matajiri ambao ana visasi nao .
 
Dhuluma waliofanyia wafanyabiashara wa pombe aina viroba waliponyang'anywa pombe yao ambayo ndio mitaji yao .
 
Dhuluma waliifanyiwa wafanyakazi wenyewe vyeti feki , maana hawakujipeleka kazini wenyewe ,hawakutenda makosa yoyote ya kiutumishi na je mtumishi akigundulika ameghushi ili apate ajira hatua zake ni zipi je jiwe alizifuata au alikurupuka kama kawaida ,vipi michango yao ya mifuko ya hifadhi ya jamii kuidhulumu .
 
Back
Top Bottom