Nunua Kitabu cha Kiswahili cha maisha ya Beyonce na Jay Z, kinapatikana kwa Tshs 10,000 tu

Kabota

Member
Aug 15, 2009
63
10
Kitabu kipya cha maisha ya Beyonce na Jay Z kimeingia mtaani. Ni kitabu kilichoandikwa kwa kina kuhusu maisha ya wanandoa hawa maarufu duniani. Kina kurasa 100, picha za kuvutia na historia zao zimeandikwa kwa ufasaha sana. Kinauzwa kwa shilingi 10,000 tu. Unaweza kuletewa ulipo popote Dar na utalipa 15,000. Tuma sms/whatsapp namba 0766173514

nunua-kitabu-cha-kiswahili-cha-maisha-ya-beyonce-na-jay-z-kwa-10000-tu_i383911


MAELEZO ZAIDI KUHUSU KITABU

Maisha, Mapenzi na Maumivu ni vitabu vinavyoyaangaza maisha ya mastaa wakubwa duniani ambao macho ya vyombo vya habari yamewafanya waishi maisha yenye faragha hafifu. Hawa ni watu ambao kila siku tumekuwa tukiona habari zao kwenye runinga, tukisikia wanayoyafanya kwenye redio, tukisoma mambo yao kwenye magazeti na mtandaoni na kamwe hatuchoki kutaka kufahamu zaidi mambo ya ndani ya maisha yao kama vile utajiri na maisha ya uhusiano wao au ndoa.

Kitabu cha kwanza cha Maisha, Mapenzi na Maumivu kimeyaangalia maisha ya wanandoa kwenye muziki wenye nguvu zaidi duniani, Shawn Carter maarufu kama Jay Z na Beyoncé Knowles. Kitabu hiki kitakupa undani wa maisha yao, ukubwa wao katika muziki na biashara na uhusiano wao pamoja na maumivu na majaribu waliyoyapitia katika ndoa yao kiasi cha kuwa katika hatari ya kuvunjika. Kitabu hiki kitakufanya uwafahamu Jay Z na Beyoncé kuliko unavyowafahamu sasa.

KUHUSU MWANDISHI WA KITABU HIKI

Fredrick Bundala ni mwandishi wa habari, mtangazaji wa redio na blogger anayeishi jijini Dar es Salaam, Tanzania. Alifahamika zaidi kupitia Radio Free Africa ambako alitangaza vipindi mbalimbali kuanzia mwaka 2006 – 2011. Mwaka 2012 safari yake ya uandishi wa habari za burudani kwenye blog ilianza rasmi. Tangu Septemba, 2012 amekuwa mhariri mkuu wa tovuti ya burudani inayosomwa zaidi nchini Tanzania, bongo5.com.

Ni msomi mwenye shahada ya mawasialiano ya umma (Mass Communication) aliyoipata katika chuo kikuu cha Mtakatifu Agustino (SAUT) kilichoko jijini Mwanza, Tanzania. Mbali na kuandika habari za burudani, amekuwa akiandika makala nyingi zenye mtazamo wenye mlengo chanya katika kuinua kiwanda cha muziki nchini Tanzania, kuongeza uelewa zaidi kwa wapenzi wa burudani ya muziki kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu burudani, kupongeza, kushauri na kukosoa pale inapobidi.

Hivi sasa amejikita pia katika uandishi wa vitabu vya burudani vinavyogusa wasanii wa nje na ndani ya nchi. Hili ni toleo la kwanza la mfululizo wa vitabu vyake.
 
Haijalishi kama wewe ni shabiki wa muziki au la lakini ni wazi kuwa Beyonce ni mtu aliyefanikiwa zaidi kwa sasa duniani na pamoja na kuwa ni Mmarekani, bado mhitimu wa chuo wa Tanzania unaweza kujifunza mengi kutoka kwake iwapo utasoma kitabu changu: Maisha, Mapenzi na Maumivu: Beyonce na Jay Z Kama una ndoto za kufanikiwa, haya ni mambo nane unayoweza kuyaiga kutoka kwa Queen Bey:

1. NI BOSI

Maisha kama mhitimu wa chuo hayatabiriki, lakini ni muda wa kuyaongoza, kwa mfumo kama wa Beyonce. Kuna sababu kwanini anajulikana kama ‘Mfalme’ na ‘Malkia’ kwa wakati mmoja kwenye muziki.

2. NI KINYONGA

Matamanio ya kazi hubadilika kila siku pindi unapoingia ukubwani, hivyo hakikisha unakuwa tayari kwa kila hali. Kama Beyonce, usiogope kuleta kitu kipya mezani, hata kama kwa wengine kitaonekana ni kituko.

3. HUTHUBUTU

Ni kitu gani cha kijasiri kama kuachia albamu bila kutangaza tena kwenye siku ya Ijumaa ambayo kwa wengine huonekana kuwa sio siku ya bahati? Pamoja na hivyo, Bey aliweza kuuza nakala milioni 1.3 ndani ya siku 17. Hivyo kama unataka kuanzisha biashara, usifikirie kuacha kazi unayolipwa mshahara mdogo na kusonga mbele kujiajiri kutumia elimu uliyopata chuoni ili kujitengenezea maisha bora zaidi.

4. HUTUMIA UZOEFU WAKE

Ile ofisi uliyoamua kujitolea katika mwaka wako wa kwanza chuoni au mradi uliouanzisha ulipokuwa sekondari vinaweza kuwa vimepotea kichwani, lakini uzoefu huu unaweza kukufanya uonekane tofauti mbele ya watu wengi wanaotaka kazi moja uitakayo pia.

Pindi Mrs Carter anapotumbuiza show zilizojaza kutoka kwenye albamu yake ya mwaka 2011, unaweza pia kutumia kitu ulichofanya nyuma kama silaha yako ya leo.

