Mambo 10 Niliyoyaona Simba Ikidhalilishwa kwa Mara ya Tano Mfululizo na Yanga

Soka Ndio Maisha Yangu

Senior Member
Joined
Nov 27, 2024
Posts
110
Reaction score
377
1. Kuna utofauti mkubwa sana baina ya Yanga vs Simba upande wa menejimenti, Yanga waliona wampe timu GSM awape furaha, GSM ndio anasajili wachezaji na kila jambo wanalisimamia wao, Simba kule Mo Dewji anaongoza, Mangungu anaongoza, kale kadada CEO kanaongoza kwa remote kutoka kwa friends of Simba, Try again anaongoza, Azim Dewji anaongoza basi vurugu tu

2. Usajili wa Yanga unafanywa na Hersi mwenyewe, Simba usajili unafanywa na watu kati, ukifuatilia kila mtu pale kaleta mchezaji ndio maana nguvu kubwa inatumika kutuaminisha uwezo wa Mutale

3. Yanga hawana migogoro baada ya kukubaliana timu kumuachia Hersi na GSM, ukimuondoa Mzee Magoma Yanga wana Umoja sana ss hv, Simba Umoja bado sana, kuna kundi lililoshindwa uchaguzi si ajabu hata mechi ya leo wamepigisha shoti uongozi ili Mangungu aonekane hafai

4 Simba Yakut’a Wakili kWa sababu weng wanaendesha maisha kupitia timu hiyo ndio maana wanaletwa akina Ahoua, Nouma, Chamou na wengine mliowaona leo

5 Mashabiki wa Yanga tofauti na Simba, Simba kuna chawa wengi sana, chawa hawa wamekuja Simba juzi tu Leo wanaonekana wafia timu

6 Kuna kitu kwenye biashara tunakiita Trade Secret, taasisi ili iweze kuwa bora na kuachieve competitive advantage lazima iwe na trade secret, Yanga wana Trade secret kuliko Simba, wanaendesha mambo yao kisomi sana na siri zao za ndani na nje hazivuji, Simba walikuwa na mkakati mzuri sana kuwahadaa Yanga kuwa hawachezi lkn wameharibiwa na maadui zao ambao walikuwa wakitoa taarifa kwa watu wa Yanga kuwa timu itakuja uwanjani, Yanga walikuwa wanajua kila kilichokuwa kinafanywa na simba kuelekea mchezo wa leo

7 Quality ya wachezaji pia ni mbingu na ardhi, wachezaji Kama Chamou, Nouma, Che Malone, Ngoma, Okajepha, Mutale, Mukwala hata warudiane mara alfu moja hawawezi kuifunga Yanga, never

8. Timu nzuri inajengwa na viongozi wazuri, Simba haina watu wa mpira ss hv, ukiwakosoa wanakupeleka polisi, wanakuzuia usije uwanjani, wanakuvua uanachama, wanakutenga nk

9. Mo Dewji abadilike, tabia zake za kususa susa zinakera sana, Simba inaweza kusurvive bila yeye

10. Tabia ya kuchukia wachezaji na kuwabagua imevunja morali ndani ya Simba, wachezaji Kama Kijiri, Chasambi, Balua wanawekwa benchi bila sababu za msingi kwa sababu tu ya chuki, kupishana na viongozi, anacheza Duchu eti Kijiri anakaa benchi

11. Kocha Fahdu ni kocha wa kufundisha KMC na aina ya timu Kama hizo, Simba kufika fainal shirikisho sio kigezo cha yeye ni bora, hakuna mafanikio yoyote zaidi ya final ya CAF yenye timu nyingi dhaifu, hana mbinu zozote Fahdu, yaan Leo nilipoona Ngoma katikati, Mukwala na Mutale wameanza wala ckutaka kujitia presha, nilijua tunagongwa t

12. Hakuna msimu wa ligi uliowahi kupita bila viongozi wa Simba kugombana, kila msimu lazima wagombane timu ipigishwe shoti ndio maisha yaendelee.Kabla ya kucheza na Yanga tulisikia watu wakigombana had mdhamin kasusa kisa hakuitwa Dodoma kwa mama wakaenda akina Hassanoo.

