Mambo gani umewahi kumuomba Mungu na akakujibu papo hapo?

Waweza kufunga kuanzia siku 7 kama afya yako inaruhusu, lakini kama kama hauko sawa kiafya funga hata siku moja, na siku hiyo jitakase kweli kweli shinda ukiongea na mungu wako kuhusu shida yako,omba ujazo wa roho mtakatifu ndani yako akuongoze njia zako zote, usimkwaze mtu yeyote, samehe toka moyoni woote waliokukosea, kuhusu sadaki toa chochote kinachokuuma| kwa maana kama una elfu kumi ukitoa mia tano haiwezi kukuuma, lakini pia waweza wapelekea mama wajane na watoto yatima mahitaji yao kulingana na uwezo wako.
Asante sana mkuu

Kwa watoto yatima ntawapata je wajane nawapata wapi?

Na hiyo sala ya toba ni ipi mkuu

Samahani kwa maswali mengi
 
Niwakumbushe tu mkifanikiwa mnayoyapata kwa nguvu za mwenyezi Mungu muwe mnatoa na sadaka na kumshukuru, kuna wengine mmekua sugu Mungu anawasaidia kila siku lakini kanisani hamuendi, sadaka za shukrani hamtoi, kuomba misa hamfanyi, kutubu mnapomkosea Mungu hamfanyi, nawakumbusha mzingatie na hayo...s
 
Hivi mkuu sala ya toba ndo ipi? Na sadaka naitoa Wakati gani?

Je wajane wanapatikana wapi?
Zaburi 51 ukiisoma kwa imani ni toba na utajikuta unamuomba Mungu msamaha na kutaja makosa yako yote
Cha kukusaidia tafuta nyimbo za kuabudu wkt unaomba ziwe zinaimba taratibu kusukuma maombi yako,jifunze kuinenea sadaka yako kbl haujaitoa
 
Nilikuwa na kesi ya mirathi ya marehemu mume wangu ambae sikuzaa nae lakini tulipata mafanikio kipindi kifupi. Ile kesi ilitawaliwa na upendeleo nadhani na rushwa hivyo ikaonekana mimi kama sina haki. Hakimu na watoto walikuwa wananitia maneno ya kuudhi sana kiasi siku moja nilopotoka mahakani nilijifungia chumbani kwanza nililia sana kwa uchungu kisha nikaanza kuongea na Mungu kama nipo nae pale.

Nilichokuwa namuomba niweze kuliondoa hili swala katika mawazo na nafsi yangu na Liwe kama halinihusu na kama vile hakuna nilichopoteza.

Niliomba/kuongea takriban kwa saa nzima na baada ya hapo nilipata usingizi mzito sana na nilipoamka nikajikuta ni kama mtu aliyetua mzigo sana.

Hadi hii leo ni mwaka wa 17 sikurudi tena mahakamani na nilishasahau kabisa!
MUNGU ANAJIBU ANAPOOMBWA KWA DHATI
huu ndo ulipaswa kuwa Uzi na mtoa Uzi alipaswa kukomenti tu basi.
 
Mie naona kama Vile hii yote ni kawaida ya maisha hata usipoba ni hivyo tu. Sema roho yako inaamini katika Kuomba ila mimi naamini katika kujituma na kutokukata Tamaa.
Mwanzoni nilikuwa mtu wa kuomba ila nikafika mahali nikaona kabisa haya mambo yanaenda kama vile yapo programmed na sio kwamba kuna kuomba na ukabadilisha mpanho uliopangiwa. Kama ulipangiwa baada ya Kukaa bila kazi kwa mwezi mmoja baada ya siku kadhaa utapata kazi au kikazi fulani, na hiyo hata usipoomba inakuja tu.
Maisha haya yapo programmed na Programmer wetu ..Mungu. Yeye akishakupangia hivyo ndio utakuwa hivyo hakuna litakalokuja kutokea yeye hajalipanga.
So wewe unaye amini katika kuomba endelea kufanya hivyo kuutidhisha Mouo wako kuwa umeongea na Mungu, ila Mungu ashapanga maisha yako kamaliza kwahiyo usidhani anajibu bali mambo yanakuwa yamefika wakati wake wa Kutokea basi nawewe unaaminj eti kajibu.
Iko siku utakuja hapa Kumkiri Yesu kwamba amekujibu, Amen.
 