5. HUFANYA KAZI KWA BIDII

Siku zote Beyonce huwa hatumbuizi nusu nusu na wewe pia hupaswi kufanya vitu nusu nusu. Unapodhani kuwa umechoka sana kuandika barua yako ya kazi yenye kurasa 10 kwaajili ya kuombea kazi uipendayo, muangalie jinsi Bey anavyoonekana wakati akitumbuiza wimbo wake Single Ladies na jinsi anavyotumia nguvu.

6. ANAJIAMINI

Ni muda wako wa kuanza kujiamini wewe mwenyewe kwasababu kama hujiamini hakuna atakayekuamini. Bey ni mtu anayejiamini na ndiyo maana ana mafanikio makubwa.

7. KUNDI LAKE LA MASHABIKI LIKO NAYE MUDA WOTE

Mashabiki damu damu wa Beyonce wanajulikana kama Beyhive. Kama mtu akimchokoza Bey, kundi hili humshambulia mtu huyu hadi ashike adabu kupitia Twitter, Instagram na Facebook. Sio rahisi kuwa na aina hii ya ushawishi lakini jaribu kutengeneza mtandao wa watu watakaokuunga mkono na wenye ushawishi chanya kwako. Kisha, unapokuja kuwa tajiri na maarufu, utakuwa na kundi imara la kukuunga mkono likikusiburi.

8. HUTUNZA UHUSIANO WA MUDA MREFU NA WATU WA KARIBU

Marafiki zako wa karibu mara nyingi ni muhimu katika mafanikio yako. Kama Beyonce na wanamuziki wenzake wa kundi la Destiny’s Child, tengeneza urafiki na wa muda mrefu na watu muhimu ili siku zote uwe na watu wa kukuangalia na kukushauri panapohitajika.

KITABU HIKI KIMEINGIA SOKONI TAYARI. KINAPATIKANA KWENYE BOOKSHOP ZOTE KUBWA KWA SHILINGI ELFU 10 TU. UKITAKA KULETEWA POPOTE ULIPO UTALIPA SHILINGI 15,000. TUMA SMS/WHATSAPP KWA NAMBA 0766173514 KUJUA ZAIDI
 
Nitapenda tu kujua zaidi ili wengine tujue tunanunua kitu ambacho watajwa wamekubali yaliyoandikwa, yaani sio ya kutungwa. Au kaandika ndani ni wapi kayatoa yaani kopi na pesti au intavyuuu nao?
 
Skywalker huwa namkubali lakini katika hili kafel huo ujanja wa kutukusanyia viarticle mtandaoni haupaswi kuvumiliwa
Ni lini uliwahoji
 
Skywalker huwa namkubali lakini katika hili kafel huo ujanja wa kutukusanyia viarticle mtandaoni haupaswi kuvumiliwa
Ni lini uliwahoji

Mkuu kuna njia nyingi za kufanya research moja wapo ni kutumia vyanzo vingine nk, sio lazima umhoji mtu moja kwa moja. Mfano walioandika historia za Nyerere nk sio wote waliomhoji bali wengi wametumia hotuba zake, maandiko yake, kile alichokifanya, kuhoji wanaomfahamu nk. Ni suala la kawaida sana katika uandishi. Kwahiyo Skywalker hajafeli, almradi yeye kaandika kitu anachoweza kukiandika kwa ufasaha
 
Kwanini msiandike kuhusu maisha ya mastar wenu wa bongo??

Mtawasoma? Si kila siku mnawatukana? Pia inspirations hazitoki kwa watu wa ndani tu. Tanzania ina watu zaidi ya milioni 50, wapo watakaopenda kukisoma, ni wazi wewe sio target audience na haumshtui mwandishi
 
Upmbv gani huu!!! Yaani nianze kufuatilia maisha ya watu wa marekani halafu uko Tanzania
 
Last edited:
Huyu mkali nimemsikia interview yake TBC pale, kitabu inaonekana kimetulia sana
 
Ni vizuri kujifunza kutoka kwa wengine, ila mwandishi sijui kama aliwahusisha wahusika
 
Jamaaa ka google!!!! Kadownload documentary Katafsiri kaongeza rojo rojo kaprint anauza anajipatia mshiko!!! beyonce ajui wala jay z ajui!! Kweli tanza nia shba labibi nami ngoja nije nitoe cha kanye west na kim k!!!
 
Tabia za kuiga au kuchukulia mfano mtu ambae tayari anaishi nchi ilio endelea ni mbaya sana na haita saidia! Ningekuwa naishi Marekani ningesoma na ningeweza kutoboa lakini kwa Tanzania kuchukulia Mfano Marekani ni ufinyu wa akili!

Mwandishi atajitetea lakini huwezi mringanisha maskini wa Marekani na wabongo.....Ugumu wa maisha Alio pitia Jay Z au Beyonce hadi kufanikiwa kutoka Nchi pia imechangia

Angekuwa Jay Z au Beyonce wamekulia Tanzania waka hustle wakatoka Tz na baadae wakaamua kuishi Marekani ningejifunza toka Kwao!

Hapa ndipo waandishi wengi huwa wanashindwa kupambanua Mambo Kumringanisha mtu ambae Nchi yake ipo kwenye G8 lakini Tz hata haijaendelea,nchi amabayo ina wasomi wengi kuliko nchi yetu,nchi ambayo ina uchumi mkubwa kila kitu wametuzidi hata science na technology yao imekua kuliko sisi afu useme utatoboa huo ni uwongo Mkubwa

Kamwe huezi ukatumia njia alizo fanya Jay Z kutoboa ukajifunzia Bongo!
 
Back
Top Bottom