Mambo 7 yanayohusu haki za Zanzibar kwenye Muungano ambayo Kikosi Kazi cha Zanzibar walikubaliana yafanyiwe kazi

Hoja zote zinalenga kuipendelea zanzibar dhidi ya bara, na utashangaa kwa utawala wa sasa ulivyokaa ki zanzibar hoja zinakubalika kama zilivyo. Huu muungano dtuliingia cha kike
 
Nafasi na Uwakilishi wa Zanzibar kwenye Baraza la Mawaziri la Muungano uwekwe wazi ili kuhakikisha taswira halisi ya Muungano wa nchi mbili inaonekana wazi kwenye chombo hicho kikuu kinachosimamia sera na uendeshaji wa Serikali ya Muungano.
... washenzi kweli! Tanganyika haina hata chembe ya uwakilishi upande wa pili wa muungano ila wao wanataka uwakilishi kila mahali hadi nafasi za ajira za Tanganyika! Aliyeanzisha huu muungano kwa ahkika aliiweza Tanganyika!
 
..Vipi kuhusu haki za Tanganyika ndani ya muungano?
... mjitete wenyewe! Wao wanatetea utaifa na haki zao. Kama viongozi wenu hayo sio kitu kwao is up to you! Hizo hoja kwa zaidi ya 100% are all in favor of Zanzibar nothing else!
 
Hoja zote zinalenga kuipendelea zanzibar dhidi ya bara, na utashangaa kwa utawala wa sasa ulivyokaa ki zanzibar hoja zinakubalika kama zilivyo. Huu muungano dtuliingia cha kike
... ila mkiambiwa Katiba Mpya mnang'aka! Watu wa ajabu sana magamba!
 
5. Umiliki wa Zanzibar wa kisiwa cha Fungu Mbaraka (Latham Island) uwekwe wazi kwa kutambua kuwa kisiwa hicho kimekuwa ni sehemu ya mamlaka ya Zanzibar tokea 1898 na hakujawahi kuwa na mzozo wa umiliki huo
Hiki kisiwa kwa sehemu kilipo sijui mpaka wa bahari kati ya Bara na Zanzibar utakuaje maana automatic Dar es Salaam itapoteza direct access ya bahari kuu
 
1. Kuundwa kwa Tume ya Pamoja ya Fedha na kuanzishwa kwa Akaunti ya Pamoja ya Fedha kwa mujibu wa Katiba ya Muungano ili mapato na matumizi ya Muungano yawe wazi.
2. Gawio la Zanzibar kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BOT) lizingatie hisa za Zanzibar zilizotoka Bodi ya Sarafu ya Afrika Mashariki (EACB) wakati wa uanzishwaji wa Benki Kuu hiyo ambazo ni 11.02% badala ya 4.5% inayotumika sasa. Asilimia hiyo pia itumike katika misaada na mikopo.
3. Pamoja na Ushuru wa Forodha, Ushuru wa Bidhaa na Kodi ya Mapato kuwa suala la Muungano, mfumo na viwango vya kodi vizingatie uchumi wa Zanzibar ambao ni uchumi wa huduma (service economy) ulio tofauti na uchumi wa Bara ambao unategemea rasilimali (resource based economy).
4. Mipaka ya Bahari kati ya Zanzibar na Tanganyika iwekwe na itambuliwe wazi ili kujua eneo la utawala la kila upande na pia kuepusha uwezekano wa mivutano katika kufaidi rasilimali hasa katika maeneo yasiyo ya Muungano.
5. Umiliki wa Zanzibar wa kisiwa cha Fungu Mbaraka (Latham Island) uwekwe wazi kwa kutambua kuwa kisiwa hicho kimekuwa ni sehemu ya mamlaka ya Zanzibar tokea 1898 na hakujawahi kuwa na mzozo wa umiliki huo.
6. Suala la Mafuta na Gesi Asilia likamilishwe kuondolewa kwenye orodha ya mambo ya Muungano ndani ya Katiba ya Muungano ili Zanzibar iweze kusimamia kikamilifu sekta hiyo badala ya hali iliopo sasa ambapo mamlaka iliyopewa Zanzibar yametoka kwenye Sheria ya Bunge.
7. Nafasi na Uwakilishi wa Zanzibar kwenye Baraza la Mawaziri la Muungano uwekwe wazi ili kuhakikisha taswira halisi ya Muungano wa nchi mbili inaonekana wazi kwenye chombo hicho kikuu kinachosimamia sera na uendeshaji wa Serikali ya Muungano.

Kwa ajili ya kukusaidia tu kidogo, Tume ya Pamoja ya Fedha iliajiri kampuni kubwa ya kimataifa ya ukaguzi (PriceWaterhouseCoopers) kufanya kazi hiyo na kutoa Ripoti ambapo ukiona mahesabu waliyoyagundua unaweza ukakimbia na hii hoja yako.
Kila kitu kiwe wazi ,sio Zanzibar wapate gawio tu,tunataka tujue kila mwezi upande wa Zanzibar na Tanganyika wamechangia shilingi ngapi .
Ili Zanzibar wakichukua gawio tujue ni haki yao .na sisi tujue ni haki yetu.
Kuhusu hizo hoja zote; kuanzia Benki kuu hazina mashiko hata kidogo.
Zanzibar na wao walipe kila kitu toka uhuru walichotumia kwenye mambo yote ya muungano kuanzia Ulinzi na vingine vyote.
 