Miaka kadhaa nyuma nikiwa Safarini Kikazi kwenda Mwanza nikapitia Moro kwa Bi Mkubwa kumsabahi na kulala home kwa siku mbili tatu maana nilikuwa na Private Car.
Kesho yake jioni Bi Mkubwa akanipeleka nje ya Mji kwenda kuangalia Shamba / Kiwanja ambacho nilikinunua Baadae.
Mara baada ya kumaliza kuangalia Shamba hamad Funguo za Gari sizioni,nilikuwa nimevaa Jeans yangu moja mfuko mmoja wa mbele kwa ndani ulikuwa umetoboka.
Sikukumbula niliweka mfuko gani ila nikahisi ntakuwa niliweka kwenye huo mfuko.
Tukaanza kutafuta kuanzia nilipo park Gari,Kumbuka giza lilishaingia na tuko Mashambani, Gari New Model,huwezi kuchonga funguo kiholela Mpaka uende through Manufacturer na kazini wanajua Mwanaume niko Safarini Mwanza.
Tafuta na kutafuta hamna kitu.
Bi Mkubwa akaanza ku Panic, Mzee mwenye Shamba ka Panic,anaogopa, Akaja kijana wake wa Maziwa kusaidia kutafuta, mimi Simu yangu charge imeisha hivyo torch imezimika.
Kijana akaja na torch.
Nikamwambia Mungu, wewe wajua hizi funguo nilipozidondosha, naomba uniongoze nizipate, nikamuweka Kijana Mbele na torch Mimi nyuma kwenda katika Manyasi nilipokuwa nakagua shamba, kufika katikati nikahisi nimeona kitu cheusi,akili ya mwanzo ikaniambia ni kinyesi cha Ng'ombe tu,nikapiga hatua kuendelea, lakini kuna kitu kikaniambia hebu rudi hatua moja nyuma uangalie vizuri.
Kurudi that was the Car Key
Lile tukio ni dogo ila liliiikuza sana Imani.
yangu juu ya uwezo wa Mungu.
Rest in Peace my Bi Mkubwa, Shamba nililonunua kwa ajili yako wala hukulifaidi
Hapo mwisho ulivomalizia mkuu, hakika ni huzuni kubwa sana, apumzike mahala Pema peponi mama
 
Zaburi 51 ukiisoma kwa imani ni toba na utajikuta unamuomba Mungu msamaha na kutaja makosa yako yote
Cha kukusaidia tafuta nyimbo za kuabudu wkt unaomba ziwe zinaimba taratibu kusukuma maombi yako,jifunze kuinenea sadaka yako kbl haujaitoa
Sante sana mkuu, barikiwa
 
Kabla ya kuomba hakikisha umetakasika hauna makando kando,jitakase kwa kuomba sala ya toba ili usamehewe dhambi zake, hata kama wewe kwa macho ya nyama hauzioni dhambi zako ila usijihesabie haki, pia kumbuka maombi mengine hayawezekani mpaka kwa kufunga na kuomba, kumbuka kufunga ni muhimu, na usisahau nguvu ya sadaki toa sadaka kubwa kwa mama wajane na hata kwa watoto yatima au kanisani, ndugu yangu kupitia haya tatizo lako ni kidogo sana kwa jehova.
Not really!
You need to be focused and plan well your prayer!
The prayer has to be the desire of your heart.
In order to align well with your heart desire-You need to consult your spirit...here some people fast and others meditate.

That is what people refers to as clingsin or purification of sins-You can get there if you have practiced your inner most communication.

At all times-You can pray;you can ask whatever you want from God-it doesn't matter what you have done or at which situation you are!Don't postpone prayers because perhaps you were in a situation you refer it as sin-God is there-Talk to him right there aiming at change anyway!

People take time to resume spirituality simply because they feel like dirty and denied by GOD-NO.
Talk to God right there especially at times you think that you have wronged!
Smile or converse with God as far as your closest but best friend!

No other friend is so dear than God.

At the bottom line-He is LOVE itself.
 
Back
Top Bottom