Mambo ambayo Wanaume hawapaswi kutuma kama ujumbe kwa Mwanamke

Kambi ya Fisi

JF-Expert Member
Feb 3, 2018
13,525
22,015
Kwa wale wanaume ambao hamjaoa, bila kujali hisia zako kwa msichana, kamwe usitume emoji za matango na ndizi. Jiheshimu na umheshimu msichana wako. Kuna zaidi ya upendo na maisha kuliko hamu yako ya ngono.

Acha kujipiga na kumtumia selfies ambazo hujakuomba -hivi unauza sura?

Epuka pia, kumtumia SMS usiku saa ya kulala - yeye si kidonge chako cha usingizi.

Kwa wanaume waliooa, epuka jibu la neno moja kama 'sawa' au, 'p'

Kamwe usimtumie maneno kama haya, "Kwa nini hunijibu?" Maneno kama hayo huwakilisha kiburi, ubabe na uonevu. Inaweza kuwa ana shughuli nyingi. Na Inawezekana pia akasahau kujibu. Isitoshe, ana haki ya kutojibu. Tambua kuwa wewe si bosi wake - wewe ni mshirika wake - kiongozi wa timu yake - na mpenzi wake kwa ridhaa ya pande zote - sio kwa kulazimishwa.

Usimtumie mkeo ujumbe kama huu, "Una uhakika?" Au, “Huyo jamaa ni nani?” Tambua kuwa kutokuaminiana kunavunja msingi wa ndoa. Shughulikia masuala yenu nyeti kwa kuongea na mkeo ana kwa ana, akiwa ameketi kwenye mapaja yako mkiwa chumba cha kulala.

Kamwe usijaribu kuelezea mahaba yenu kwa njia ya maandishi - ni sawa kumshukuru kwa mtanange wa usiku uliopita, mshukuru ukiwa naye huko huko chumbani na sio kumwandikia SMS baadae - Kumbuka watoto huchagua simu ya mama yao ili wacheze game - haitakiwi mtoto wako asome jinsi unavyosokota na kumviringisha mama yake.

Ubarikiwe
 
Huyu Jamaa kwani anawachukuliaje wanawake wa sasa? Anafikiri ndio wa zamani ? Saa hii ukimuuliza una uhakika anakuuliza maswali gani hayo sasa
Pole sana mkuu kama unapambana na wanawake wa kisasa, Ila wewe waweza kuwa kisababishi cha matatizo na mwanamke wako.
 
Kwa wale wanaume ambao hamjaoa, bila kujali hisia zako kwa msichana, kamwe usitume emoji za matango na ndizi. Jiheshimu na umheshimu msichana wako. Kuna zaidi ya upendo na maisha kuliko hamu yako ya ngono.

Acha kujipiga na kumtumia selfies ambazo hujakuomba -hivi unauza sura?

Epuka pia, kumtumia SMS usiku saa ya kulala - yeye si kidonge chako cha usingizi.

Kwa wanaume waliooa, epuka jibu la neno moja kama 'sawa' au, 'p'

Kamwe usimtumie maneno kama haya, "Kwa nini hunijibu?" Maneno kama hayo huwakilisha kiburi, ubabe na uonevu. Inaweza kuwa ana shughuli nyingi. Na Inawezekana pia akasahau kujibu. Isitoshe, ana haki ya kutojibu. Tambua kuwa wewe si bosi wake - wewe ni mshirika wake - kiongozi wa timu yake - na mpenzi wake kwa ridhaa ya pande zote - sio kwa kulazimishwa.

Usimtumie mkeo ujumbe kama huu, "Una uhakika?" Au, “Huyo jamaa ni nani?” Tambua kuwa kutokuaminiana kunavunja msingi wa ndoa. Shughulikia masuala yenu nyeti kwa kuongea na mkeo ana kwa ana, akiwa ameketi kwenye mapaja yako mkiwa chumba cha kulala.

Kamwe usijaribu kuelezea mahaba yenu kwa njia ya maandishi - ni sawa kumshukuru kwa mtanange wa usiku uliopita, mshukuru ukiwa naye huko huko chumbani na sio kumwandikia SMS baadae - Kumbuka watoto huchagua simu ya mama yao ili wacheze game - haitakiwi mtoto wako asome jinsi unavyosokota na kumviringisha mama yake.

Ubarikiwe
usitupangie
cha muhimu usiige style ya familia nyingine ukataka kuhamishia kwako, utafail
 
Back
Top Bottom