aleesha
JF-Expert Member
- Oct 17, 2016
- 768
- 1,104
1. Kuundwa kwa Tume ya Pamoja ya Fedha na kuanzishwa kwa Akaunti ya Pamoja ya Fedha kwa mujibu wa Katiba ya Muungano ili mapato na matumizi ya Muungano yawe wazi.
2. Gawio la Zanzibar kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BOT) lizingatie hisa za Zanzibar zilizotoka Bodi ya Sarafu ya Afrika Mashariki (EACB) wakati wa uanzishwaji wa Benki Kuu hiyo ambazo ni 11.02% badala ya 4.5% inayotumika sasa. Asilimia hiyo pia itumike katika misaada na mikopo.
3. Pamoja na Ushuru wa Forodha, Ushuru wa Bidhaa na Kodi ya Mapato kuwa suala la Muungano, mfumo na viwango vya kodi vizingatie uchumi wa Zanzibar ambao ni uchumi wa huduma (service economy) ulio tofauti na uchumi wa Bara ambao unategemea rasilimali (resource based economy).
4. Mipaka ya Bahari kati ya Zanzibar na Tanganyika iwekwe na itambuliwe wazi ili kujua eneo la utawala la kila upande na pia kuepusha uwezekano wa mivutano katika kufaidi rasilimali hasa katika maeneo yasiyo ya Muungano.
5. Umiliki wa Zanzibar wa kisiwa cha Fungu Mbaraka (Latham Island) uwekwe wazi kwa kutambua kuwa kisiwa hicho kimekuwa ni sehemu ya mamlaka ya Zanzibar tokea 1898 na hakujawahi kuwa na mzozo wa umiliki huo.
6. Suala la Mafuta na Gesi Asilia likamilishwe kuondolewa kwenye orodha ya mambo ya Muungano ndani ya Katiba ya Muungano ili Zanzibar iweze kusimamia kikamilifu sekta hiyo badala ya hali iliopo sasa ambapo mamlaka iliyopewa Zanzibar yametoka kwenye Sheria ya Bunge.
7. Nafasi na Uwakilishi wa Zanzibar kwenye Baraza la Mawaziri la Muungano uwekwe wazi ili kuhakikisha taswira halisi ya Muungano wa nchi mbili inaonekana wazi kwenye chombo hicho kikuu kinachosimamia sera na uendeshaji wa Serikali ya Muungano.