Mama wa kambo si mama | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mama wa kambo si mama

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mkwaruzo, Mar 1, 2011.

 1. Mkwaruzo

  Mkwaruzo JF-Expert Member

  #1
  Mar 1, 2011
  Joined: Feb 21, 2011
  Messages: 566
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Ni msemo wa kwanza kati ya miwili nisiyoipenda. Mama wa kambo kama mama (na mlezi) anapaswa kupewa umuhimu wake kutokana na kazi anayoifanya na siyo kumjengea taswira ya ubaya ktk jamii. Mi naona ubaya wa mama wa kambo unaanzia ktk consept zetu mbaya juu yake hivyo kuyapindisha hata yale anayoyafanya kwa nia njema akiwa kama mlezi husika kwa wakati huo, mfano kumrudi mtoto kwa kosa alilofanya.
  Msemo wa pili nisiyoupenda ni huu unaosema 'mtoto usiyemzaa ni mkubwa mwenzako'. Baada ya msemo ambao umekuja kumtia ila mama wa kambo, umekuja na huu unaomfanya asiupe umuhimu wajibu wake na pindipo akisibiwa na msemo huu, ndiyo ubaya wa mama wa kambo unapojitokeza. Mfano mtoto anapokosea, atampa adabu isiyoendana na uzito wa kosa na hata isiyo sawa na yule anayepewa.
  Kwa maelezo hayo, hebu tuangalie ubaya wa mama wa kambo ulipo na ni sababu zipi zinazompelekea awe hivyo.
   
 2. Maty

  Maty JF-Expert Member

  #2
  Mar 1, 2011
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 2,170
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Mimi yote tisa kumi hapo wanaitumia sana hii misemo wapenda serengeti boys kisa mtoto huyo si wake watu wamepinda sana
   
 3. Sita Sita

  Sita Sita JF-Expert Member

  #3
  Mar 1, 2011
  Joined: Aug 25, 2008
  Messages: 1,196
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  hormones zinawasumbua, mbona hatusikii cases za baba wa kambo
   
 4. Desidii

  Desidii JF-Expert Member

  #4
  Mar 1, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 1,212
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Huo ni ukosefu wa akili na adabu mama wa kambo si mama?? Ujinga mtupu.
  Ushapitwa na wakati huo msemo watu wanalelewa na mama wa kambo na huwezi kujua kama si mama yake aahhh
   
 5. Mkwaruzo

  Mkwaruzo JF-Expert Member

  #5
  Mar 1, 2011
  Joined: Feb 21, 2011
  Messages: 566
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kwa vile tittle imetokana na msemo, acha nitumie misemo zaidi.
  "kulea mimba si kazi, kazi kulea mwana". Kama ni hivyo, inakuaje mama wa kambo awe sura awekewe taswira mbaya ilhali anayotokea kuyafanya yeye, pia yanafanya na mama wazazi pengine kwa kiwango zaidi ya kile alichokifanya m wa k. Mida nitakuja kueleza hali fulani...
   
 6. Mkwaruzo

  Mkwaruzo JF-Expert Member

  #6
  Mar 2, 2011
  Joined: Feb 21, 2011
  Messages: 566
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Inaweza kuwa inachangia....
  Kuna hii tabia ya mume kumjibu mke wake majibu ya ovyo mbele ya watoto wake. Au kuonyesha yuko upande wa watoto zaidi kuliko kwa mama. Au kuwa mkali pale watoto wanapoleta kesi dhidi ya mama yao bila ya kutanguliza uchunguzi juu ya kile alichoambiwa. Hivyo mambo hayo hutoa fursa kwa watoto ya kutokumpa heshima inayostahiki mama yao wa kambo. Hivyo huanza kumfanyia vituko mama huyo. Pia inaweza kuwa inawapitia moyoni mwao au hata kuibainisha kauli hii "bila ya wewe, hata mama yetu asingeliondoka humu"
   
 7. T

  Tasia I JF-Expert Member

  #7
  Mar 2, 2011
  Joined: Apr 21, 2010
  Messages: 1,226
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  nahisi we ni mama wa kambo, anyway naeza kua rong. huyu ni mlezitu, na labda hyo sifa ya mama imekaa kijamii zaidi lakini sio ki-sense ya mama. ni kama shangazi, mamdogo, dada wanavyolea.basi nao waitwe mama wa kambo.ukisema kwakua analiwa na faza basi hata mahawara zake wengine nao wawe maza.
   
 8. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #8
  Mar 3, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Mama wa kambo ni mama nae ila watu washajenga mtazamo hasi. Inapotokea anamwadhibu mtoto ataonekana anamnyanyasa. Yaani sijui wafanye lipi jamii iwaelewe ingawa wapo wengine nao watata sana.
   
 9. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #9
  Mar 3, 2011
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,773
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Sio lazima awe mama wa kambo ndo akutende vibaya, mie nimeishi na mama mdogo kwangu ni sawa na mama kambo!!!
   
