Mambo JF Family

DocJayGroup

JF-Expert Member
Jan 17, 2020
1,654
3,327
Jina langu ni John. Nafurahi kujiunga na JF family au jumuiya ya JamiiForums. Nilizaliwa Dar miaka ya 80's. Primary nilisoma Kilimanjaro na Tanga. Secondary nilisoma shule ilioko mkoa wa Arusha.

Baada ya hapo nilifanikiwa kwenda nje kimasomo na kimaisha. Hobbies zangu ni kusafiri na kuona mambo (travel and adventure), kujifunza mambo mapya, kusoma vitabu, kufanya biashara, na kuwa pamoja na familia na marafiki.

Niulize chochote nitakujibu.
 
Huko nje ni nchi gani hususani unaishi, na je ni fursa zipi za uwekezaji na kibiashara zinapatikana huko uliko?

Sent using Jamii Forums mobile app
Nipo USA. Fursa zipo nyingi na nyingi na nyingi sana hasa za kufanya kazi na unalipwa kwa dola. Tatizo ni kupata US viza sababu ubalozini wanasumbua siku hizi na sheria pia USA kwa wahamiaji wamebana sana sio kama zamani. Kwa hio fursa zipo lakini ndio hivyo inabidi ufike States kwanza kisha upate makaratasi ya kufanyia kazi. Hayo mawili ndio shughuli kidogo ipo, lakini inawezekana.
 
Huko nje ni nchi gani hususani unaishi, na je ni fursa zipi za uwekezaji na kibiashara zinapatikana huko uliko?

Sent using Jamii Forums mobile app
Uwekezaji kwa kweli USA kwa immigrants ni challenging kidogo sababu una-compete na corporations kubwa sana zenye billion of dollars. Kwa immigrants jambo zuri ni kufanya kazi na kulipwa dollars ambazo inaweza kuwa kati ya $5,000 na $10,000 kwa mwezi. Halafu unajitahidi ku-save ili uwekeze nyumbani tz sababu huko hata $10,000 inafanya kitu wakati kwa USA kuwekeza unahitaji hundreds of thousand of dollars au hata 1 million dollars na zaidi ili kufanya kitu at least cga kueleweka.
 
Nipo USA. Fursa zipo nyingi na nyingi na nyingi sana hasa za kufanya kazi na unalipwa kwa dola. Tatizo ni kupata US viza sababu ubalozini wanasumbua siku hizi na sheria pia USA kwa wahamiaji wamebana sana sio kama zamani. Kwa hio fursa zipo lakini ndio hivyo inabidi ufike States kwanza kisha upate makaratasi ya kufanyia kazi. Hayo mawili ndio shughuli kidogo ipo, lakini inawezekana.
Sawa mkuu ahsante, ila jitahidi utafute na fursa za kibiashara na uwekezaji mkuu hizo za kazi peke yake hazitoshi kwa kipindi ulichoishi huko naamini unanafasi ya kufahamu zaidi kuhusu uwekezaji na biashara hasa kwa kuzingatia bidhaa tunazozalisha hapa kwetu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sawa mkuu ahsante, ila jitahidi utafute na fursa za kibiashara na uwekezaji mkuu hizo za kazi peke yake hazitoshi kwa kipindi ulichoishi huko naamini unanafasi ya kufahamu zaidi kuhusu uwekezaji na biashara hasa kwa kuzingatia bidhaa tunazozalisha hapa kwetu

Sent using Jamii Forums mobile app
Nimejaribu kutafuta masoko ya Tanzanian products hasa agricultural lakini quality ndio tatizo. Hawaamini kabisa products za africa. Ndio maana hata korosho yetu kwa USA wananunua tokea India na Vietnam sababu zina higher quality vs product inayotoka tanzania moja kwa moja. Sijakata tamaa lakini ni uphill battle.
 
