Mamba Aiangusha Ndege Kongo, 20 Wafariki

Mamba Aiangusha Ndege Kongo, 20 Wafariki

hii imekaa kimzaha zaidi....inakuwaje usafirishe mnyama bila kujulikana....na alitokaje huko kwenye begi? anyway RIP wote waliokufa but hainiingii akilini....
 
kwa comgo unaweza kukuta hakuwa mamba alikuwa mtu..any way RIP.
 
Evolution is still at work in Africa!
 
Inanikumbusha TRL naikia ugogoni watu walikuwa wanapanda na mbuzi.
Asije ikawa alikuwa Kenge bse mamba wa kutosha kwenye begi ni issue labda kama ana week toka azaliwe.
Sasa kamamba kadogo ako taharuki inatoka wapi?Naona mazoea nakumbuka nikiwa mdogo nshawai mtimua mamba akiwa nchi kavu ila alipofika majini akataka nichenjia nkachapa mwendo.
Kwetu mamba tunaoga nao mbona
 
Snake on a plane anyone?

I am sad about the accident though. Let this be evidence that stupidity kills, you can add this to Darwin Awards at the end of the year.
 
Africa....Africa...ooh Africa. I love it!
 
Mamba Aiangusha Ndege Kongo, 20 Wafariki
5061966.jpg

Mabaki ya ndege iliyoangushwa na mambaMonday, October 25, 2010 2:35 AM
Watu 20 wamepoteza maisha yao nchini Kongo baada ya ndege waliyokuwamo kuanguka toka angani baada ya mamba aliyeingizwa kinyemela ndani ya ndege hiyo kuchoropoka na kuleta kizazaa kikubwa ndani ya ndege.Abiria aliyetaka kumsafirisha mamba wake kinyemela kwa kumficha mamba huyo ndani ya begi na kuingia nalo ndani ya ndege amesababisha vifo vya watu 20.

Ni mtu mmoja tu kati ya watu 21 waliokuwemo ndani ya ndege huyo ndiye aliyenusurika maisha yake.

Kwa mujibu wa abiria huyo aliyeponea chupu chupu kupoteza maisha yake, mamba huyo aliyekuwa amefichwa ndani ya begi na kuingizwa kinyemela ndani ya ndege nchini Kongo alisababisha mtafaruku mkubwa ndani ya ndege na kupelekea ndege kuanguka.

Mamba huyo alichoropoka toka kwenye begi wakati ndege ndogo ya abiria iliyotengenezwa nchini Czech aina ya Let 410 ilipokuwa angani ikitoka mji wa Kinshasa kuelekea Bandundu.

Ilikuwa ni patashika nguo kuchanika wakati mamba huyo alipoanza kuranda randa ndani ya ndege na kupelekea abiria waviache viti vyao kusalimisha maisha yao.

Wahudumu wa ndani ya ndege walikimbilia ndani ya chumba cha marubani na kufuatiwa na baadhi ya abiria ambao nao waliamua kuitumia nafasi hiyo kusalimisha maisha yao.

Inasemekana kuwa ndege hiyo ilianguka toka angani kutokana na uzito ndani ya ndege kuelemea upande mmoja.

Ndege hiyo iliangukia kwenye nyumba iliyopo maili chache toka kwenye uwanja wa ndege ambao ndege hiyo ilipanga kutua.

Mamba aliyesababisha ajali hiyo alitoka salama salimini toka kwenye mabaki ya ndege hiyo lakini aliuliwa kwa kuchomwachomwa na kisu na watu waliojitokeza kuwaokoa majeruhi wa ajali hiyo.
Huko Congo usafiri wa ndege ni kama wa daladala za Mwenge hadi Mbagala,kwenye ndege utakuta imejaa na imesimamisha abiria wakiwa na mizigo lukuki,kwa mtu ambaye umetoka huko East Afrika utashangaa ,na humo ukipanda kila mtu anasali kivyake ,sijawahi kuona usafiri wa hatari na mbovu na usio na sheria za usafiri wa anga kama DRC,hakika tembea uone.
 
Mamba ndani ya bag, Isije ikawa kafara za biashara
 
Back
Top Bottom