Mama wa kambo kashaniendea mara mia moja kwa waganga wa kienyeji ili Mzee asinijali, anisahau

Dogo tafuta pesa ili watoto wako uwalee,umeshakuwa mtu mzima kukofoleavya wazazi utakufa mapema ukiwa umesimama.

Baba yako angekodolea Mali za babu yako usingekuzaa wewe.
Mtoto kwa Mzazi akui Boss
 
Uvivu wako na kupenda raha ndo kunakutesa, mtoto wa kiume pambana tengeneza vyako usipokuwa makini utakuwa mwehu.
Mkuu Mimi Fighter sipo hivyo kama unavyofikilia
Au wee ni walewale nini? Acheni Roho ngebe nyie Mama wa kambo
 
Nimelelewa pia na mama wa kambo, wengi wao wana roho mbaya.

Nilishawahi kufikia hatua ya kuacha kuongea na mzee wangu ila Mungu ni mwema hayo matatizo yaliisha na mzee akaanza kunikubali.

Nilikuwa nakaa home ila Mzee akanichana live, nijikatae si ubaya lakini....

So mkuu kama na wewe unaishi hapo ni bora uondoke tu, uende ukaishi na washikaji zako tu huko maghettoni kisha maisha yataanza mdogo mdogo kujipa.

Be a man, upunguze kulalama.
 
mtoa mada inaonekana we ni mshirikina maana hata hujatounyesha huyo mama kaenda lini kwa waganga na ulimuona au vp ila umeconclude tu
Ila mkuu moderetor ndiyo wameiweka Title hivyo Mimi sikuandika hivyo ila hayo maelezo waliyowka Mods niliweka ndani ya Uzi.
 
Mkuu Hii Dunia huijui vzuri subiri ukue kidogo
 
Nimefanya hivyo mkuu lakini huyu mam Kila nikienda pale vijembe haviishi
 
Amini tu MUNGU,ipo siku atakuvusha,ikiwezekana hama nchi uone vitu vipya na ufute memory mbaya.
Pole sana.
 
Hii changamoto tupo wengi, ushauri muhimu ni kuzingatia na kutilia maanani masuala yanayohusu mustakabali WA maisha yako.

Jiweke mbali kabisa na mbaya wako/mnafiki wako hata aoneshe kukujali vipi.

Usinisumbue kuuliza kuuliza chochote kuhusu mabaya anayokutendea au kujaribu kitafuta suluhu na badala yake potezea na kujifanya kama hujali yanayoendelea.

Kamwe usikwazike na mabaya anayokutendea yeye hata familia yake na badala yake mabaya Yao yakupe hasira za kupambana zaidi na maisha.

Kitendo Cha wewe kufanya yote hata kutamfanya mbaya wako kuwa na sintofahamu ya ama amefanikiwa au ameshindwa kukuangamiza na hata kuhisi pengine maisha yako yamefanikiwa zaidi tofauti na ambavyo angetamani uanguke.

Hali hii itapelekea kukuogopa na pengine kuhisi kwamba wewe ni mchawi zaidi yake jambo ambalo litampa sintofahamu na Kimnyima usingizi daima.



Muhimu: Endapo unaishi karibu Nate ondoka kabisa na ukiendelea kua karibu Naye vita itakua kubwa zaidi kadiri siku zinavyosonga.
 
Ahsante mkuu kwa hiki ulichokiandika, Nitakifanya kazi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…