Mambo gani umewahi kumuomba Mungu na akakujibu papo hapo?

Mungu ni mkuu wa mbingu na ardhi ukimuomba na ukalishika neno lako utauona ukuu wake ndani yako, na utaweza kutawala duniani pasipo mawaa ya wanadamu, hakuna mchawi yeyote wala mganga wa kichawi yeyoote wala jini lolote litakusogelea kama ukijenga urafiki na mungu, ukampenda kwa moyo wako wote , kwa nguvu zako zoote nakuwapenda majirani zako kama unavyojipenda hata kama wanakuchukia wapende tu maana wakikufanyia ubaya wowote wanakutana na moto mkali kwenye ulimwengu wa roho, mungu hajawahi kushindwa chochote na yupo na wanaomwamini popote wanapokwenda kila sekunde.
 
Nilikuwa chooni, bado mtoto mdogo miaka nane hivi, baada ya kumaliza kukata gogo nafungua maji bombani holaa!! Nikafunga bomba alafu nikamuomba Mungu, baada ya sala nikafungua tena, maji hayoooo......HAKUNA ZAIDI YA MUNGU.
Mfyuuuuu
 
Mke jamani mke, kuna siku niliomba nikamwambia Mungu niko tayari sasa naomba umlete mke wangu sasa, siku kadhaa baba akaniambia mwanangu kuna bint hapa mimi na mama yako tunaona atakufaa, nilipo mwangalia kwa siku kadhaa anafaa kabisa, leo hii tunataka kutoa posa nimuoe, Mungu ni kila kitu kwetu wanadamu aisee.
 
Maisha yana mambo mengi jamani, ukiujua ulimwengu na ukawajua vizuri walimwengu hakika utaishi kwa raha sana, nilichokigundua duniani watu wanaokufa/kutwaliwa na mwenyezi mungu ni wachache saana. Vifo vingi watu wanauliwa na shetani kwa sababu ya kuishi katika dhambi na wengine kujikabidhi kwake kama suruhisho la kufanikiwa kimaisha na kusahau kuwa shetani hajawahi kuwa na urafiki na mwanadamu. Waganga wa jadi, mizimu, majini na wachawi wote ni mawakala wa shetani kwa maani hayo ni matawi madogo madogo ya kumkusanyia watu shetani, ukijiungani nao ni kama vile ukisajili laini mtandao wowote wanabaki na data zako zote, popote unapoenda wanakuona na wakiitaji kukufanya chchote watafanya saa yoyote. waganga hao wakiitaji kafara yoyote ya damu wanaangalia kati ya wateja wao wanachua mmojawapo saa yoyote wakikuitaji, kupitia ugonjwa wowote duniani wanaweza kukutengezea hata UKIMWI au ungonjwa wowote na vipimo hospital vikaonesha hivohivo, na ukafa watu wakajua ni ngoma ya kawaida kumbe ya kutengeneza kwenye madhabau ya giza, mimi ni muhanga wa hayo mambo nimepiga ushirikina saana mpaka waganga wenyewe wakaanza kunitengenezea magonjwa nimeugua saana kwa magonjwa ya kawaida na hospital wanaona lakini ukitumia dawa unapona mwezi huu mwezi unaofata unaugua tena, nilikuwa nishaacha kula baadhi ya vyakula sababu ya madonda ya tumbo kumbe mazingaombwe tu. Tokea nilivojua kuwa MUNGU anaokoa na kuponya nimemkabidhi maisha yangu nakula mpaka pilipili wala sisikii chochote. ni magonjwa mengi tu yamepotea.Ukweli ni kwamba wanadamu tunaangamia kwa kukosa maarifa mungu yupo na anatupenda sana, hata kama una dhambi nyekundu mungu anasamehe zitakuwa nyeupe kama theruji, mpende mungu wako kwa moyo wako woote inua imani yako usiamini kitu kingine unapopatwa na tatizo muamini mungu muite kwa IMANI utamuona sekunde hiyo hiyo kupitia malaika wake, tatizo la wanadamu ni IMANI NDOGO.
 
mimi pia nashangazwaga na hilo mtu anakwambia utaona nakuweka kwenye maombi.
Maombi ukiwekwa mambo yanaanza kukuharibikia na Muombaji anamtukuza Mungu kwa kukuonyesha magumu anayokupa. Aisee "being righteous isn't easy task" Mfalme suleiman ndio maana anasema mambo yote ni ubatili na kujilisha upepo yafaa nini hekima aliyojijaza mtu wakati mwisho wa siku atalala kitandani pake ausubirie umauti
Inategemea anakuweka kwenye maombi yapi!mi naongelea maombi yanayoombwa sawasawa na Neno la Mungu Biblia haijasema umuombee mtu mabaya!
Na nafikiri kuna ambacho umeshindwa kuelewa!

Mfano;Biblia hiyohiyo inasema Mungu anarudisha vilivyoibiwa,kwahiyo unapoanza kuomba kudai virudishwe unafikiri aliyekua ameviiba atabaki salama?kumbuka wanaoiba ni watu(ambao adui anawatumia,Mungu ni roho shetani ni roho ili wafanye kazi wote wanahitaji watu kutimiza kusudi)

Biblia hiyohiyo inasema "usimuache nwanamke mchawi aishi"...! Ss km mtu anamuomba Mungu ashughlike na waliomroga unafikiri Mungu atamuacha salama huyo mchawi?

Isaya 42:22... Watu hawa wameibiwa wametekwa wamenaswa kwenye mashimo na hapana asemae rudisha...... Unaposimama sawasawa na neno kudai na kurudisha unafikiri waliofanya hayo wanabaki salama?
Yaani mtu aende kwa mganga akuharibie ndoa,au vyovyote vile,then unapoomba sawasawa na neno Mungu anapita kukupigania mtt wake halafu aliyekuendea kwa mganga abaki salama?!
Nimekupa mifano michàche ipo mingi tu.

So huu ndo uchawi?,cha msingi kuomba sawasawa na Warumi 8:26!nje ya hapo Mungu huwa hajibu!
Soma tu neno vzr Roho mtakatifu yupo kutusaidia!
maombi ya Vita yapo,lkn biblia inasema "vita ni vya Bwana"kwahiyo ukiomba kazi ya kukupigana ni ya Mungu,ss atapiganaje ,watapigwaje we haikuhusu!

Ushafikiria Mungu alivyowaokoa wana wa israel,akapita na kuwapiga mpk kufa wazaliwa wa 1 wa misri?utasemaje hapo? Israel waliwahi omba hivyo?
Nachojua natakiwa kuomba na Mungu anaingia kazini unless otherwise utaishia kulalamika!

So case yangu isikushangaze sn mkuu!mi mtu akienda kwny nguvu za giza kwa ajili yangu,familia yangu simuachi,naomba sana tu!

JESUS IS LORD
 
upo vizuri
 
Maisha yana mambo mengi jamani, ukiujua ulimwengu na ukawajua vizuri walimwengu hakika utaishi kwa raha sana, nilichokigundua duniani watu wanaokufa/kutwaliwa na mwenyezi mungu ni wachache saana. Vifo vingi watu wanauliwa na shetani kwa sababu ya kuishi katika dhambi na wengine kujikabidhi kwake kama suruhisho la kufanikiwa kimaisha na kusahau kuwa shetani hajawahi kuwa na urafiki na mwanadamu. Waganga wa jadi, mizimu, majini na wachawi wote ni mawakala wa shetani kwa maani hayo ni matawi madogo madogo ya kumkusanyia watu shetani, ukijiungani nao ni kama vile ukisajili laini mtandao wowote wanabaki na data zako zote, popote unapoenda wanakuona na wakiitaji kukufanya chchote watafanya saa yoyote. waganga hao wakiitaji kafara yoyote ya damu wanaangalia kati ya wateja wao wanachua mmojawapo saa yoyote wakikuitaji, kupitia ugonjwa wowote duniani wanaweza kukutengezea hata UKIMWI au ungonjwa wowote na vipimo hospital vikaonesha hivohivo, na ukafa watu wakajua ni ngoma ya kawaida kumbe ya kutengeneza kwenye madhabau ya giza, mimi ni muhanga wa hayo mambo nimepiga ushirikina saana mpaka waganga wenyewe wakaanza kunitengenezea magonjwa nimeugua saana kwa magonjwa ya kawaida na hospital wanaona lakini ukitumia dawa unapona mwezi huu mwezi unaofata unaugua tena, nilikuwa nishaacha kula baadhi ya vyakula sababu ya madonda ya tumbo kumbe mazingaombwe tu. Tokea nilivojua kuwa MUNGU anaokoa na kuponya nimemkabidhi maisha yangu nakula mpaka pilipili wala sisikii chochote. ni magonjwa mengi tu yamepotea.Ukweli ni kwamba wanadamu tunaangamia kwa kukosa maarifa mungu yupo na anatupenda sana, hata kama una dhambi nyekundu mungu anasamehe zitakuwa nyeupe kama theruji, mpende mungu wako kwa moyo wako woote inua imani yako usiamini kitu kingine unapopatwa na tatizo muamini mungu muite kwa IMANI utamuona sekunde hiyo hiyo kupitia malaika wake, tatizo la wanadamu ni IMANI NDOGO.
kweli mzee hata ajali nyingi ni shetani tu.wachache sana wanajua jinsi gani huu ulimwengu unavyoendeshwa
 
Hakika mkuu,kwanza alikuwa islam akamfuata Yesu...so ananipenda nampenda sana....

Alikuwa na form six failure...nilimsomesha cerificate up to degreee!

So....wanaosema mwanamke asomeshwi mie nawaangalia tu maana elimu yake sasa inamsaidia mwenyewe na watoto wake.

Kwahiyo hata nikodondoka leo hii ataweza kuwamudu watoto badala ya kutafuta masaada wa ndugu.

Ni risk kwa Mabaharia lkn penye upendo wa kweli na Mungu kuwasimamia very simple.

Hata house tumeshare names kumpa assurance no one atakusumbua in my absentee.

Note. Kila mtu ana njia zake za kuendesha familia yake don't copy and pest, huyu ni mshauri wangu namba moja.

Ana miproject kibao kichwani nashindwa kukimbizana caz mshiko sina.

Ubinafsi,choyo,vimetingisha sana ndoo.....hapa kwenye ubinafsi ndio issue sana....

Wanaume tunakwama tukipata pesa tu tunaongeza mademu, marafiki wengi msululu,tunaanza kuwa viburi kwa sana hiyo yote nguvu ya pesa.

Mungu hamtupi mja wake tukipigika sasa mikono nyuma tunarudi kwa wake zetu..

Take note brothers tuwapende wake zetu all weathers hakika Mungu ataendelea kutubariki na hatutapungukiwa kamwe,nyumbani ndio sehemu pekee ya kupata faraje kwingine ni temporarily tu.

Mwisho tumuombe sana Mungu atuongoze ktk njia zake.

1.Omba Mungu sana
2.Penda familia yako mke, watoto na ndugu wa pande zote 2
3.Tufanye sana kazi ni jukumu letu kuzilisha,kulinda na kusimamia familia
4.Piga sana show za kibabe kwa mke wako sio nduguyu,wenyewe wanasema hata kwetu nimeacha kitanda,sijaja kulala wala kula hapa.

Huyu ni zaidi ya mke ni rafiki,mpenzi,mwanangu nk....kwanza yy ananiita best au baba mzazi maana mzazi wake alitangulia mbele za haki.
Wanaume kama wewe mmebaki wawili tu nafikiri.Ubarikiwe sana.
Wachache sana utakuta anajali sala no.4 anazembea.
 
Vip mkuu?
Kabla ya kuomba hakikisha umetakasika hauna makando kando,jitakase kwa kuomba sala ya toba ili usamehewe dhambi zake, hata kama wewe kwa macho ya nyama hauzioni dhambi zako ila usijihesabie haki, pia kumbuka maombi mengine hayawezekani mpaka kwa kufunga na kuomba, kumbuka kufunga ni muhimu, na usisahau nguvu ya sadaki toa sadaka kubwa kwa mama wajane na hata kwa watoto yatima au kanisani, ndugu yangu kupitia haya tatizo lako ni kidogo sana kwa jehova.
 
Hivi mkuu sala ya toba ndo ipi? Na sadaka naitoa Wakati gani?

Je wajane wanapatikana wapi?
 
Unafunga siku ngapi na sadaka ya aina gani inayotakiwa?
Waweza kufunga kuanzia siku 7 kama afya yako inaruhusu, lakini kama kama hauko sawa kiafya funga hata siku moja, na siku hiyo jitakase kweli kweli shinda ukiongea na mungu wako kuhusu shida yako,omba ujazo wa roho mtakatifu ndani yako akuongoze njia zako zote, usimkwaze mtu yeyote, samehe toka moyoni woote waliokukosea, kuhusu sadaki toa chochote kinachokuuma| kwa maana kama una elfu kumi ukitoa mia tano haiwezi kukuuma, lakini pia waweza wapelekea mama wajane na watoto yatima mahitaji yao kulingana na uwezo wako.
 
Back
Top Bottom