13. Mashabiki wa Simba tumeumia sanaaaaa leo, mara ya 5 mfululizo tunafungwa halafu hawajibiki mtu, watu wanaendelea na mambo Kama kawaida, leo wanaolalamika ni mashabiki na wanachama tu lakini viongozi mmepotea mmetuachia msiba.

14. Kama msimu ujao mnajenga tena timu na akina Ahoua, Ngoma na Chamou tujiandae kula mabao 10

15. Uwanja wa Bunju hatujawahi kuweka camp tukamfunga Yanga, tumejitahid sare, uwanja ule nje kuna majirani kibao nje ya fensi wanashabikia Yanga, tumesema lkn hamtuelewi

Kila la Heri Msimu Ujao, Mungu awabariki sana wasaliti wote ndani ya timu yetu, haşa wewe unayeenda kugombea ubunge.
 
Simba tatizo ni management na mashabiki mbumbumbu
We fikiria huwa wanagoma kukiri kama YANGA ana quality wao kila siku eti GSM anaharibu ligi, ila wao wakija wanapigwa kama Ngoma
Si ndio umbumbumbu wenyewe huo ,halafu hawaoni...na hata ktk huu uzi atakuja mbumbumbu kujibu umbumbumbu
 
Kuendesha timu ni gharama, hata GSM anajikaza tu. Fikiria unatoa. 700M kumsajili na kumlipa Chama kwa msimu mmoja tu, inahitaji moyo na sio ushuhaa wa keyboard
 
Mashabiki wengi wa simba unavyowasikiliza unagundua kama vile mtu kachukuliwa halafu ashangilie kitu ambacho hakijui ye anashangilia tu hajui yeye ni shabiki wa nn Simba ilikusanya mashabiki wengi kipindi kile simba inafanya vizuri ilibeba mamba na kenge unakuta mtu anabishana kuhusu mpira hizo point anazotoa mpaka unaionea huruma familia yake kwa kuwa na mtu kama huyo
 
Msema kweli ni kipenzi cha mwenyezi Mungu!
 
Hahaha...

Mambo ya before and after ni tofauti kabisaaaaa...

Kabla ya game Simba walikuwa wanapiga kelele sana za kubeba ndoo hadi kuwatumia manabii sijui kina Suguye...

Msimu umeisha ndoo pekee Simba kabeba ni ndoo ya rangi na malalamiko kibao...
 
Simba ni mbovu toka ligi inaanza.Kuanzia menegment hadi kwawachezaji haiko vizurii.Ni timu iliyowekeza sana kwenye propaganda za mdomo kuliko kutengeneza timu yenye ushindani inayoonekana ikibadilika ukuaji.ISRAEL MWENDA amekua kiwango kaiacha simba iko vile vile.Pengo la CHAMA bado liko vile vile pamoja na timu kua inapata matokeo.Imekua ni timu yakutegemea juhudi za mchezaji mmoja mmoja badala yakucheza kitimu.Viongozi wanasema wanajenga timu isiyoonekana ikijengeka.
 
Simba tatizo ni management na mashabiki mbumbumbu
We fikiria huwa wanagoma kukiri kama YANGA ana quality wao kila siku eti GSM anaharibu ligi, ila wao wakija wanapigwa kama Ngoma
Oya kushinda mmeshinda na hongereni kwa hilo. Ila suala la kulazimisha eti Mashabiki wa Simba wakiri sijui Yanga ina quality HILO HALIPO. Wewe ulionao lini Iran, Urusi au China ikakiri uwezo wa Marekani? Au ulionao lini Israeli, Uingereza,na Marekani wamekiri uwezo wa hizo nchi nilizozitaja?

Au nikuulize swali jingine. Wakati Simba ikifanya vyema ikiwa na akina Chama na Miquissine wa kwanza, au ile Simba ya akina Okwi iliyompiga Yanga 5-0. Ni lini wewe binafsi ulikiri kuwa Simba hizo zilikuwa bora kwa Yanga?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…