MVUMBUZI
JF-Expert Member
- Jan 8, 2011
- 5,182
- 2,304
Mama wa kambo si mama,hakuna la kubisha hapo:spider:
Si always, Mimi wife ni mama wa kambo kwa kijana wangu wa ujanani na tunaishi naye sambamba na watoto wetu wa ndoa ,tukitoka tunatoka wote, tukila wote tukienda ibadani wote. Na hata nikisafiri wife ana mtake care kama mtoto wake wa kuzaa na sijawahi sikia malalamiko kupitia kwa bibi, majirani wala kwa baba wadogo au wakubwa. Tulianza kuishi naye tangu O-Level na sasa yuko Higher learning institution na hujisikia comfortable zaidi kukaa hapa nami kuliko kwenda kumtembelea mama yake mzazi.
Kwa hiyo hii ina maanisha nini? ni kwamba mama wa kambo akiwa na hofu ya Mungu na mkakubaliana modality ya malezi bila kinyongo na baba kutokuwa biased basi hakutakuwa na tatizo lolote la malezi. Mtoto anapokuwa chokoraa na kuwa na pre -conception kwamba mama wa kambo ni wabaya basi ataishi ki defensive zaidi hata kama mama wa kambo ana mtreat fairly