Ni sawa mkuu nimekuelewa lkn hata hizo USD 10000 kwa mwezi hapa kwetu pia zinalipwa

Kila la heri huko nje
Uwekezaji kwa kweli USA kwa immigrants ni challenging kidogo sababu una-compete na corporations kubwa sana zenye billion of dollars. Kwa immigrants jambo zuri ni kufanya kazi na kulipwa dollars ambazo inaweza kuwa kati ya $5,000 na $10,000 kwa mwezi. Halafu unajitahidi ku-save ili uwekeze nyumbani tz sababu huko hata $10,000 inafanya kitu wakati kwa USA kuwekeza unahitaji hundreds of thousand of dollars au hata 1 million dollars na zaidi ili kufanya kitu at least cga kueleweka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sawa mkuu ahsante, ila jitahidi utafute na fursa za kibiashara na uwekezaji mkuu hizo za kazi peke yake hazitoshi kwa kipindi ulichoishi huko naamini unanafasi ya kufahamu zaidi kuhusu uwekezaji na biashara hasa kwa kuzingatia bidhaa tunazozalisha hapa kwetu

Sent using Jamii Forums mobile app
Hio post hapo juu nimemaanisha kwamba Tanzania tuna korosho. Na nikienda supermarket hapa USA kama Walmart au Costco kununua korosho, nitakula korosho ya Tanzania lakini kwa kopo itasema made in India/ Vietnam kwa sababu ilitoka tz ikaenda kuwa processed huko India au Vietnam na ndio ikaletwa USA. Makampuni ya USA hayaamini kununua products directly kutoka nchi kama tz. Tuendelee kuboresha bidhaa zetu na kukuza kiwango, iko siku tutaaminika tu.
 
Ni sawa mkuu nimekuelewa lkn hata hizo USD 10000 kwa mwezi hapa kwetu pia zinalipwa

Kila la heri huko nje

Sent using Jamii Forums mobile app
Tatizo ya Tz ni kwamba ugali kidogo walaji wengi ndugu yangu. Kazi hizo wanazozitaka ni wengi sana na zipo chache sana. Kwa USA ziko nyingi sana ni wewe tu. Hio ndio tofauti. Asante kunitakia la kheri. Ni kupambana tu kwa kweli.
 
Karibu sana jukwaani mkuu.

Swali: Hivi wewe hapo ulipo unajiona ni tajiri au fukara? Kama ni fukara, Je, unadhani kwa nini wewe ni fukara? Kama tajiri, Je, unadhani kwa nini wewe ni tajiri?

KARIBU.
 
Kuna watu wanatusadikisha kuwa ukienda USA maisha ni matamu sana,hebu tueleze maisha yakoje na utamu huo ni vipi,watu wanapata pesa kiulaini bila ya kutoka jasho sana au pesa yake iko nje nje sana ukilinganisha na huku kwetu...?
 
Kuna watu wanatusadikisha kuwa ukienda USA maisha ni matamu sana,hebu tueleze maisha yakoje na utamu huo ni vipi,watu wanapata pesa kiulaini bila ya kutoka jasho sana au pesa yake iko nje nje ukilinganisha na huku kwetu...?
Inategemea na mtu amekuja kutafuta nini. Kwa starehe kweli zipo za kila aina na kila sehemu. Ukitaka mademu wa kizungu ndio kwenyewe. Nina mdogo wangu anawabadilisha kama nguo. Yap. Na kuna sehemu kama Vegas kila kona starehe masaa 24. Kuna matamasha kila sehemu ya watu kama Jay Z nk ukitaka kuwaona. Anasa za kiutu uzima pia. Pia urahisi wa maisha, Mabarabara makubwa. Umeme haukatiki, maji unakunywa kwa bomba nk.

Lakini kwa mtu kama mimi niliyekuja kutafuta maisha wala hakuna raha yeyote. Nilikula sana raha USA miaka ya awali baadaye nikaona ni ubatili mtupu. Ukiamua kujijenga na kuwekeza Tz kwa kweli hakuna raha yeyote huku. Unafanya kazi tu na chakula chenyewe kibovu, matunda sio fresh, nyama ya kuku mbaya nk. Pia hali ya hewa barafu kila kona. Kwa hio Tanzania ina raha zake nyingi tu.

Kwa hio inategemeana na mtu. Kwangu binafsi napenda Tz zaidi huku niko kikazi na ku-make tu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom