Mambo kumi (10) ya ali kamwe katika derby ya Simba na Yanga

Mnyuke Jr

JF-Expert Member
Jul 3, 2021
4,471
6,371
Anaandika @alikamwe

Mambo 10 nilioyaona Simba vs Yanga

1: DAR ES SALAAM is GREEN & YELLOW 🟢🟡. WENYE NCHI NI WANANCHI🙌 Pointi 3 za HESHIMA. Pointi 3 za KIBABE. Yanga wanaweza kukosa Ubingwa, Lakini angalau wameweka alama isiyofutika kwenye moyo wa Rais, Mama Samia..👏

2: WHAT A MATCH! Yanga walicheza mechi yao kipindi cha kwanza, wakafunga 1. Simba wakacheza mechi yao kipindi cha pili, Hawakufunga. End of The Story.

3: Wapi Yanga walifanikiwa kipindi cha kwanza? System ya 4-2-3-1 with Style ya Pressing kwenye High Line iliwapa mshangao mkubwa sana Simba. Kocha wa Yanga, Nabi alikuja kuwabana Simba katikati ya kiwanja na kumtega Kisinda kwenye mgongo wa Tshabalala. Kama Yacouba angekuwa makini, Yanga ingeweza kufunga bao zaidi ya moja kipindi cha kwanza

4: Nini Simba walibadili kipindi cha pili? Sub ya Bwalya ilikuja kuwapa Simba style tofauti ya kuvunja Line ya kiungo ya Yanga. Waliutoa mchezo katikati na kupiga mipira mirefu iliyowatanua Yanga pembeni. Yanga waliandaliwa vyema sana kisaikolojia👏 Licha ya presha kubwa, Safu ya ulinzi haikupaniki..

5: Shomari Kibwana👏 WOW. WHAT A PERFOMANCE🙌 Dhidi ya mawinga bora East Africa, Kijana alitulia. Alicheza kwa moyo wake! Alijitoa kukimbia na kujitolea kuweka miguu yake kwenye kila hatari

6: Nilipenda Reaction ya wachezaji wa Simba kipindi cha pili! Bocco alikuwa vyema kwenye pressing, Miquissone akaongeza presha na Wawa akawa anapiga mipira mingi mirefu kwenye nafasi.

7: Nafikiri Simba ilihitaji 'sub' ya Dilunga kipindi cha pili kabla ya Kagere na Mugalu. Kwanini? Simba ilihitaji kasi katikati ya kiwanja. Dilunga angewapa Option nzuri katika kutengeneza nafasi kuliko kujaza straika ambao walitegemea kufunga kwa mipira ya juu tu

8: Fei Toto 🙌 Hii Perfomance ya Leo inaweza anaweza kuitunza kwenye Diary yake. WoW. Utulivu, ukokotaji wa viwango na pasi za uhakika.. ASANTE SANA FEISAL.

9: Nafikiri Dickson Job aliutanua mwili wake kwa mkono. ILISTAHILI KUWA PENALTI. Nafikiri pia Morrison alivutwa akiwa ndani ya boksi. ILISTAHILI KUWA PENALTI

10: Well Done Dickson Job. Tshabalala aliteswa na kasi ya Kisinda kwa kukosa msaada wa winga wake

Nb: Man Of The Match ... MZEE MPILI 😀

© Insigne
 
Mzee mpili amefika salama Kigoma jioni ya jana, tunamtakia kila lenye kheri katika majukumu yake.
 
Kwa refa makini Simba alikua angepata penati mbili ila kwakuwa Simba sio malamiko f.c tupo kimyaa,ila ingekuwa kwa Utopolo ndo wamenyimwa penati hizo mbili wangelalamika mpaka chato kwenye kaburi la mzee.
 
Sawa tumechukua malalamiko yenu, tutayafanyia kazi
 
Kwa refa makini Simba alikua angepata penati mbili ila kwakuwa Simba sio malamiko f.c tupo kimyaa,ila ingekuwa kwa Utopolo ndo wamenyimwa penati hizo mbili wangelalamika mpaka chato kwenye kaburi la mzee.
Ili kuwathibitishia kuwa timu yenu iko bora, mkikutana nao kigoma wapigeni 3-0. Sio tena iwe kulilia penati na huko.
 
Ili kuwathibitishia kuwa timu yenu iko bora, mkikutana nao kigoma wapigeni 3-0. Sio tena iwe kulilia penati na huko.
Ilo halina mjadala Simba ya sasa ni ya kubeba mataji na sio kutolea macho Derby wakati kubeba VPL ni uhakika 100%.
 
Back
Top Bottom