Mambo 10 niliyojifunza katika mikutano ya Tundu Lissu ya kutafuta wadhamini

Nov 27, 2019
35
145
Yafuatayo ni mambo kumi ambayo nimeyaona katika ziara ya LISSU ya kutafuta Wadhamini:

1. LISSU anatumia muda mwingi kushambulia haiba za wagombea anaochuana nao kuliko kueleza sera mbadala alizonazo.

2. Wanachama wengi waliojitokeza katika mikutano yake wakienda kutazama majeraha aliyonayo na sio kusikiliza sera zake.

3. LISSU ameonesha kuwa ni mtu mwenye jazba, kisasi hivyo akipewa Mamlaka makubwa ya kuongoza nchi atatumia muda mwingi kufanya visasi badala ya kuleta maendeleo.

4. LISSU anafanya makosa ya kiufundi kwa kuzishambulia taasisi za Serikali mathalani vyombo vya ulinzi na Usalama bila kujali zina mchango mkubwa wa kumfanya ashinde au la.

5. Idadi kubwa ya watu waliojitokeza kwenye mikutano yake ni wanachama wa CHADEMA jambo linaloleta taswira kwamba nje ya chama hicho hakubaliki.

6. Kuna viashiria vya kutosha kwamba LISSU anatumika na mataifa ya nje. Anatumia muda mwingi kuonesha anaungwa mkono na MABEBERU.

7. Idadi kubwa ya wagombea waliojitokeza ni vijana wa mitaani ambao kwa uzoefu wa chaguzi zilizopita unaonesha huwa hawapigi Kura.

8. LISSU na Chadema inajenga matumaini HEWA ya ushindi kupitia watu waliojitokeza kwenye mikutano yake, ikumbukwe kwamba kwa mujibu wa takwimu za Tume idadi ya wapiga Kura walioandikishwa ni Milion 29, hebu fikiria idadi waliojitokeza wanafiki hata asilimia 5.

9. LISSU ameonesha kushindwa hata kabla ya Uchaguzi kufanyika. Hajiamini anajenga mazingira ya kwamba ataonewa na Mamlaka za usimamizi wa Uchaguzi.

10. LISSU ana Mpango wa kuharibu amani iliyopo chini, anahamasisha Wananchi kufanya fujo wakati wa Uchaguzi kwa kisingizio cha kutotendewa haki.

Kwa namna ambavyo LISSU amejinadi kwenye mikutano yake ni wazi kabisa mgombea wa CCM Mhe Dkt JOHN POMBE MAGUFULI ananafasi KUBWA YA KUSHINDA kutokana na uchapakazi wake, weledi na uzalendo kwa Taifa.
 
. LISSU anatumia muda mwingi kushambulia haiba za wagombea anaochuana nao kuliko Kueleza sera mbadala alizonazo.
Anadi sera zipi keng& wewe kwani kampeni zimeshaanza??

Mnawashwa washwa na Lissu misukule nyie, mlimuandama mbowe sahivi mnalala na kuamka na lissu, eti "kuliko kueleza sera alizonazo" hata hujui kuwa muda wa kunadi sera haujafika, ndorobo ww
 
Nilikuwa sijui kumbe vyombo vya ulinzi vinakazi nyingine ya kuamua Nani awe Mshindi kwenye chaguzi....???
Ana maana hii
tapatalk_1583402596058.jpg
tapatalk_1582299881767.jpg
FB_IMG_1582080397242.jpg
FB_IMG_1583310167549.jpg
 
Mwana wa Tanzania nadhani ingekuwa vyema tusubiri kipenga kipulizwe kipute kianze ndiyo tujue Lisu ana sera au hana. Kwa sasa tume haijaruhusu wagombea ktk vyama vyao kunadi sera zao kwa maana ya kwamba kampeni hazijaanza. Hizo anajaribu kugusia gusia tujue serikali tuliyonayo na Rais tulienae. Mfano hata Democrats marekani juzi katika kupitisha mgombea wao walimchambua Trump kisawasawa na serikali yake.

Sidhani kama ana jazba ila hivyo ndivyo Tundu Lisu alivyo miaka yote na hiyo haimaanishi kuwa atalipiza kisasi, je hicho kisasa atakilipa kwa nani na kwann?

Umesema waudhuriaji wote ni Chadema tu na ni vijana wasiyo piga kura, wewe umejuaje kuwa ni Chadema watupu na siyo wapiga kura? inamaana waudhuriaji wa mikutano ya wagombea wengine ni wazee tu wanaoenda huku wamebeba kadi za kupigia kura jambo ambalo kwa Lisu hujaliona?

Ni dhambi wagombea wakiwa vijana waliotokea mitaani kugombea uongozi katika nchi hii? na hao wa mitaani si ndiyo wapiga kura wenyewe au wao wanatakiwa wawapigie kura wazee wanaotokea angani .

Tumpe muda kampeni zianze kama hana sera atabaki hivyo hivyo wenye sera watashinda kwa kishindo. Tusubiri tuone.
 
Endelea kujifunza na kujifunza na kujifunza utaelimika ipasavyo kupitia Tundu Lissu
 
Back
Top Bottom