Mambo 30 yanayokuonesha kuwa sasa umri umekutupa mkono

Kishoka1

Member
Joined
Apr 27, 2024
Posts
8
Reaction score
54
1. Huna muda wa kushinda na mpenzi wako kutwa nzima mkipiga stori za mapenzi

2. Ukihitaji kufanya mapenzi mahali unakokufikiria ni kitandani

3. Unaanza kujaza friji lako kwa vyakula zaidi kuliko pombe

4. Muziki unaoupenda unausikia ukiwa kwenye lifti ama kwenye gari lako ukienda na kutoka kazini

5. Saa 11 alfajiri ndiyo muda unaoamka, na siyo muda tena unaorudi kulala

6. Unatazama taarifa ya habari hadi utabiri wa hali ya hewa

7. Rafiki zako wanakualika zaidi kwenye vikao vya harusi kuliko mtoko wa kwenda Maisha Club

8. Ukienda dukani kununua kitu unakuwa na juhudi sana ya kuomba upunguziwe bei

9. Idadi ya tisheti na jinsi inapungua kwa kasi kwenye kabati lako la nguo

10.Wewe ndiyo unayekumbuka kuwapigia simu polisi endapo mtaani kwenu kuna vijana wavuta bangi wanaowasumbua

11. Ndugu zako watu wazima wanajisikia kawaida tu kufanya utani wa kiutu uzima mbele yako

12. Hukumbuki tena Azam Ice Cream na Samaki Samaki wanafunga saa ngapi

13. Timu yako ya mpira ikifungwa hutaki tena kutaniwa na watu

14. Wanyama uwapendao kama mbwa na paka unawaandalia chakula kwa kanuni za kisayansi badala ya kuwapa mabaki uliyotoka nayo Subway ama Steers

15. Ukilala kwenye kochi unaamka mgongo unakuuma sana

16. Unaithamini sana ratiba yako ya kulala

17. Ukiwa nyumbani unaanza kutumia muda wako wa ziada kulima lima bustani ya maua ama mbogamboga badala ya kutazama filamu na kuzurura

18. Kila kitu kikinunuliwa nyumbani jambo la kwanza unalouliza, "Umenunua sh' ngapi?"

19. Unakwenda duka la madawa kununua Ibuprofen na Antacid, siyo kondomu tena wala kipima mimba

20. Unaanza kununua magazeti ya Mwananchi, The Express, Citizen na Nipashe badala ya Uwazi, Ijumaa, Kiu na Amani

21. Unapata kifungua kinywa kwa wakati

22. Ukiwa baa unanunua bia unazohitaji wewe badala ya kusema "zungusha kama tulivyo"

23. Asilimia 90 ya muda unaoutumia kwenye kompyuta yako unautumia kufanya kazi badala ya kuchati

24. Ukijisikia hamu ya kunywa kilevi unaanza kunywea nyumbani ili kupunguza gharama kabla hujaenda baa

25. Ukimwona rafiki yako yu mjamzito unampongeza sana badala ya kumwuliza, "imekuwaje tena?"

26. Ukienda kutembea mahali unaulizia bei za viwanja

27. Hupendi tena kuwaazimisha marafiki zako magari yako

28. Ukiwa na rafiki zako unapenda kujadiliana nao kuhusiana na mfumuko wa bei na mfumo mbovu wa utawala

29. Ukiwa unakula chakula unakuwa mkali ikitokea chakula kimewekwa mafuta mengi ama chumvi nyingi

30. Ukimaliza kusoma kanuni hizo 29 hapo juu unaanza kuhesabu ambazo unaingia wewe.

Ukiona una nusu ya sifa hizi 30 basi huhitaji kupigiwa kengele kukumbushwa kuwa umri ushayoyoma..-...!!!
Utu uzima uambatana na lawama za ovyo ovyo sana na manung'uniko sasa tuvumiliane 😊😊
 
Kwa 89.9% umesema kweli kiasi chake ongeza hujali watu watahoji umevaa nini, unaenda wapi au unatoka wapi kufanya nini lini na muda gani hio inabakia upande wako in short kila unachokifanya kinakua juu yako yaan hakiwahusu wao lastly unaanza kufikiria jinsi ukifa unazikwa peke yako hakuna atakaekubari kuzikwa na wewe awe ndugu, mtoto, jamaa, rafiki au jirani
 
Kwa wale waliofika 40yrs na kuendelea ni muhimu sana kuwa na mashine ya kupima mapigo ya moyo (BP machine) na note book au app ya simu. Kucheki uzima wa moyo, uwingi cholesterol na sukari mwilini walau mara 2 kwa mwaka
 
Hili la kusikiliza na kuangalia taarifa ya habari hadi hali ya hewa na kusoma magazeti makubwa wengine tulipenda tangu tukiwa watoto wadogo wa shule ya msingi hadi utu uzima bado tunapenda mambo hayo. Kama kuna vijana hawafuatilii taarifa ya habari na kusoma magazeti basi wana IQ ndogo
 
Orodha hii kuna mambo kama hukuyapenda na kuyafanya utotoni basi hata ukiwa mtu mzima hutayapenda na kuyafanya kwa kuwa huna historia nayo, hukuwa na interest nayo. Hapa nakupa 20% ya ukweli, kwani mambo mengine inabidi tu uachane nayo kutokana na majukumu ya utu uzima na kubadili interest, ila kuna mengine utazeeka nayo mpaka unakufa still unayependa
 
Kilichonifanya nijue umri umenitupa ni kama mambo 5 hivi.
1. Shikamoo nyingi hata kwa watu ambao nawaona ni wakubwa, na hawapaswi kunipa shikamoo.
2. Magonjwa ya tabia. Uric acid, kisukari, pressure nk
3. Madaktari wanaonitibu. Ni wadogo sawa na wanangu kabisa.
4. Sina tena wivu kwa mwenza wangu
5. Narudi mapema nyumbani. Saa 1 usiku nisharudi nyumbani.
 
Kiufupi wewe ni mlevi

Back
Top Bottom