Kimahesabu Lazima Jibu la msingi lipatikane kwanza ili iwe rahisi kukamilisha vipengele vyote vyenye changamoto ndani ya Muungano.:
1.Muungano ni baina ya Tanganyika na Zanzibar.Zanzibar inaendelea kudai haki zaidi,huku Tanganyika ikiwa imemezwa.Kuna umuhimu wa kuangalia aina ya Muungano.
2.Muungano ubainishe nafasi ya nchi zilizounda Muungano (Zanzibar na Tanganyika).
3.Mtizamo wa "Chako ni Chetu(cha wote) ,"Changu ni Changu" itatuchelewesha sana kuondoa kasoro zilizopo.
Kwani kuna baadhi ya vitu mwananchi wa bara(Tanganyika) hana haki,lakini mwananchi wa visiwani (Zanzibar)ana haki.
4.Mbinu zile zile za enzi hizoo,Tutajikuta Zanzibar ina zalisha nchi iitwayo Pemba.
Maana tuienda kwa "HAKI",kesho Muungano hautakuwepo,bali inakuja "Zanzibara" na "Zanzibar" na hatimaye "Mimi ni wa Unguja na sisi ni Wapemba.
Hii inaenda pole pole,Ilidaiwa Bendera,wakapewa Bendera;Ilidaiwa wimbo wa Taifa,wakepewa wimbo wa Taifa.
Likaletwa swali la mtego,"Zanzibar ni nchi au sio nchi?!
Ikatafutwa mbinu nyingine kwenda kuomba wanachama umoja wa Mataifa,bado haikutosha jaribio kupitia Micheal wa mpira wa miguu(kuomba wanachama wa Shirikisho la Mpira Afrika).
Kwa mtazamo wa mtiririko wa matukio ipo siku vizazi vijavyo vitakuja na Ufumbuzi wa kero za Muungano,kwa sasa Wanasiasa watengeneza maisha yao ya kisiasa.
Chama cha ccm kimejaa mafii kichwani viongozi mazwazwa wasio na chembe ya akili ndiyo wanaendesha huu muungano ...ukweli muungano ni lazima uvunjike ili kila pande wapate haki na heshima
 
1. Kuundwa kwa Tume ya Pamoja ya Fedha na kuanzishwa kwa Akaunti ya Pamoja ya Fedha kwa mujibu wa Katiba ya Muungano ili mapato na matumizi ya Muungano yawe wazi.

2. Gawio la Zanzibar kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BOT) lizingatie hisa za Zanzibar zilizotoka Bodi ya Sarafu ya Afrika Mashariki (EACB) wakati wa uanzishwaji wa Benki Kuu hiyo ambazo ni 11.02% badala ya 4.5% inayotumika sasa. Asilimia hiyo pia itumike katika misaada na mikopo.

3. Pamoja na Ushuru wa Forodha, Ushuru wa Bidhaa na Kodi ya Mapato kuwa suala la Muungano, mfumo na viwango vya kodi vizingatie uchumi wa Zanzibar ambao ni uchumi wa huduma (service economy) ulio tofauti na uchumi wa Bara ambao unategemea rasilimali (resource based economy).

4. Mipaka ya Bahari kati ya Zanzibar na Tanganyika iwekwe na itambuliwe wazi ili kujua eneo la utawala la kila upande na pia kuepusha uwezekano wa mivutano katika kufaidi rasilimali hasa katika maeneo yasiyo ya Muungano.

5. Umiliki wa Zanzibar wa kisiwa cha Fungu Mbaraka (Latham Island) uwekwe wazi kwa kutambua kuwa kisiwa hicho kimekuwa ni sehemu ya mamlaka ya Zanzibar tokea 1898 na hakujawahi kuwa na mzozo wa umiliki huo.

6. Suala la Mafuta na Gesi Asilia likamilishwe kuondolewa kwenye orodha ya mambo ya Muungano ndani ya Katiba ya Muungano ili Zanzibar iweze kusimamia kikamilifu sekta hiyo badala ya hali iliopo sasa ambapo mamlaka iliyopewa Zanzibar yametoka kwenye Sheria ya Bunge.

7. Nafasi na Uwakilishi wa Zanzibar kwenye Baraza la Mawaziri la Muungano uwekwe wazi ili kuhakikisha taswira halisi ya Muungano wa nchi mbili inaonekana wazi kwenye chombo hicho kikuu kinachosimamia sera na uendeshaji wa Serikali ya Muungano.
Nilisahau jambo moja muhimu sana lililowekwa

SHARED SOVEREIGNTY: Kuwapo kwa sheria inayotafsiri kwamba Mamlaka ya KiDola ya Jamhuri ya Muungano ni ya pamoja (shared sovereignty) kati ya #Tanganyika na #Zanzibar na katika sheria hiyo ielezwe kila upande una haki SAWA ya kuitumia.
 
Back
Top Bottom