 10. Keren_Happuch

  Keren_Happuch JF-Expert Member

  #10
  Mar 3, 2011
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 1,880
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Ni kweli imekuwepo misemo ambayo labda inapelekea hizo tabia za mama wa kambo na huyo mtoto wa kambo. Ninaelewa kuna kazi kubwa sana kumlea mtoto ambaye sio wako, hasa linapokuja suala la kumwadhibu, maana siku zote itaonekana unamuonea. Lakini nafikiri jukumu kubwa liko kwa mama. Akimpa upendo yule mtoto, hakika hapatakuwa na tatizo kabisa. Na kama huyo mama ana watoto wake, basi inabidi kutokuwa na ubaguzi wa aina yeyote kati ya watoto wake na hao wa kambo. Tatizo wamama wengi hawawaonyeshi watoto wale upendo, wakati watoto wale wanahitaji sana upendo wa mama.
  Ukitoa upendo, utapokea upendo pia!
  Usku mwema.
   
 11. s

  shosti JF-Expert Member

  #11
  Mar 3, 2011
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 4,949
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Mama wa kambo si mama,hakuna la kubisha hapo:spider:
   
 12. S

  Slm Senior Member

  #12
  Mar 3, 2011
  Joined: Jan 26, 2011
  Messages: 103
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  nani kakuambia mama wa kambo ni mama ila tu sio mama mzazi. Hii huwa inategemea mtu na mtu, kama mwanamke huyo anarohombaya na uchoyo atafanya hivyo hata kwa step chidren wake na kuwajari wa kwake tu
   
 13. 22nd

  22nd JF-Expert Member

  #13
  Mar 3, 2011
  Joined: Aug 1, 2010
  Messages: 498
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  mmesahau mashangazi, hawapendi sana watoto wa kaka zao, sijui kwanini.
   
 14. s

  shosti JF-Expert Member

  #14
  Mar 3, 2011
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 4,949
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  sijaelewa labda kwa kuwa natumia kibatari:rain:
   
 15. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #15
  Mar 3, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  kweli. Kama shangazi zangu mimi....mmh!
   
 16. Mkwaruzo

  Mkwaruzo JF-Expert Member

  #16
  Mar 3, 2011
  Joined: Feb 21, 2011
  Messages: 566
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  kwanza mm siyo fimel. Kama alivyosema hosninyo kuwa wapo mama wakambo watata ila asilimia kubwa kati yao hutiwa utatani kwasababu ya dhana tuliyokwisha jengeka nayo.....
  dada, mamdogo, shangazi wanaweza kuwa ni walezi kama alivyo yy ila wao hawapewi mzigo wa kasumba kama anavyozipata yy. Wala kuitwa mama hakuna umuhimu ila muhimu ni kupewa afueni.
   
 17. S

  Slm Senior Member

  #17
  Mar 3, 2011
  Joined: Jan 26, 2011
  Messages: 103
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  May be.
   
 18. s

  shosti JF-Expert Member

  #18
  Mar 3, 2011
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 4,949
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  hahahha unanikumbusha mbali sana mpendwa,halafu sasa wanabeep kutwa ukipiga wanakuambia tunakutegemea mwanetu wanalamba matapishi yao pambafu wakubwa na wanataka uwape sawa na mamako mi huwa nawajibu kwa kuwaonyesha vidole tu kama viko sawa mtakula sawa na mamangu:rain:
   
 19. Mkwaruzo

  Mkwaruzo JF-Expert Member

  #19
  Mar 3, 2011
  Joined: Feb 21, 2011
  Messages: 566
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  any way, mbaya kwako mzuri kwa mwenzako...
   
 20. Da Pretty

  Da Pretty JF-Expert Member

  #20
  Mar 3, 2011
  Joined: Dec 9, 2010
  Messages: 3,050
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Na tunakoenda kila ndoa mpya mke anaenda kuwa mama wa kambo!
  Mungu atusaidie wanawake,atupe hekima na roho ya upendo
  tuweze kuwalea kwa mapenzi hawa watoto waliozaliwa kabla
  ya ndoa maana sio kosa lao na kama wazazi wangekua makini
  na kurekebisha makosa huenda hii ndoa isingekuwepo!
  Naamini mtoto akilelewa kwa upendo amani itakuwepo
  LAKINI
  Mtoto kulelewa nyumba mbili mara kwa mama mara kwa baba hapo
  ndipo zinapoanza chokochoko na kutafuta kasoro za mama wa kambo!
  Mara ananitesea mwanangu na maneno kibao wakati ukweli
  upo wazi.
  Mimi sio mama wa kambo ila nina ndugu zangu waliolelewa na
  mama yangu. Tunamshukuru Mungu tunaelewana na tunashirikiana vizuri
  hata na watoto wengine wa mama yao (marehemu)
  na wasiotujua hawaoni tofauti.
   
Loading...