Mambo 7 mabaya usiyoyajua kuhusu mifuko ya Pensheni Tanzania

Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Nov 28, 2013
10,129
35,148
Haya ni mambo muhimu 7 mabaya usiyoyajua kuhusu Mifuko ya Pensheni (Mafao) hapa Tanzania. Ni sehemu ya maelezo kutoka kwa baadhi ya wakurugenzi katika mifuko hiyo.

1/Inaendeshwa kwa mtindo wa UPATU (Yaani Michango ya wanachama wake wa sasa ndio inatumika kulipa mafao ya mstaafu wa Leo. Kasheshe ni pale wanachama wake wengi wakijitoa mara moja..)

2/Mwisho wa siku mifuko yote ITAFIRISIKA. (Katika hilo hakuna ujanja, ni jambo la kiasili na kihistoria, lipo tu na limeshatokea sana duniani, kinachofanyika ni kusukuma siku tu ili kizazi kingine kifie nalo..)

3/Mifuko yote inaendeshwa kwa msukumo wa KISIASA zaidi na sio kiuchumi. (Mwenendo wa mifuko hiyo iko kuwaridhisha wanasiasa wakuu ndani ya serikali kwa sababu watendaji wake wote wa juu wanateuliwa kisiasa zaidi)

4/Mifuko yote ni AKIBA ya dharula ya serikali (Wakati wowote serikali inaweza kuamuru kutumia mitaji ya kifedha ya mifuko hiyo ili kukidhi mahitaji ya uendeshaji wa miradi na mipango ya kiserikali)

5/Miradi yake mingi imewekezwa kwa HASARA.
(Mifuko hii ndio inayoongozwa kuwekeza kwenye miradi mingi isiyokuwa na faida ya maana kibiashara, mingi ya miradi yake ni ili kulinda mtaji tu)

6/Inaendeshwa kwa GHARAMA kubwa sana.
(Mifuko hii imeajiri watumishi wengi sana, ina kurugenzi nyingi sana, ina matumizi makubwa sana huku mengine yakiwa ni matumizi ya Anasa. Gharama za uendeshaji wa mifuko hii ni zaidi ya Faida inayoweza kupatikana katika miradi yake)

7/Mifuko hii haifanani katika kulipa MAFAO.
(Kila mfuko unatumia kanuni yake, kanuni nyingine zinapunja na kanuni nyingine zinalipa vizuri, kanuni hizi sio za kudumu milele, ziliwahi kubadilika, zinabadilika na zitabadilika kufuatana na msukumo kutoka kwa wanasiasa nk).

*UJUMBE.
Wafanyakazi walioajiriwa wajipange namna bora ya kuishi kwa kuweka Akiba ya Mali na Pesa binafsi wakati wakiwa bado wanafanyakazi, suala la kungojea Mafao ya Kustaafu kutoka kwenye mifuko ya Pensheni ili wafanikishe mambo yao huko baadaye ni hatari sana hasa hasa kwa kipindi hichi na huko tunapoelekea.
 
Wafanyakazi, tuwekeni kwenye mindset zetu kwamba pesa inayokatwa kwenye mifuko hiyo ni kama kodi nyingine tu wala msiziwazie.
Mishahara tunayo ipata tuwekeza kwenye miradi na akiba zetu binafsi.
Mifuko hii ilipofikia hamna jinsi, tayari tupo kibla
 
Naona unaniongezea machungu maana nikimuona waziri akisoma mswada natamani nimrukie na kumnyang'anya makaratasi kama alivyofanya Dr.Kamani kwa msimamizi wa uchaguzi.
 
Wafanyakazi, tuwekeni kwenye mindset zetu kwamba pesa inayokatwa kwenye mifuko hiyo ni kama kodi nyingine tu wala msiziwazie.
Mishahara tunayo ipata tuwekeza kwenye miradi na akiba zetu binafsi.
Mifuko hii ilipofikia hamna jinsi, tayari tupo kibla
Yap, hii ni aina nyingine ya kodi
 
Kama walivyokimbia kukanusha kujiuzulu kwa MR kwa taarifa ya mtandaoni waje wakanushe na hii ya kuwa mifuko ya jamii ni Upatu wa wanasiasa kama DECI
 
Mtoa mada nadhani watakuwa wamekuelewa kupanga ni kuchagua, wakati unakatwa hela yako kwenda huko kwenye mfuko na wewe tengeneza mfuko wako mwingine binafsi au kakibubu flani hivi uwe unajikata tena unaweka huwezi kujua huko mbeleni nini kitatokea wakati wa kustaafu unaeza hata kuambiwa faili lako hatulioni au mwajiri alikuwa haleti mchango, (Mungu aliumba dunia na maajabu yake) NAWAZA TU DONT TAKE IT SERIOUSLY
 
Back
Top Bottom