Mama wa kambo kaniharibia kila kitu

Huyo mama sio mama yangu mzazi baada ya baba kuniacha alikua kidogo ananisaidia za matumizi ikafika muda nikipiga simu ananambia utajua utakachofanya
 
Kwa hiyo hukushirikishwa wakati wa ugawaji mali? Baada ya msiba kumalizika hamkukaa kikao kujadili suala la mirathi? Nani alichaguliwa kusimamia mali zilizoachwa na marehemu?
Mkuu inasikitisha sana muda wote mimi akili haikuwa katika kufikiria mirathi japokua kikao kiliwekwa na mama wakambo alichangia hoja akisema nimadeni mengi yalibakia ivo mali nyingi kufidia madeni na mama wa kambo akiwa kama anajua kila kitu
 
Mkuu idea yako ni nzuri ila kumbuka kuna watu wakigundua ni mtu flani hufurahi kwa kushindwa kwako na inakua tangazo kwa kila wanaomfahamu au kumuona, sio kila mtu ni mzuri kwako mkuu
 
Mkuu yeye ndio alitengwa japo alikua akisaidia sana upande wa pili
 
Alikua na mwanamke akawa kaachana nae zamani ambapo tulibaki nababa na ndipo akawa na mwanamke mwingine ambaye ndio mama wa kambo na mambo yake yote alikua akijua mama wa kambo
 
Nenda kwenye vyombo vya sheria au kwa mfumo wa sasa piga shortcut nenda kwa mkuu wa wilaya au mkoa.

Angalizo:Utakapofanikiwa heshimu mali za mzazi wako ziendeleze miaka mitano ijayo watu watataka mrejesho.
mkuu ninavyoongea hapa hakuna kilichobaki na mama wa kambo aliniambia nitajua mwenyewe
 
Vilikua tayari chini yake mkuu
 
Huyo mama sio mama yangu mzazi baada ya baba kuniacha alikua kidogo ananisaidia za matumizi ikafika muda nikipiga simu ananambia utajua utakachofanya
Mkuu Path Creator hutakiwi kurudia kila comment yako habari ya mama wa kambo,mwandiko wako unanionyesha kuwa unajificha kwenye mwavuli wa mama wa kambo sana.

1.mam yako wa kambo aliwezaje kujimilikisha mali bila kikao cha familia au hata wazee wa ukoo❓

2. Unasema baba yako aliwekeza kwenye elimu sana,sio,ni elimu ipi aliyoiwekeza❓

3. Wewe ni mtoto halali wa marehemu huyo baba❓

4. Unasema kuwa mama yako alianza kukubadilikia baada ya kuanza kuhangaikia mirathi sio!uliangaikia kwa namna ipi❓

5.kuna mkuu fulani hapo juu amejaribu kukuvuta akusaidie lakini kulingana na unavyocomment 💯 huonyeshi ushirikiano ipasavyo kwanini❓

6. Mpka umefikia hatua ya kwenda chuo maana umeshavuka umri wa kuwa mtoto,kwanini baba yako hakukupatia japo urithi ikiwa wewe ni mwanae?❓

7. Kama baba aliwekeza kwenye elimu,kwenye Bank ac kuna shilingi ngapi ya kuweza kukuendeleza kielimu❓

8. Ina maana kwenye ukoo wenu marehemu alikuwa hapatani na ukoo mzima kisa kupenda kwake elimu❓

9.kwahiyo nyie mlikuwa hamna japo ndugu mmoja ambae alikuwa anawatembelea na nyie mnamtembelea❓

Natamani kutichape bakora kidogo kustua akili yako itoke huko ilipo😅😅maana unatoa majibu mepesi kwenye maswali magumu.

JF ni kubwa hii na inawatu wakubwa wengi ila huwezi kuwajua wengine kwa ajili ya fake idz.ondoa ukakasi katika mwandiko wako upate msaada kijana.sentensi zako zinapwaya sana.

Pole kama mwandiko wangu hauonyeshi yale uyategemeayo.jibu maswali niliyokuuliza tafadhali.

Poleni kwa gazeti na kutokupangilia vizuri maswali🥂
 
Yaani mambo ya mirathi siku hizi, hakuna namna ya msimamizi kudhulumu warithi kama mali zote za marehemu zinajulikana. Huyo mama yako wa kambo hawezi kukudhulumu hata kidogo kama mkienda kufungua kesi ya mirathi mahakamani. Lakini kama utazembea mambo yaendeshwe kimila hiyo ni shauri yako maana mm mila zenu sizifahamu. Lakini ukienda kisheria haki yako utapata.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acha kuhuzunika kisa Mama wa kambo hiyo situation ikupe nguvu za kufight!..yaan tumia huzuni zako kupambana..tena utafanikiwa .yaani huu muda unaotumua kulalama anza kuchora ramani unachomokaje! Kila siku chora ramani yako ya maisha...ukikosea rekebisha... Najioneaga uvivu kabisa kusikia mtu analia lia kisa mirathi .eish!
 
Mkuu nimeona maswali yako yote na jibu ni kwamba tayari vilikua vimeandishwa chini ya mama wa kambo, kama mtu yuko willing kunisaidia nitamletea yote anayohitaji naku abide maelekezo yake
 
Idea nzuri mkuu ila mimi hapa saiv chuo nimestop kwakukwama ada, kodi sina nishaambiwa niondoke na pakujishikiza wala kunishika hakuna
 
Umemuuliza maswali mazuri sana, ambayo hata mimi nilijiuliza lakini nikaona kwa kua yupo chuo basi asome amalize elimu yake,

Nimemwambia nitakulink na mtu na huyo mtu niliongea nae jana ile ile, ajabu mwenye tatizo hajanitafuta mpaka sasa,

Sasa sijajua anahitaji msaada gani au alitaka aambiwe weka namba tukuchangie na hapo bado angeona ugumu, fatilia kisheria anasema mambo ya jadi sijui mila na desturi, ni zipi hizo hasemi,

Vijana wa sasa hivi wanachukulia mambo kiwepesi wepesi sana, hawajui penye wengi pana mengi.
 
Idea nzuri mkuu ila mimi hapa saiv chuo nimestop kwakukwama ada, kodi sina nishaambiwa niondoke na pakujishikiza wala kunishika hakuna

Kashitaki kwa mwenyekiti...! Fika nazi za mbele ikiwezekana mwone diwani wako..amka upambane! Na kwann ulijitune kupata urithi?
 
Mkuu nimeona maswali yako yote na jibu ni kwamba tayari vilikua vimeandishwa chini ya mama wa kambo, kama mtu yuko willing kunisaidia nitamletea yote anayohitaji naku abide maelekezo yake
mim tangu primary mpaka chuo nilikuwa nalelewa na mama wa kambo,naomba nikushauri kitu mkuu..wewe mtoto wa kiume acha kulalamika saana mzee dunia hii apo ulipofika pambana upate chako marehemu hufa na chake ata ukipewa hizo mali kama hauna moyo wa kutafuta chako zitakufa zote.pili,baada ya baba kufa kama wewe ndo ulianza kuulizia mali basi jua bi.mkubwa kashakujua wew una tamaa hauna moyo wa undugu fanya jua mali zetu zipo ila ondoa swala la kuonyesha kutaka kugawana endelea na maisha mengine.mm nilikuaga sielewani nae kabisa nikiwa na mawazo kama yako nikitaka tugawane nyumba ziizopo na mali zingine ila nikashauliwa na mwanaume mmoja..sasa hivi bi mkubwa ata akisikia mwanangu anaumwa anakuja faster kumchek na maisha yanasonga kama mtu na mwanae mzazi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…