Mama yangu hamtaki mke wangu mtarajiwa!

Mama yangu hamtaki mke wangu mtarajiwa!

vickboy.com

Member
Joined
Jul 29, 2013
Posts
85
Reaction score
23
Habarin wandugu,

Nina mpenzi wangu ambaye tulianza uhusiano tangu mwaka 2006 yeye akiwa form 2 wakati huo mm nilikuwa form 3.

Tumekuwa katika uhusiano katika kipindi chote hicho tukiwa serious na shule na tulikuwa shule tofauti japo likizo tulikuwa pamoja.

Walinifahamu wazazi wake na yeye pia kwetu walimfahamu japo hawakujua kama ni wapenzi kwa muda huo, tuliendelea na uhusiano wetu mpaka tulipomaliza shule japo nilimtangulia, niliendelea na shule baada ya kufaulu nikamuacha yeye bado na alipomaliza alienda Kusoma Ualimu grade A.

Alipomaliza Tu nakuajiliwa nikamtia mimba sasa hizi mtoto wetu ana miaka 3, tulipendana sana na msichana wangu huyo, na mama yangu alimsaidia ktk kipindi chote cha ujauzito wake wakati huo mimi nilikuwa chuoni, lakini sasa kawa mkali anadai siwezi kumuoa huyo mwanamke kwa kigezo ni ndugu, na undugu wenyewe ni kwamba, bibi yangu mzaa mama ni dada ake wa babu wa huyu mchumba ambaye ni mzaa baba yake, so sisi ni ndugu.

Anasema tutunze tu mtoto na sio mengine, naumia sana maana tunapendana sana.

Ushaur wenu plz!!
 
huo undugu duh! sikumbuki kama ndugu zake na bibi nawajua!!!
 
acha ungese oa, kule kwetu kuna faini ya kuua undugu, then unatoa mahari unaoa.

Hakuna jambo gumu kama kusaka mke/mme, ukishpata na kumwachia ni ujinga wako.
 
"bibi mzaa mama ni dadake babu mzaa mchumba" huyo anaoleka bila shida bwana!!...undugu upo ila damu zimeshachanganyika Sana...
 
acha ungese oa, kule kwetu kuna faini ya kuua undugu, then unatoa mahari unaoa.

Hakuna jambo gumu kama kusaka mke/mme, ukishpata na kumwachia ni ujinga wako.

nilisha sikia kitu kama hicho
 
"bibi mzaa mama ni dadake babu mzaa mchumba" huyo anaoleka bila shida bwana!!...undugu upo ila damu zimeshachanganyika Sana...

we kabila gani? babu na bibi mtu ni wa tumbo moja, huyo ni ndugu wa karibu sana kwetu. Ngoja nikurahisishie, wewe una dada yako, mtoto wa mwanao anaweza kumwoa mtoto wa mwanae dadaako? hiyo ni family moja, sema siku hizi mambo ya undugu hayapo, hata mjomba anasimamia show kwa mpwa na ni kawaida tu, huo ni uchafu na mbaya kibayolojia! Kwa vile wameshazaa yeye aongee vizuri na mama yake tu, ikibidi aongee na ndugu zake wengine wakubwa, hapo kuna kulipa fine ya kuvunja undugu then wanaowana!
 
nimekupata ndugu, nibora nilipe fain kuliko kumuacha kabisa,,,
 
Wakati kabla hayajakuwa haya ya mpk mmezaa mama yako halikuwa hajui huo uduguu? DNA mkipima mnafanana? Binamu mbona kwa unaweza muoa sembuse huyu bibi ni.......! sioni mantiki we rekebisha mambo labda na wewe kama humtaki tuuu huyo bi dada no enythng else
 
hapo inategemea mila na mila na kwa tamaduni zilizo nyingi tanzania uhusiano wa bibi na babu ni wa karibu. Lakin kuna makabila hawajali sana mfano kuna wengne wanaruhusiwa kuoa binamu zao.
Kupenda umependa lakini mila na desturi ni muhimu sana so fuatilia mila zenu zinasemaje juu ya hilo otherwise utakuja kupata 'Social Rejection' ukilazimisha vitu ambavyo kwa utamaduni wenu haviruhusiwi
 
acha ungese oa, kule kwetu kuna faini ya kuua undugu, then unatoa mahari unaoa.

Hakuna jambo gumu kama kusaka mke/mme, ukishpata na kumwachia ni ujinga wako.

Kumbe waume nao mnatusaka siku hizi? haya ni mapinduzi mazuri.
 
Huo udugu mbona wamakopa wakukutanika pakachani?
sasa mtoto mmezaa lakini kuona hakuna au kuzaanae tena poa lakini kumuoa hakuna?
ebu mueke mzee wako chini mueleze,watu wanaowana baba mkubwa kwa baba mdogo,mtoto wa mjomba na shangazi
seuze huyo kakake babu na dadake babu.....
 
huuu ni uswengele mshazaa kaa na wazee lipa fain fikir madhara ya kubrake relationship....yy kashazaa atapata shida kumpata mume.....mtoto wenu atalelewa na nani??
simama kiume tetea uhusiano wako
 
huuu ni uswengele mshazaa kaa na wazee lipa fain fikir madhara ya kubrake relationship....yy kashazaa atapata shida kumpata mume.....mtoto wenu atalelewa na nani??
simama kiume tetea uhusiano wako

Hiyo faini mbona sijawahi kuiskia?,nifahamishe
 
Tunawasaka indirectly, ndo maana unaweza kuta wamejitokeza watu wanne wanataka kuchumbia lakini hujakubali hata mmoja.

Kumbe waume nao mnatusaka siku hizi? haya ni mapinduzi mazuri.
 
Back
Top Bottom